alex method
Member
- May 18, 2015
- 10
- 1
Ndooooo bongo yetu
taratibu za kazi hazihitaji kuleana, kuna mambo ya kuleana,
huyo dada ni haki yake kupigwa chini,
Lakini kiofisi wewe hutakiwi kumjibu huyo mumewe,
Kwanini mnamkataba nae wowote ule, au mna mahusiano yoyote yale kiofisi???
Dhambi ya uzinzi hata kwenye Biblia ndio imeruhusiwa watu kuachana. Huyo mwanamke ni mpumbavu, kama alitaka kufanya uzinzi angeweza kufanya hata Gesti ila sio ofisin kwa mtu. Ipo siku ataweza mleta mwanaume kitandani kwa mmewe.
Mimi nashauri mume aambiwe ukweli, ukweli ukijulikana utasaidia kufumbua tatizo lako, kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga. Mpeni tu ukweli, siku zote ukweli unaleta haki na Na uongo haudumu.
Wakuu kuna staff hapa kwenye shirika letu ni mke Wa mtu ameshikwa live akifanya mapenzi na jamaa mmoja hivi ambae ni mume Wa mtu pia ofisini
Bahati mbaya aliewashika ni bosi wao ambae ni raia wa canada
Walisubiri staff wengine waondoke ndipo wakaanza kufanya ndani ya Chumba cha ofisi, unfortunately huyu m Canada akarudi ofisini alisahau kitu akaona taa zinawaka kwenye Chumba kingine akaamua aangalie kama bado kuna mtu, ndo akawafuma wakifanya zinaa
Kwa sasa tumewasimamisha wakati uchunguzi ukiendelea kama sheria za kazi zinavyotaka na policy ya shirika pia, tayari walishaleta barua za kujieleza
Hivi karibuni mume Wa huyu mama kaja kuniona kupata undani Wa tatizo la mkewe , alitaka kujua ni kwa nini tumemsimamisha mkewe kazi na tumetumia vigezo gani
Bahati mzuri/mbaya malalamiko yake ameweka kwenye maandishi kwa njia ya barua, ni Mzee Wa kikoloni hivi very conservative.
Nikamwambia nitakujibu kwa barua pia utaikuta kwa secretary siku flani
Sasa wakuu mm kama hr business partner Wa hapa kwetu nalazimika kutunza siri za staff, tumelichanganua na wenzangu wakadai hatuwezi kumficha mume jambo zito kama hili, hivyo bado sijaridhika na majibu ya viongozi wenzangu hivyo nije kwenu wana jf kupata opinion zaidi maana humu nna uhakika kuna viongozi maofisini na kuna wasomi wengi tunaweza kuchanganua kwa pamoja suala hili
Mara ya mwisho nilikua na tatizo la kikazi kama mjuavyo idara ya hr ina changamoto nyingi nikaja hapa kuomba ushauri nikapata msaada mkubwa sana
Naomba nisieleweke vibaya, yapo mambo ya kikazi yana vikao vyake hayahitaji kuja hapa ila kuna Yale ya kikazi ambayo yamekaa kijamii kama hili yenyewe nimeamua niwe nawashirikisha kwa mawazo
Swali
Nimjibu mume kwamba mkewe alishikwa akifanya mapenzi ofisini?
Mkewe kaja kazini Jana na kunipigia magoti kwamba nimdanganye mumewe kuwa amesimashwa kaingizia kampuni hasara
Kwamba mm ndo nimeshikiria ndoa yake kwa sasa, kwamba akiachika na umri huo ataenda wapi
Situation ni very tricky na mwisho sijui EXCOM itaamua nini kuhusu hawa watu wawili
Your opinion please
NB
Kama wahusika Wa hili sakata wamo humu ndani I do regret in advance for inconvenience caused in one way or another
Hiyo ni kampuni binafsi???Anatambulika
Kanuni za utumishi (standing order)zinatambua haki za mume,mke na mtoto kwahiyo mwenza yeyote ana haki ya kwenda kushtaki kwa mwajiri kwa issue yeyote inayoathiri familia kwa namna moja ama nyingine.kwa upande wa suala la huyu mzee na mkewe ni haki kabisa kwa mwajiri kumweleza ukweli mwanaume tatizo lililopelekea mkewe kuachishwa kazi.lakini sisi kama binadamu sometime unatakiwa kutumia busara na kuona side impact endapo utaeleza ukweli wa jambo hilo.
