Tumuenzi Kikwete Historia isije Ikamsahau

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
View attachment 38509
Baada ya kutafakari sana na kutumia muda mwingi kuwaza jinsi gani kama ningepewa nafasi ya kumuenzi Rais Kikwete ningefanya nini nimejikuta na mapendekezo mengi sana yaliyonijia kwa ghafla kichwani kama maporomoko ya maji kwenye magema ya Udzungwa. Kama ukungu ukiinuka na kuachana na manyasi kwenye kona za Mlima Kilimanjaro alfajiri na mapema ndivyo fikra zangu zilivyofunguka na kutambua kuwa Rais Kikwete hajaenziwa vya kutosha kutoka na mchango wake mkubwa katika maisha, historia, hali, na hatma ya watu wetu. Hivyo mapendekezo yangu nimeyatoa kwa moyo wa furaha uliojaa tabasamu, kicheko na matumaini kuwa yatakubaliwa na wale wote wenye kuitakia mema nchi yetu ambao hawapendi kuendeleza chuki binafsi, udini, ukabila na ubaguzi wa aina yoyote.

Ni mapendekezo ya kiungwana ya kumuenzi Rais wetu wa nne.

Pale Ikulu pabadilishwe na kuitwa Kikwete House
Barabara ya Morogoro iitwe Jakaya Highway
Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam ambapo alisomea kibadilishwe kwa heshima yake na mchango wake katika uchumi na kuitwa Jakaya Kikwete Dar-es-Salaam University (tunaweza kuongeza "national" kwenye hiyo title)
Jengo jipya la sanaa lililojengwa na Wachina liitwe Jakaya Kikwete Center for Performing Arts
Chuo Kipya cha Kijeshi kule Kigamboni kiitwe Lt. Col. J. M. Kikwete War College
Jeshi la Wananchi ambalo alilitumikia kwa umakini na umahiri limpandishe cheo ili we Gen. Jakaya Kikwete ili kuonesha mchango wake wa jinsi alivyoliendeleza jeshi hilo hadi kukamata maharamia nane.
Kwa vile nimekuwa nikipigia sana kampeni ya kujengwa kwa hospitali ya taifa ya watoto naamini kama atalifanyia kazi wazo hili hospitali hiyo iitwe Dr. Jakaya Kikwete National Children's Hospital kwa masharti kwamba kama itatokea ikajengwa wakati hayupo basi tunaweza kuongeza neno "Memorial" humo katikati.
Kutokana na kuendelesha mahusiano yake ya karibu na viongozi mbalimbali wa dini napendekeza viongozi wa Kiislamu waangalie ni Msikiti gani maarufu nchini upewe hadhi ya Kikwete Mosque; Viongozi wa Makanisa wanaweza nao - kutokana na mambo mbalimbali ambayo amewasaidia - kutafuta mahali ambapo pangeweza kupewa jina la Jakaya Kikwete National Chapel. Kama ni kubwa sana tunaweza kuliita Cathedral! Kama ni Wakatoliki na jengo hilo lina hadhi ya Kipapa tunaweza kuita "Kikwete Basilica of Our Lady of Fatima"
Daraja linalotarajiwa kujengwa la Kigamboni kwa ushirikiano mkubwa wa serikali na NSSF laweza kupewa jina la Kikwete International Bridge (sasa hii 'international' ni kwa sababu tu watu watakuwa wanavuka kwenda ng'ambo kupitia daraja hilo).
Nimekumbuka kuwa ile Maktaba ya Taifa kwa kweli haina hadhi ya kitaifa kwani haina jina la kiongozi wa kitaifa. Hivyo naipendekeza - sidhani kama kuna watu watanipinga - iitwe Dr. Kikwete National Library. Hii ni kutokana na mchango wake wa kuendeleza usomaji nchini na huduma ya library na hasa kutokana na mipango ya miaka kumi iliyopita ya ujenzi wa maktaba mpya jijini Dar kukidhi mahitaji ya watoto wetu ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwa utawala wa Rais Kikwete

Ukiondoa maeneo hayo nadhani wapo watu wengine wanaoweza kufikiria maeneo, vitu na hata majengo mbalimbali ambayo yatalibeba jina la Rais Kikwete. Na licha ya hivyo wakati umefika wa kuanza kuweka picha zake sehemu mbalimbali nchini. Picha kubwa zinaweza kuanza kupambwa kuanzia uwanja wa ndege na maeneo yote ya kuingilia mijini. Kwa vile ofisi zote tayari zinapambwa na picha ya rais ndani nafikiri hii si heshima nzuri kwa maana si watu wote wanaingia maofisini humo. Napendekeza picha kubwa za rangi (zinaweza kuwa zile za kutabasamu au akimpa mtoto peremende) ziwekwe maeneo ya wazi ya nje ili ionekane.

Sasa tukiwa tunafanya hivyo napendekeza kuwa kumtaja kwa jina la Dr. Kikwete kwa kweli hakuendani hasa na hisia za Watanzania wengi. Binafsi kuanzia leo hii nitamtambulisha kama Kiongozi Mpendwa Dr. Sasa hili ni muhimu sana kusema hivi kwa sababu isije ikaonekana anachukiwa. Kwa kiingereza tunaweza kumuiwa "Dear Leader" au "Beloved Leader" ili kuonesha mapenzi yetu kwa uongozi wake mahiri na jinsi gani amegusa mioyo ya watu wetu na kuwafanya wainuke kujiletea maendeleo.

Kama unakubaliana na mapendekezo yangu nawe unaweza kupendekeza ni maeneo au vitu gani muhimu vibebe jina la Rais Mpendwa Kikwete? