Tumwambie mumewe ukweli au?

Tumwambie mumewe ukweli au?

Mkuu Mchakavumlasana, tuko pamoja hapa ila ofisi haina wajibu wa kumwambia chochote huyo, akamuulize mkewe, ni mtu mzima na ana uwezo wa kujieleza mwenyewe kwa nini atake maelezo kutoka ofisini? Niliisha sema nina wasiwasi na uwezo kiutendaji na huyo HR. Huyu HR eti bila aibu anasema alimuahidi kumjibu kwa maandishi, you must be out of your mind mr/mrs HR.

Tiba

mi nahisi mke atakuwa ajamuonyeshe mume hiyo barua
atakuwa ameificha ndo maana mzee akaamua kwenda kuwauliza kwa maandishi
 
Napata shaka kuamini kama kweli wewe ni hr.kwani mkataba wa kazi wa huyo mama,alisign akiwa na mumewe?sasa hapo amekuja kuuliza akiwa kama nani,na nyie mtamjibu kama nani?
 
Mkataba Wa mwajiri unasemaje? Na huyo mume kaandika barua kama nani? Hebu fata procedure zote umuterminate huyo mama na uweke document zote kwenye faili lake ndo litafanya kazi iwapo huyo mama atakwenda CMA na siyo huyo mume cause kampuni haimtambui na hana mkataba Wa kampuni hope muna mwanasheria Wa kampuni iwapo huyo mume ataenda mahakamani Kwa kosa lipi? Ukijiloga kumujibu barua yake Kwa maandishi utakuwa umejifunga mwenyewe cause maandishi ndo ushaidi mzuri Wa mahakama hata kama upo right so mujibu Kwa mudomo kuwa maandishi anayo mwenye mkataba na kampuni ambaye ndo mkewe.
 
Kama story hii ni ya kweli basi huyo mama ni mpuuzi na hastahili kuonewa huruma ama kufichiwa siri. Kama alijua alichokuwa anakifanya ni kibaya, kwa nini alikubali kufanya hivyo tena ndani ya ofisi? Si basi wangekwenda hata hotelini au guest house?

Halafu huyo mume wake inakuwaje anakuja kutaka kujua kwa maandishi ni kwa nini mmemsimamisha kazi mke wake? Kwani nyie kama ofisi mna uhusiano gani na huyo Bwana mpaka awatake maelezo kiofisi? Mjibu kwa urahisi huyo mume kwamba sababu zilizofanya mke wake asimamishwe ni za kiofisi na anayezijua ni mke wake, hivyo akamuulize mke wake. Huyo mume kwenu ni third party na hana haki ya kujua ni kwa nini mmemchukulia hiyo hatua mke wake. Amuulize mkewe.

Tiba

Mkuu wa kichwa ndo maana unaitwa Tiba
 
Stili aibu ya mwenzio na yako pia istiliwe ila kama unaweza tu!
 
Iko hivi, hakuna utaratibu unaoruhusu mume kuandika barua akitaka kujua hatma ya mkewe. Hata mke akifa, urithi huwa ni jukumu LA mahakama kutoa tamko/amri baada ya vikao vya kifamilia.

Mjibu huyo mzee kuwa suala la mkewe ni kiofisi na kwamba yeye mkewe ndio amjulishe mumewe kosa, hata akimdanganya. Msimjibu kwa barua itakula kwenu.

Mwambie pia mkewe kuwa mume asiingilie suala ambalo lipo kwenye comm likisubiri maamuzi.

Hatari ya wewe kuongopa kwa mumewe eti hasara utafukuzwa kazi! Hatua ya wewe kumwqmbia mumewe kosa LA mkewe pia utafukuzwa kazi, huna mamlaka juu ya comm na utakuwa umeingilia ndoa ya watu.

Kukaa kimya pia mtaonekana mna njama dhidi ya mkewe na nakuapia babu atazaa na mtu hapo.

Pangu Pakavu.

Fuata ushauri huu na utakuwa salama.
 
Kumfukuza mtu kazi ni jambo linalofuata taratibu na kanuni na sheria.Hivyo lazima kufuata mambo hayo kwa umakini.Kwa mfano lazima mhusika aandokiwe barua ya kujieleza au suala lichunguzwe ukweli uwekwe wazi halafu ndipo barua ya kumfukuza kazi kulingana na kosa lilivyokubwa inaandikwa.Barua yenyewe ni mfanyakazi husika.

Sio ya familia wala sio ya mwenza.Kwa hiyo mme hana haki ya kujua chochote kuhusu hilo isipokuwa kupitia kwa mkewe.Sio vema kujihusisha na mme kwa suala kama hilo.Kwani waweza kujikuta kwenya matatizo kama kesi kama mme akijua kipitia kwako halafu akasababisha madhala au kifo.

