Tuna cha kujifunza kutoka CHADEMA

Tuna cha kujifunza kutoka CHADEMA

Umeshindwa kuficha mapenzi uliyonayo juu ya CHADEMA.

MSALANI kila siku kwenye LB7 caucus pale Lumumba tunasema jadili hoja na siyo eti mleta hoja ana mapenzi na CDM.
Kwa mtindo huu tutapokea hiyo Ipad ya chama tumpe hata Doto Rangimoto manake wewe umeshindwa kazi.
Kumbuka boss wetu alishasema
Dawa yenu watu wa aina ya ifweero na MSALANI,ni kuwafungia ID zilizofunguliwa na chama tu. Hamtetei chama badala yake mnaweka mbele matusi,kejeli,fitina na maneno ya maudhi. Operesheni iko njiani. Mtaingia na vi-ID vyenu muda si mrefu. Jifunzeni kujadili hoja na si mleta hoja.Ndivyo mnavyoambiwa chamani. Hamsikii.Dawa yenu iko jikoni

Mzee Tupatupa

au hukusoma?
 
Last edited by a moderator:
Ilani ya chadema ilikuwa ni kuhakikisha kuwa nchi haitawaliki labda hujui vema unachokisema.

Ata kama Chadema ni dhaifu lakini CCM ni mfu kabisaaa.na mnaopotosha umma subirini hukumu yenu nchi imegawanywa wachache wanafaidi na familia zao.wananchi wanakufa na shida .maish mabovu mnawaza wizi tu.

We ni mtu mzima naamini unajua nchi imefikia pabaya kwasababu ya vingozi wa ccm kukumbatiw a na chama kufanya maovu.katika mikataba na biashara haramu.damu za watoto wenu zitawahukumu.

kwahiyo kulinganisa mabaya ya chadem na mabaya ya Ccm ni uhayawani.najua umenielewa kama mmeshiba achia nchi ata itawaliwe na jeshi but Ccm no.

Huo uchaguzi wenyewe mnatumia hila kushinda kama mko makini kwanini msi tumie haki kwenye uchaguzi muone kama mtashinda.
 
Chadema tumekwenda kwa hatua zote muhimu za ukuaji wa chama toka mwanzo mpaka tunachukua nchi 2015,ina wanamikakati,wanamaono,wajenga hoja mpaka wanamipango kuhakikisha kila hatua moja inazaa hatua nyingine kwa mpangilio wa mambo na matukio.Hili ndilo jambo linalowafanya watanzania kuyakumbuka maneno ya B.wa Taifa ya kwamba Chadema ndo chama kinachoonekana kuweza kujipanga kupewa nchi na sasa mipango ndo hiyo.Karibu sana mzee wa lumumba na karibu CDM

Ndoto za mchana kweupeeee!
 
Huyo Mwehu mwenzenu Tupa
tupa anafahamu napatikana kona ipi katika jiografia ya nchi hii? Au
anapiga porojo tu kuwafurahisha?

Acha kujifagilia wewe!? tunakufahamu vizuri, si umepanga chumba kule Arusha Ngalelo pale soko mjinga kwa bibii.
 
Unaijua vema ilani ya cdm au unabwatuka 2!sera za elimu bure(ambayo mlisema haiwezekani lakini jk akaja kusema wanafikiria kufanya hvyo),katiba mpya(haikuwemo kwny ilani ya ccm bali cdm)
 
Unaijua vema ilani ya cdm au unabwatuka 2!sera za elimu bure(ambayo mlisema haiwezekani lakini jk akaja kusema wanafikiria kufanya hvyo),katiba mpya(haikuwemo kwny ilani ya ccm bali cdm)

Chadema mmetekeleza kipi hadi sasa????
 
Nyuma ya chadema kun watu makini na wengine wapo maeneo nyeti serikalini.mtadharau lakini watu washachoka na siasa za Ccm.
Nikiona mtu anashabiki Ccm namtoa akili.Chadema yaweza kuwa dhaifu san but Ccm inahitaji marekebisho ambayo akuna kiongozi wa kuyafanya ili irejeshe sifa zake.kilichobaki pale ni kutumia chama kuficha uharamia wa viongozi.
 
Na hata hivyo si mbaya kuwapenda CDM, ikiwa wanapendeka. Hakuna sabbau ya kueneza chuki bila ukweli. Na ya kujifunza CHADEMA siyou hayo tu aliyoyataja hapo juu. Sera zao zimeenda shule. Kama unavyowakubali kimoyo moyo, ccm wote wanakubali sera za CDM kimoyo moyo. Hawawezi kusema kama ulivyotaka kumhukumu mzee Tupa tupa kwa kuufungua moyo wake.

CDM walikuwa na agenda ya kusimamipa unadishi wa katiba Mpya, ccm wamekurupuka kudandia hoja bila maono, imewashinda. Somo la kujifunza.

CDM walikwa na agenda ya serikali kugharimia Elimu, ccm wakasema uwongo haitekelezeki.. Leo wanazungumzia nini? Somo lingine.

