Tumwambie mumewe ukweli au?

Mumewe hana mamlaka ya kutaka maelezo ya kwanini mkewe amesimamishwa kazi, unless otherwise huyo mumewe ndio mwanasheria wake!
 
taratibu za kazi hazihitaji kuleana, kuna mambo ya kuleana,
huyo dada ni haki yake kupigwa chini,
Lakini kiofisi wewe hutakiwi kumjibu huyo mumewe,
Kwanini mnamkataba nae wowote ule, au mna mahusiano yoyote yale kiofisi???

Anatambulika
 
Mjibu hivi huyo Mzee,

Kwako Ndugu Mume,

Tafadhali rejea barua yako yenye kumbukumbu No........ ya tarehe ...... ambapo uliitaka kampuni itoe maelezo na sababu zilizopelekea kusimamishwa kazi kwa mfanyakazi wetu Bi..........., ambaye ulidai pia kwamba ni mke wako.

Hata hivyo, tunapenda kukufahamisha kwamba kampuni haina wajibu wowote kisheria wa kutekeleza ombi lako kama ulivyotaka. Usimamishwaji kazi wa Bibi........ ulizingatia sheria, taratibu na sera za mazingira ya kazi katika kampuni yetu.

Tunashauri kwamba endapo lipo jambo litakaloonekana kutofuata sheria na taratibu basi Bibi............, anaweza kulileta rasmi ofisini na tutalifanyia kazi ipasavyo.

Wako
HR
 

Hata huyo mwanaume aliyezini na mke wa mtu naye pia ni mshenzi!
 

Vipi kuhusu huyo mume wa mtu aliyezini je yeye hajachukuliwa hatua yoyote? je vp mkewe yeye hajaja kuulizia?
 
Anatambulika
Hiyo ni kampuni binafsi???
Je mna taratibu za kushirikisha spouse wakati wa ajira???
Kama ni hivyo basi mjibuni kama si hivyo kwa taratibu za kiutumishi wa umma haina haja ya kumjibu
 
Vipi kuhusu huyo mume wa mtu aliyezini je yeye hajachukuliwa hatua yoyote? je vp mkewe yeye hajaja kuulizia?

Mkewe hakuja kuulizia, alinifuata na kuniambia amemdanganya mkewe na mkewe ameamini
Nikamwambia aombe mke asije kazini
 

Asante ndugu yangu kwa elimu hii.
 
sawa bhana kaka, ishu hiyo ni ya mwajiri na mwajiriwa ss itakuwaje mumewe anataka kujua sbb, tambua kuwa hana haki ya yy kupewa sababu amuulize mkewe ndio mwenye kujua kosa alilofanya kazini kwake.
 
Mkuu ni sawa kabisa mwanamke ameshapewa barua ya kufukuzwa kazi.anapaswa kumweleza mumewe.lakini pia kama ofisi hakuna sehemu yeyote inayozuia mwajiri kumnyima taarifa ya kufukuzwa kazi mwenza wake ama tatizo lolote ingawa pia ni lazima mwajiri atumie busara ili kusitokee madhara kwa familia.hapa naelezea kwa upande wa utumishi wa umma sijajuwa kwa makampuni binafsi inakuaje.any way suala kama hili kwa serikalini lingekuwa na mlolongo mrefu na si kufukuzwa kazi mara moja kama inavyotokea kwa vyombo binafsi.kwa kuwa sina uzoefu wa kufanya kazi kwenye private firms sitaweza kuelezea zaidi.
 

Sijui kama kuna mahali imesemwa kwamba huyu mama amefukuzwa kazi. Amepewa barua ya kusimamishwa kazi kwa maana ya suspension wakati maamuzi zaidi yakisubiriwa. Na kwa hicho ulichokisema, ni ajabu kama sheria za kazi za serikalini zinaruhusu masuala ya kikazi ya mtu kuwasilishwa kwa spouse wake. Nasema hiyo ni ajabu kwangu.

Tiba
 
"Mumewe akaleta barua kuuliza kwanini mkewe kasimamishwa kazi"only in Tanzania,ila ni ka novel kazuri.
 

ok.sorry kumbe amesimamishwa hakufukuzwa.ninachoeleza ni kwamba spouse hakatazwi kujuwa taarifa za matatizo ya mwenzake na si ofisi kuwasilisha taarifa hizo kwa huyo mume kwa case hii hapa.lakini pia nikasema masuala kama haya mwajiri anapaswa kutumia busara kuona je suaa hili nikilieleza familia itaathirika kwa kiasi gani?familia inayotambulika hapa ni baba,mama na mtoto.zinazotumika nyingi ni kanuni tu mkuu.
 

Ndugu yangu, huyo mama hakufa kwamba sasa familia au mume apewe taarifa ni kitu gani kimesababisha kifo chake akiwa kazini. Yuko hai na anao wajibu wa kumueleza mumewe ni kwa nini amesimamishwa kazi, ofisi haina huo wajibu kwa mume. Period

Tiba
 
Very good advice Tiba!
 
Last edited by a moderator:
Kwani ukimweleza ukweli nini kitakudhuru?
Au nawe wataka kuonjeshwa?
 
Mlime mke barua yenye maelezo yote kwa kina kwa sababu yeye ndo una mkataba nae..
Then mwanaume akija kwa sababu hamna mkataba nae, mwambie mmempa barua mkewe yenye maelezo yote.. ni juu ya mkewe kumuonesha au vp..
Hapo utakua
 
Ingekuwa mbongo kawafuma wakizini angeuchuna tu.
Ila huyo mzungu kaona akachomeee......au na yeye alikuwa anammendea huyo mwanamke akamtosa!!!!
 
Kimsingi kampuni haina ulazima wala uhusiano wa moja kwa moja na mume wa huyu dada. Hivyo, barua iwe fupi tu kuwu mke wake amesimamishwa kazi kutokana na masuala ya ofisi. Maelezo zaidi atapata kwa mkewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…