Tumuunge mkono mwakilishi wa Tanzania

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Jamani nimepokea hii kwenye PM yangu nikiombwa niiweke hapa JF ili kuhamasisha watanzania (watakaopenda) kumuunga mkono Rachel Temu anayeshiriki kwenye MISS AFRICA UNITED STATES.

Admin naomba uiache hapa kwa muda ili watu wengi waione na baadae unaweza kuihamishia kwenye forum yoyote utakayoona inafaa.


Mshindi anapatikana kwa kupiga kura online na Watanzania tufuate hiyo link hapa ili kumpigia kura Rachel Temu:

http://www.missafricaunitedstates.com/mausa/vote.htm

Asanteni.
 
Tumuunge mkono kwasababu ni Mtanzania au tumuunge mkono kwasababu she is the most qualified person? Mshindi atakuwa ni muwakilishi wa Africa, kama kuna mtu anasifa zaidi yake kwanini nisimpigie kura ili Africa ipate muwakilishi bora zaidi?

Sina nia mbaya ila ninaomba ushauri kabla sijapiga kura yangu.
 
U have no idea MWK!! i saw the photo of Rachel kwa Michuzi, she is not the type of a girl that i would vote for!!Very unattractive indeed!! Mwafrika wa Kike i urge u to do the same for the Miss Tz of this year competing against a bunch of the world most skinny girl, thats where i'm gonna pay attention!!Thats where being a Tz counts!! Anayetaka ampigie asiyetaka naye poa just dont play pushy!!
 

Ninavyojua mimi,

washiriki wote ni waafrika. Kwa hiyo katika group la kina dada waafrika kutoka nchi za bara la Afrika hapa USA, unapigia kura mmoja unayetaka ashinde.

Kwa hiyo ukimpigia kura Rachel ina maana unafanya choice ya Tanzania kutoka katika kundi la nchi za Afrika. Na wala sio kuwa ni Africa inashindana na mabara au nchi za mabara mengine.

Nimejibu swali kwa kadri nijuavyo mimi, natumai limeridhisha swali lako.

Asante
 

Hii pia ni sawa.

Huu ndio uzuri wa JF, kila mtu anatoa wazo lake na analisimamia kwa hoja. Nakubalia na wazo lako na ndio maana nimetumia neno kwa atakayependa.

Kwa kuwa wewe unamuona hafai, natumai kuna wengine watamuona anafaa na anaiwakilisha nchi yetu na hivyo watampigia kura.

Asante!
 
kwani huyu si ndiyo yule mdogo wa Hoyce Temu(ex miss tz aliye olewa kinyemela) amabye alishiriki miss arusha kama mara mbili??
 

Brazamen upo?
 
Masatu.. usimwalike brazameni.. maana atageuza topiki.. hii inahusu mwakilishi wa Tanzania.. sasa yule wa kwatu hata haoneshi mlima Kobelo.. lakini huyu jirani yetu anaonesha "Mlima Kilimanjaro".. so.. naona tumpigie debe huyu huyu awakilishe nchi zetu mbili..
 

mhhhhhhhh!!!!!!!
 
that said, kwa vile sidhani kama wanaweza kubadili utaratibu wao... nimeshampigia kula Temu.. if for anything else.. kuna bendera ya Tanzania chini ya picha yake..
 
ha ha hah!! thanks Mwanakijiji, kumbe kijijini wanafatilia sana hizo "overqualifications"!!!
 

Niwie radhi mzee....
 
duh ! haya lakini pia itakuwa vizuri vile vile yule Richard sijui nani ndani ya big braza aungwe mkono ! ni ushauri tu !
 
that said, kwa vile sidhani kama wanaweza kubadili utaratibu wao... nimeshampigia kula Temu.. if for anything else.. kuna bendera ya Tanzania chini ya picha yake..

nadhani ukitumia different computer unaweza kumpigia hata huyo jirani yetu.

Teh teh teh..... mbona kwenye ile bash ya Chicago hukusema kuwa unapenda mlima Kobelo? Au ndio hivyo tena preference zinaenda kulingana na season! kwi kwi kwi

mpigieni dada yetu pia jamani... hayo mambo ya milima kobelo yatatumika wakati wa kutafuta mchumba...... lol
 
duh ! haya lakini pia itakuwa vizuri vile vile yule Richard sijui nani ndani ya big braza aungwe mkono ! ni ushauri tu !

Asante Kada kwa kukumbushia kuhusu Richard.

Mwenye info ya namna ya kumpigia kura Richard anaweza kuweka hapa pia kabla wakuu hawajahamisha hii thread.

Mimi nilipewa za Rachel pekee.

Thanks!
 
dadangu we.. mimi na wabongo wenzangu tu vingine hivyo fahari ya macho tu.. anyway.. nadhani milima isiyooneshwa ndiyo inayowafanya watu kama kina Livingstone kuifungiaga safari.. Mtu unaweza kujikuta unashabikia kichuguu (no pun intended) ukidhania ni milima!! so.. Go TEMU.. go Tanzania..! and Go Taifa Stars!!
 

Asante kwa kumpigia Rachel,
Nitawasiliana naye atangaze milima yote ya Tanzania vyema.

Asanteni wote mnaoendelea kumpigia kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…