CDM walikua na sera ya ujenzi wa nyumba kwa gharama ndogo..ccm wakasema haliwezekani... Leo nini wanasema? Somo lingine.

Na wewe unaonyesha kutoridhishwa na upenzi wa Tupatupa kwa CDM hata pale walipofanya vizuri...."Kumbe mnaendekeza sizitaki mbichi".

CCM kudandia hoja za CDM, ni kuzikubali moyoni na kuzikandia hadharani ni ulaghai na kujiondolea sifa ya ukweli na uaminifu ambavyo hata hivyo ccm tayari hawana.

Sisi tusio na vyama, tunaangalia na kutathimini kila linalofanyika na vyama vyenu. Tunafahamu mbichi na mbivu na sasa kilichobaki ni kutangaza sifa za kila chama ili makosa yaliyotufikisha hapa yakome..

Mchana mwema!.

Umeshindwa kuficha mapenzi uliyonayo juu ya CHADEMA.
 
  • Thanks
Reactions: mpk
Tangu MM ameenguliwa Chadema kumetuli maana zingekuwa enzi za MM basi ni makundi, Siri za chama kuvujishwa hata matokea tungeletewa hata kabla ya upigwaji wa kura kuisha... Hakika MM alikuwa ni sumu kwa Chadems
 
hivi kwa akili yako una waza kweli chadema kuchukua nchi 2015? kwa mgombea Urais yule babu yenu Slaa?

Chadema ukienda makao makuu wanadanganyana sana! Utasikia njia ya Urais nyeupe kabisa 2015,dr slaa atapita bila kupingwa! Kweli gongo na bangi ni mbaya sana!
 
Ninapata shida sana kuamini kwamba kumbe hapa JF tuna mchanganyiko mkubwa sana wa watu. Hivi kumbe Hansard hata huna uelewa hata kwa kujua tu kwamba chama tawala ndicho kinawajibu wa kufanya maendeleo kwa sababu nicho kinachooongoza nchi na kwamba ndicho kinakusanya na kutumia kodi zetu vile kinavyotaka na ndicho chenye access na uwezo wa kuingia mikataba ya kitaifa kwa maslahi ya nchi?

Unahoji CDM wanatekleza sera gani, kwani wanakusanay kodi? Wameunda seriakli hadi uhoji ufanisi wao?

Ukitaka uwaone makali yao, subiri mwakani.

Masikini. Kumbe tunapoteza muda kubishana na fahamu za kiwango hiki? Hata hivyo nimeelewa, twende tu, utaelewa ila uache ubishi uwe unauliza maswali ili upanue ufahamu!.

Chadema mmetekeleza kipi hadi sasa????
 
Chadema ukienda makao makuu wanadanganyana sana! Utasikia njia ya Urais nyeupe kabisa 2015,dr slaa atapita bila kupingwa! Kweli gongo na bangi ni mbaya sana!

hahhahaah mabwege kweli urais watausikia tu slaa mwenyewe ana stroke!
 
Hata kama ni wapinzani wetu,mazuri yao tutayachukua.Ima kwa kuwaomba au kuyafanya tu na wao wagutuke baadaye. Kwenye chaguzi za CHADEMA zinazoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City, CHADEMA inatufunza mambo mbalimbali ya kidemokrasia. Wametulia;wamejipanga na wanapendeza. Kuanzia maandalizi ya nje ya ukumbi;ukumbini na luningani. Na hata fulana na kofia zao. Tutajifunza kwa maboresho yetu.

Kuanzia Baraza la Wazee; BAVICHA na leo hii BAWACHA,CHADEMA wamejipanga na wakapangika. Intelijensia huru imeshindwa kuona mikutano mbalimbali ya kificho nje ya Ukumbi rasmi inayolenga kupanga takrima au mshikemshike wa hapa na pale. Mbabe wa sera na sura huonekana Ukumbini (Ukumbi rasmi wa mikutano). Kambi za wagombea mbalimbali huishia mlangoni ili kuwapa wasio na kambi muda wa kutafakari sera na sura za wagombea wao.

Hadi kufikia leo, hakuna hata mgombea aliyekimbilia kwa waandishi wa habari kulalamikia ukiukwaji wa sheria na kanuni za kichama. Kila mmoja anamuamini aliyeshinda na kuapa kupambana naye kwa hoja uchaguzi ujao. Mipango ya CHADEMA isitutishe wapinzani wao ila itufunze. Tukubali kuchukua angalau utulivu na umeremetaji wa ukumbi na wanaukumbi katika vyama vyetu. CCM yangu isibaki tena nyuma. Ichote mema ya CHADEMA.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

mkuu hapo hakuna ubishi laziama tukubaliane chadema wako makini sana
 
CC Ifweero, Ritz, Lisbon, Bethlehem, et al
 
asante sana mkuu , ila sitashangaa ukishambuliwa na ID ZA CHAMA CHAKO ULIZOSHIRIKI KUZITENGENEZA .
 
Usibishane na wehu kaka yamevurugwa cku nyingi,ukiona mtu anasifia ccm,kama ni ndugu yako kaa nae mbali maana hao vichaa.
 
Back
Top Bottom