Tumwamini nani matokeo ya kidato channe? TBC1, ITV au StarTV?

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
47
Taarifa za saa 2 usiku huu toka Televisheni za TBC1, ITV na StarTV zinapishana. Pamoja na kwamba, kimsingi, ITV na StarTV wanaonyesha kuwa ufauru umeshuka (StarTV wanaonyesha ~ 22%, ITV kadri ya 50%), TBC1 wanaonyesha ufauru umeongezeka. Kama mimi sijaelewa, naomba mnisaidie jamani. Sasa uchakachuaji hadi kwenye matokeo jamani?
 
Mkuu ni kama darasani tu mwalimu ni yule yule lakini matokeo ya madenti lazima yatofautiane, wengine wanasinzia darasani, wengine wanatoroka wengine ndo kuangalizia. Ndo siasa za bongo uchakachuzi dunia nzima!
 
Kama ni kweli basi Huu ni upuuzi, wanachakachua kwa maslahi ya nani? Taarifa si inatolewa na baraza la mitihani kupitia wizara ya elimu? Tena kwa maandishi
 
ahahaa ina maana tbc watoro
 
Tbc watoro kweli,haiwezekani itv waseme kiwango kimeshuka kwa kadri ya 50percent yani mishule ya kata wanayojivunia imekuwa less productive ,kiukweli kabsa mitoto imefail na chanzo cha yote ni kuwa na kaka mkuu asiye na elimu,mwenye doctorate za uchakachuaji....Doctarates 5 looh ?
 
Halafu kufauru kunakoongelewa hapa ni Div4. Kwa hiyo waliofeli ni wale waliopata Div0, yaani kadri ya 50%...hii haitishi tu, inatisha na kutikisisha.

Nasikia pia waliofeli hawaruhusiwi kurudia mitihani kwa utaratibu wa kurudia masomo unayotaka...kama ndivyo, hawa ndg waliofeli, watafanya nini? Wataajiriwa wapi amabko hawahitaji kufauru?
 
eti waliopata division 1 mpaka 3 ni asilimia 11 tu, hao ndo wenye uwezo wa kwenda 4m5,,,sasa wajameni, taifa linaelekea wapi ndugu zanguni?? Hawa asilimia 89 waliofeli, si ndo wanauchungu kabisa na wapo tiyari kufanya kama tunisia??
 
Tunisia???? May be!
 
Taarifa za saa 2 usiku huu toka Televisheni za TBC1, ITV na StarTV zinapishana. Pamoja na kwamba, kimsingi, ITV na StarTV wanaonyesha kuwa ufauru umeshuka (StarTV wanaonyesha ~ 22%, ITV kadri ya 50%), TBC1 wanaonyesha ufauru umeongezeka. Kama mimi sijaelewa, naomba mnisaidie jamani. Sasa uchakachuaji hadi kwenye matokeo jamani?

Ukweli ni kuwa wote ITV, Star TV na TBC1 hawakutoa analysis iliyosahihi. Ukweli wenyewe ni kuwa kiwango cha ufaulu wa kidato cha nne 2010 ni asilimia 50.74 kwa maana hiyo waliofeli (Division Zero) ni asilimia 49.26. Ila ukilingatinganisha na matokeo ya mwaka 2009 kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia karibu 20. Manake 2009 ufaulu ulikuwa ni asilimia 68 na kufeli asilimia 32. Tafakali!!!!!!
 
Ifike mahala matokeo yawe yanabandikwa kwenye mbao za matangazo kama jinsi matangazo ya shule yanavyotangazwa. Kila shule inayotangaza mabango ya kutaka wanafunzi, ipewe na masharti ya kutangaza matokeo ya kila mwaka kwenye mbao za matangazo na TV kwa muda uleule wanaotangaza matangazo ya kujinadi.....
 
tbc naona sasa wanataka kuwa ki ushabiki zaidi wakati ni shirika la umma. Wanadanganya ili kumfurahisha nani hasa?! :coffee: :faint: :car:
 
Taarifa za saa 2 usiku huu toka Televisheni za TBC1, ITV na StarTV zinapishana. Pamoja na kwamba, kimsingi, ITV na StarTV wanaonyesha kuwa ufauru umeshuka (StarTV wanaonyesha ~ 22%, ITV kadri ya 50%), TBC1 wanaonyesha ufauru umeongezeka. Kama mimi sijaelewa, naomba mnisaidie jamani. Sasa uchakachuaji hadi kwenye matokeo jamani?
Watangazaji na waandaji wa vipindi wote vilaza ndio maana wanatofautiana. Wanajiongelea tu sidhani kama wanafahamu hiyo 22% imepatikana vipi.
 
Kama ni kweli basi Huu ni upuuzi, wanachakachua kwa maslahi ya nani? Taarifa si inatolewa na baraza la mitihani kupitia wizara ya elimu? Tena kwa maandishi

Hiyo si shirika la serikali kwa hiyo wanachakachua kwa masrahi ya wakubwa zao
 
Unajua kama ukipata taarifa za kwenye magazeti zitakusaidia kujua mkweli ni nani. Ngoja nikanunue na niakuelezeni baadaye
 
Gazeti gani kwani anatakiwa anunue?ha ah ahaaa

Yapo magazeti mengine ndg, kwayo ukweli ni nadra!! Yanaeleweka. Hata ukitaka kulichukua, lazima kwanza uangalie kama hakuna watu wanaokuzunguka, au wanaokuona. Ni kama unachukua vitu fulani dukani!
 
tehe tehe si ungeyataja na wengine tukayajua!:madgrin:
 
tbc naona sasa wanataka kuwa ki ushabiki zaidi wakati ni shirika la umma. Wanadanganya ili kumfurahisha nani hasa?! :coffee: :faint: :car:

Nasikia kufeli kwa wanafunzi kunatokana na wanafunzi kukosa molari ya kusoma...sasa sijui ni kwa nini wamekosa molari. Gazeti moja la leo limeripoti! Ama kweli TZ. Yaani 50% kupata Div0 ni MAAFA MAKUBWA kwa Taifa.
 
Mi nahisi kuna wanafunzi wengi hawakuwa sawasawa kisaikolojia wakat wa kujiandaa na hii mitihani. Walikuwa na tension kubwa sana, waliona hii mitihan kama tukio la kutisha sana ktk maisha yao. Isitoshe wengine waliathirika kwa namna moja au nyingine na pilika pilika za uchaguzi mkuu wakajikuta wanapoteza muda wao ktk kampeni badala ya kusoma. Na isitoshe wengine walikuwa wanajaza FULL MATUSI YA NGUONI ktk karatasi ya majibu. Inasikitisha sana na ndio mwanzo wa hawa vijana kuwa majambazi, machanguoa n.k.
Nimekuta huku mitaani wakilalamika eti bora hiyo miaka mi4 angekuwa anatengeneza kimtaji kwa kuuza karanga
Its very sad
 
Back
Top Bottom