Matokeo ya kidato cha nne, shule zifuatazo zimenivutia

Barnabas Mashamba

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
503
1,435
WanaJF

Kwanza nianze kwa kusema ya kuwa, nimefanikiwa kufika kwenye shule mbalimbali nikiwa kwenye harakati za kusaka tonge.

Shule hizo, nyingi nilizifikia mwaka wa masomo wa 2020 na 2021.

Kiufupi, nilifikia shule kwa orodha ifuatayo.

Wilaya ya Geita
1. Halmashauri ya wilaya ya Geita vijijini - sikufika shule 1 tu.
2. Halmashauri ya mji Geita - Sikufika kwenye shule 3 pekee.

Wilaya ya Mbogwe
Sikufika shule 3 pekee.

Wilaya ya Bukombe
Nilifikia shule 6 pekee.

Wilaya ya Kahama
Shule zote za halmashauri ya Ushetu na 2 pekee za manispaa ya Kahama ndizo nilizifikia.

Wilaya ya Kaliua
Nilifikia shule zote.

Wilaya ya Urambo
Nilifikia shule zote.

Wilaya ya Uyui
Nilifikia shule 8

Wilaya ya Nzega
Nilifikia shule 4.

Wilaya ya Chato shule moja pekee.

Kiufupi nilifikia shule angalau 100 katika kipindi hicho cha miaka miwili. Shule hizo ni za Sekondari pekee (O Level).

Sababu ya kuandika uzi huu ni ifuatayo.

Katika shule zote nilizofikia, nilivutiwa na shule nyingi (uendeshaji wa shule, nidhamu ya wanafunzi, na attitude ya walimu), lakini zaidi ni shule mbili. Na shule hizo ni kama ifuatavyo.

1. Igwisi secondary school
2. Zugimlole secondary school.

Shule zote mbili zipo wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. Shule zote mbili zilianzishwa mwaka 2019, hivyo mwaka 2022 ndiyo ulikuwa mwaka wa kwanza wa wanafunzi kuhitimu katika shule hizo.
Pia shule hizo ziko vijijini (ndani ndani). Igwisi inapatikana pembeni ya barabara ya kutoka Kaliua mjini kwenda Ulyankulu. Na kabla hujaifikia lazima upite kwanza Kazaroho secondary school. Zugimlole inapatikana barabara ya kutoka Kaliua mjini kwenda kilomita 60 bila kusahau Ugalla River National Park.

Kilichonivutia kwenye shule hizo ni mambo yafuatayo.
1. Ushirikiano wa walimu.
2. Nidhamu iliyojengwa kwa wanafunzi. Mfano, pale Igwisi ilikuwa ni marufuku mwanafunzi kuonekana mtaani anazurura kuanzia saa moja usiku, huo ni muda wa kujisomea.
3. Attitude ya walimu katika kuwafundisha wanafunzi. Katika shule hizo, sikuwahi kusikia kauli za "watoto wa vijijini hawafundishiki", bali nilisikia kauli zifuatazo, "tumejipanga kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri kitaaluma".

Sasa baada ya kuvutiwa na hayo yote, nikawa nasubiri matokeo ya kidato cha nne kwa hamu kubwa, na nipende kusema hawajajiangusha, na niimani yangu watazidi kuboresha zaidi na zaidi na hata baadaye wafute division 4, maana katika matokeo yao ya kwanza hakuna division 0, na hata division 4 nyingi ni za 26 - 29, kuanzia 30 - 33 ni za kuhesabu.

Screenshot_20230129-140826_Chrome.jpg

Pia
Screenshot_20230129-141010_Chrome.jpg

Bonus
Katika halmashauri ya Ushetu, shule ya sekondary Ukune, wao walishajiwekea mkakati wa kutopata division 0, na kwa miaka miwili niliyofatilia matokeo yao (2021 na 2022), hapakuwa na division 0. Nao naamini wanajipanga kuongeza kiwango (kufuta division 4).

NB. Simaanishi hizi ndizo shule pekee zinazofanya vizuri huku zikiwa mazingira ya vijijini, zipo nyingi (maana sijatembelea shule zote za Tanzania), bali hizi ndizo ambazo binafsi zilinivutia kwa namna walimu walivyokuwa wanatimiza wajibu wao.

Mfano, katika shule nilizofika na hawana (wana division ziro chache) ni kama ifuatavyo
1. Ulewe secondary school (ushetu, hakuna ziro).
2. Vumilia secondary (urambo, ziro 2).
3. Iyogelo secondary (Bukombe, hawana ziro).
4. Nkome secondary (Geita, ziro 2).
5. Mkindo secondary (Kaliua, ziro 1).
6. Nyankende secondary (Ushetu, hakuna 0)
7. Uyumbu secondary (Urambo, division 0 tatu).

Kwa uchache.

Nawasilisha.
 
Kutangaza shule bora kinara wa matokeo mazuri ya mtihani ni kuzi promote kibiashara shule za kibinafsi, wazazi watahemka kupeleka watoto huko wakiamini kuna ufundishaji uliotukuka kumbe ni matokeo tu hata kwingine wanaweza kupata matokeo mazuri kama wakidhamiria kufanya vizuri
 
Back
Top Bottom