Mkuu ni sawa kabisa mwanamke ameshapewa barua ya kufukuzwa kazi.anapaswa kumweleza mumewe.lakini pia kama ofisi hakuna sehemu yeyote inayozuia mwajiri kumnyima taarifa ya kufukuzwa kazi mwenza wake ama tatizo lolote ingawa pia ni lazima mwajiri atumie busara ili kusitokee madhara kwa familia.hapa naelezea kwa upande wa utumishi wa umma sijajuwa kwa makampuni binafsi inakuaje.any way suala kama hili kwa serikalini lingekuwa na mlolongo mrefu na si kufukuzwa kazi mara moja kama inavyotokea kwa vyombo binafsi.kwa kuwa sina uzoefu wa kufanya kazi kwenye private firms sitaweza kuelezea zaidi.Mkuu unless kuna kitu sijakielewa hapa au wengi tunaochangia hatujaelewa. Huyo mama aliposimamishwa kazi kutokana na kitendo alichokifanya alipewa barua ya kiofisi. Kwa hiyo huyo HR alipashwa amwambie mume kwamba mke aliisha pewa barua na hiyo inatosha. Hii ni tofauti kabisa na mtu ambaye anatelekeza familia na mke au mume anakwenda ofisini kulalamika. These are two different cases ambazo wala hazina ulinganisho.
Huyo mume kwa nini asipate maelezo kutoka kwa mke wake? Kwani mke wake ni bubu kwamba hawezi kujieleza?
Tiba
Mkuu ni sawa kabisa mwanamke ameshapewa barua ya kufukuzwa kazi.anapaswa kumweleza mumewe.lakini pia kama ofisi hakuna sehemu yeyote inayozuia mwajiri kumnyima taarifa ya kufukuzwa kazi mwenza wake ama tatizo lolote ingawa pia ni lazima mwajiri atumie busara ili kusitokee madhara kwa familia.hapa naelezea kwa upande wa utumishi wa umma sijajuwa kwa makampuni binafsi inakuaje.any way suala kama hili kwa serikalini lingekuwa na mlolongo mrefu na si kufukuzwa kazi mara moja kama inavyotokea kwa vyombo binafsi.kwa kuwa sina uzoefu wa kufanya kazi kwenye private firms sitaweza kuelezea zaidi.
Sijui kama kuna mahali imesemwa kwamba huyu mama amefukuzwa kazi. Amepewa barua ya kusimamishwa kazi kwa maana ya suspension wakati maamuzi zaidi yakisubiriwa. Na kwa hicho ulichokisema, ni ajabu kama sheria za kazi za serikalini zinaruhusu masuala ya kikazi ya mtu kuwasilishwa kwa spouse wake. Nasema hiyo ni ajabu kwangu.
Tiba
ok.sorry kumbe amesimamishwa hakufukuzwa.ninachoeleza ni kwamba spouse hakatazwi kujuwa taarifa za matatizo ya mwenzake na si ofisi kuwasilisha taarifa hizo kwa huyo mume kwa case hii hapa.lakini pia nikasema masuala kama haya mwajiri anapaswa kutumia busara kuona je suaa hili nikilieleza familia itaathirika kwa kiasi gani?familia inayotambulika hapa ni baba,mama na mtoto.zinazotumika nyingi ni kanuni tu mkuu.
Very good advice Tiba!Kama story hii ni ya kweli basi huyo mama ni mpuuzi na hastahili kuonewa huruma ama kufichiwa siri. Kama alijua alichokuwa anakifanya ni kibaya, kwa nini alikubali kufanya hivyo tena ndani ya ofisi? Si basi wangekwenda hata hotelini au guest house?
Halafu huyo mume wake inakuwaje anakuja kutaka kujua kwa maandishi ni kwa nini mmemsimamisha kazi mke wake? Kwani nyie kama ofisi mna uhusiano gani na huyo Bwana mpaka awatake maelezo kiofisi? Mjibu kwa urahisi huyo mume kwamba sababu zilizofanya mke wake asimamishwe ni za kiofisi na anayezijua ni mke wake, hivyo akamuulize mke wake. Huyo mume kwenu ni third party na hana haki ya kujua ni kwa nini mmemchukulia hiyo hatua mke wake. Amuulize mkewe.
Tiba