Tumwambie mumewe ukweli au?

Tumwambie mumewe ukweli au?

Inawezekana Mkuu maana mie sijui utaratibu wao, lakini kisheria kwenye hili la kusimamishwa kazi hawana obligation yoyote ile kwa mume.

Well, nadhani kila ofisi ina utaratibu wake, na according to the story inaonyesha hiyo ofisi wako obliged kufanya hivyo, ndio maana wamemuahidi watamjibu na wameshajadili namna ya kumjibu pia.
 
Usiwe chanzo cha ndoa yao kuvunjika acha wayamalize wenyewe think if you were the one ungependa mkeo ajue ulioyafanya?
 
caxton

Watu lool!ndoa kaz...vp ukishamwambia mumewe kazin atarudishwa?au ndo kukosa ndoa na kazi pamoja?
 
Last edited by a moderator:
Ikiwa kuna mtu mwenye neno na ndoa hii aseme sasa, la sivyo akae kimya milele! Huwa nayatafakari maneno haya yanayozungumzwa kwenye matangazo ya ndoa na bado sijapata majibu! In short nadhani mnashauriwa mkae kimya milele!
 
hakuna huruma hapo unaweza kumuhurumia akaendelea na huo mchezo akampelekea mumewe ngoma wakazaa kidemu kikali chenye ngoma na mim nikapata ngoma na nikazaa mtoto mwenye ngoma kata hii series mapema bwana HR!!
 
kama wenzio ofsini wamekushauri uweke mambo wazi we Ukaona si busara means una maamuzi mengine... YAFUATE.
 
Msemee tu bwana, mambo ya nini kitafuata muachie mumewe watajuana wenyewe, kama atamsamehe juu yake.
 
Iko hivi, hakuna utaratibu unaoruhusu mume kuandika barua akitaka kujua hatma ya mkewe. Hata mke akifa, urithi huwa ni jukumu LA mahakama kutoa tamko/amri baada ya vikao vya kifamilia.

Mjibu huyo mzee kuwa suala la mkewe ni kiofisi na kwamba yeye mkewe ndio amjulishe mumewe kosa, hata akimdanganya. Msimjibu kwa barua itakula kwenu.

Mwambie pia mkewe kuwa mume asiingilie suala ambalo lipo kwenye comm likisubiri maamuzi.

Hatari ya wewe kuongopa kwa mumewe eti hasara utafukuzwa kazi! Hatua ya wewe kumwqmbia mumewe kosa LA mkewe pia utafukuzwa kazi, huna mamlaka juu ya comm na utakuwa umeingilia ndoa ya watu.

Kukaa kimya pia mtaonekana mna njama dhidi ya mkewe na nakuapia babu atazaa na mtu hapo.

Pangu Pakavu.
 
taratibu za kazi hazihitaji kuleana, kuna mambo ya kuleana,
huyo dada ni haki yake kupigwa chini,
Lakini kiofisi wewe hutakiwi kumjibu huyo mumewe,
Kwanini mnamkataba nae wowote ule, au mna mahusiano yoyote yale kiofisi???
 
Fuata taratibu za kazi zinavyosema,mumewe kaandika barua yakuuliza kulikoni na nyie mjibuni kwa barua kwa hali halisi ilivyotokea..kwa mfano ukadanganya halafu huyu mume wake alivyo mtata akitaka kufuatilia hiyo hasara mkewe aliyoingiza kampuni ipoje ili acheze nayo mahakani,wewe(nyie) mtakuwa katika nafasi gani??fuata taratibu za kazi...zungumzeni ukwel,hiyo ni kazi siyo maneno ya mtaani....
 
Wewe HR wa wapi unayeyumbishwa na wahusika wasiohusiana na mkataba wa kazi wa waajiriwa wako?

Mume kama anaona hajapewa majibu ya kuridhisha na mkewe mwambie atangulie mahakamani awashitaki ninyi kama ofisi...
 
Pole kwa huu mtihani mgumu. Hilo la kumwambia ukweli mume liepuke hasa ukitilia maanani mke kishakupigia magoti umsitiri kwenye ndoa yake. Ila kama mume yumo humu ndio siri ya mkewe kuhusu kusimamishwa kazi imeshavuja.

Mtaua watu kwa pressure! Members wrote humu watakosekana ambao wake zao wamesimamisjhwa kazi kwasababu moja au ingine?!
 
Hilo linawezekana lakini details hazishabihiani. Sikukusudia kumpa pressure yoyote humu ambaye mkewe kasimamishwa kazi bali kuandika ukweli kuhusu huu uzi husika.

Mtaua watu kwa pressure! Members wrote humu watakosekana ambao wake zao wamesimamisjhwa kazi kwasababu moja au ingine?!
 
wewe kama hr unawjibika kwa mfanyakaz wako au kwa spouse wa mfanyakaz wako? be real mumewe hamkuingia nae mkataba wa kaz na ushasema sheria za kaza hazitak kutoa private information kwa mtu ambae hausiki na ofis yako so mwambie mumewe kwamba wewe huwajibik kwake kwa namna yoyote ile kufanya hvyo itakua nikuharbu privacy ya mfanyakaz wako
so kama anataka kujua sababu za kusimamishwa kaz mwambie akangalie kwenye barua ambayo mmempa huyo mfanyakaz ya kusimamishwa kwake!
 
Ndugu yangu nakusgauri kuwa kama mtu kakupigia magoti na kukuomba msamaha halafu bado ukamwambia mumeo utakuwa umemuhukumu na neno la Mungu linasema usimuhukumu mwenzako nawewe hutohukumiwa kupiga magoti niishara ya unyenyekevu na hali ya kujishusha chini na mpaka anakupigia magoti n kweli kabsaa ndoa yake ipo mikononi mwako hvyo wewe ndo mtu wa pekee wa kuangamiza au kuiokoa ndoa yake hakuna mwanadamu asiyetenda dhambi na hakuna dhambi Mdogo na kubwa zote zipo sawa na inasameheka isipokuwa ya kumkashifu roho mtakatifu .Kumbuka yule mwanamke mzizi aliyeshikwa watu wakatala kumpiga mawe hadi kufa Yesu akawaambia anayejijua hana dhambi na awe Wa kwanza kumrudishia huyu mwanamke jiwe wote wakaondo bila kusema neno. Usihukumu na wewe usije ukahukumiwa
 
Naona Watu wengi wamechangia vizuri....kuwa mume hahusiki
ila kwa namna yoyote ile usije kumuambia mumewe hicho kilichojiri; gharama yake ni kubwa sana kuliko kunyamaza.
usije uka angamia kwa kukosa maarifa!!
 
Back
Top Bottom