Hata vile kumbuka kwamba sio lazima kila kosa litolewe adhabu.Na adhabu sio lazima iwe kubwa kadri iwezekanavyo.Kama adhabu sahihi ni kufukuzwa kazi na kweli ndivyo ilivyo basi sio lazima ndoa yake nayo ivunjike.Si vema asipate adhabu nyingine kwa sababu yako.
 
Fuata Maadili Yako Ya Kazi!
Achana Na Ndoa Ya Hao Wachepukaji Itaweka Ajira Yako Panaya!
 
atanieleza leo nikifika nyumbani,yaani anafanya umalaya ofisini kwake alafu ananidanganya mimi

Acha mkwara mr mkude loo utadhani kweli ulivyowaka...ila issue imekaa vibaya lkn naona hr ajibu tu kwa busara kuwa mke ndio mwenye jibu lkn ht hivyo mume sidhani km ana.mamlaka ya kuhoji masuala ya kiofisi
 
Ni vema ukajivua jukumu hili na umwachie mke ajibu vizuri kwa mumewe. Mwambie pia mume akamuulize huyo mkewe kama anaipinga vipi hatua iliyochukuliwa.
 
Nakubaliana na wanaoshauri umjibu mzee kwa mdomo kuwa utaratibu wa kazi hauwaruhusu kumjibu his query kwa kifungu cha confidentiality
 
Human resource does not have to disclose anything to anybody if he/she feels employee's right/provacy will be violated. In the matter of fact, you can even hid the information from the boss if he/she has an interest in the matter. So be, DO NOT disclose any information abt this incident to anybody outside these employees line of duty, otherwise you risk a huge civil suit to ur organization. Give the husband a letter asking him to refrain from soliciting your employees private matters.
 
Mkuu sina uhakika na utaalamu wako kwenye mambo ya HR lakini mume wake na huyo Mama hana uhusiano wowote na hiyo kampuni kiasi cha kufikia kutaka maelezo kwa maandishi. Mke ni independent legal entity na mume hana nafasi ya kwenda kuhoji ni kwa nini mke wake alisimamishwa. Kwa nini asimuulize mkewe? Mkewe ni bubu hawezi kuongea? Na wakati anasimamishwa si alipewa barua? Apewe hiyo barua na mkewe asome period.

Tiba

Tiba
Tiba naomba kujua hili nalo limekaaje, Mara nyingi wanawake huenda kushtaki ofisini kwa mumewe iwapo huduma stahiki ya matunzo kwa familia haipo, na Mara nyingi husikilizwa unakuta baba atakatwa mshahara wake, sehemu itaenda kwa mkewe, je kwann wakate mshahara,kwani familia au mke ndo kaajiriwa pale? Kwani na wenyewe si third part? Kwanini asiambiwe hili jambo halituhusu kamalizaneni nyumbani?
 
Last edited by a moderator:
Be extremely careful with this matter, the evidence presented to you about the matter must be anything but hear-say. You must make an informed decision not because the white-guy saw them. Obtain physical evidence about these 2 individuals conduct.

If you have to obtain their email communications pls do, but do not make your decision solely based on what the white-guy said. Anything involving a woman, MUST be handled with extreme care.What about she changed the story that the Two Men wanted to rape her in the office. What about she claim the white guy wanted her for an affair and just said that for revenge.

This is the time the Organization's legal counsel steps in and not Jamii Forum.If you do not have a company's lawyer, pls ask the organization to pay for you to consult one before you proceed. Well, Bongo hakuna sheria anyway I guess you can whatever you want bro..
 
Anyway mkuu unaweza usimweleze ukweli this time lakini nina uhakika taarifa atazipata tu kwa baadae.mweleze mzee kuwa mkewe ametenda kosa kinyume na taratibu na maadili ya kiutumishi.akiuliza kosa gani mwambie huruhusiwi kutoa taarifa za ofisi kwakuwa siyo maadili ya kazi.ila huyo mama ni ndorroooobo.
 
Boss, Sina utaalamu na mambo ya HR, na sijaajiriwa bado. Nimejaribu kuongea kulingana na story ilivyo. Naweza kutokuwa sawa.

According to the HR of moment here, huyo mzee ana wajibu/haki ndio maana walikaa kujadili kama wamwambie ukweli ama lah, na ndio maana huyo mama alienda kumlilia huyo boss wake ili asiseme ukweli, na ndio maana pia walimuahidi huyo mzee kwamba watamjibu, na ndio maana yuko hapa kuomba ushauri wa namna ya kumjibu.

Now, i'm sure 'Mr HR' anajua sheria na utaratibu wa ofisi yake better than anyone here, na kama yeye anadhani huyo mzee anastahili kupewa maelezo, then that's it.

Ndugu yangu kama hayo maelezo yako ndivyo ilivyo, huyo HR anapashwa kibarua chake kioteshwe nyasi. Hakuna cha kujadili hapo, huyo Mzee hana haki ya kuuliza ni kwa nini mke wake amesimamishwa kwani kampuni haina mkataba wowote na huyo mzee. Mwenye mkataba ni mke wake. Hayo maswali yake akamuulize mkewe kwani yeye ni mtu mzima na anao uwezo wa kujieleza.

Kazi zina taratibu zake Bwana. Kwa mfano mume wangu hata kama nimemuandikisha ofisini kama mume, nisipotaka kumwambia nalipwa shilingi ngapi kwa mwezi, hawezi kuja ofisini kudai ofisi imwambie nalipwaje. Hata akija ofisi haipashwi kutoa jibu. Ni sawa na hii issue, huyu HR hakupashwa kutoa nafasi ya ili suala kujadiliwa kiofisi wala kutoa ahadi ya kuijibu barua. Kama alifanya hivyo, basi hiyo nafasi haimfai hata kidogo.

Hapa nazungumzia taratibu za kazi zilivyo, huyo mume ni third party hana haki ya kuhoji chochote kinachohusu ajira ya mke wake iwe kwa mdomo au maandishi. Ningekuwa ni boss wa huyo HR, mpaka sasa angekuwa kazi hana kwa kuukaribisha huu ujinga.

Tiba
 
Tiba naomba kujua hili nalo limekaaje, Mara nyingi wanawake huenda kushtaki ofisini kwa mumewe iwapo huduma stahiki ya matunzo kwa familia haipo, na Mara nyingi husikilizwa unakuta baba atakatwa mshahara wake, sehemu itaenda kwa mkewe, je kwann wakate mshahara,kwani familia au mke ndo kaajiriwa pale? Kwani na wenyewe si third part? Kwanini asiambiwe hili jambo halituhusu kamalizaneni nyumbani?
Kanuni za utumishi (standing order)zinatambua haki za mume,mke na mtoto kwahiyo mwenza yeyote ana haki ya kwenda kushtaki kwa mwajiri kwa issue yeyote inayoathiri familia kwa namna moja ama nyingine.kwa upande wa suala la huyu mzee na mkewe ni haki kabisa kwa mwajiri kumweleza ukweli mwanaume tatizo lililopelekea mkewe kuachishwa kazi.lakini sisi kama binadamu sometime unatakiwa kutumia busara na kuona side impact endapo utaeleza ukweli wa jambo hilo.
 
mkuu mke wa jamaa yeye vipi, hakuja? manake wote si wana ndoa zao
 
Ndugu yangu kama hayo maelezo yako ndivyo ilivyo, huyo HR anapashwa kibarua chake kioteshwe nyasi. Hakuna cha kujadili hapo, huyo Mzee hana haki ya kuuliza ni kwa nini mke wake amesimamishwa kwani kampuni haina mkataba wowote na huyo mzee. Mwenye mkataba ni mke wake. Hayo maswali yake akamuulize mkewe kwani yeye ni mtu mzima na anao uwezo wa kujieleza.

Kazi zina taratibu zake Bwana. Kwa mfano mume wangu hata kama nimemuandikisha ofisini kama mume, nisipotaka kumwambia nalipwa shilingi ngapi kwa mwezi, hawezi kuja ofisini kudai ofisi imwambie nalipwaje. Hata akija ofisi haipashwi kutoa jibu. Ni sawa na hii issue, huyu HR hakupashwa kutoa nafasi ya ili suala kujadiliwa kiofisi wala kutoa ahadi ya kuijibu barua. Kama alifanya hivyo, basi hiyo nafasi haimfai hata kidogo.

Hapa nazungumzia taratibu za kazi zilivyo, huyo mume ni third party hana haki ya kuhoji chochote kinachohusu ajira ya mke wake iwe kwa mdomo au maandishi. Ningekuwa ni boss wa huyo HR, mpaka sasa angekuwa kazi hana kwa kuukaribisha huu ujinga.

Tiba

Mume ana haki ya kujuwa ukweli. Kama mwajiri ataamuwa kumweleza wala haitakuwa na shida kwani kanuni zinamlinda.hapa ni mwajiri kutumia busara kuona kwamba jambo hili akieleza litaweza kuwa na madhara gani kwa familia ya mtumishi aliyesababisha makosa.
 
Back
Top Bottom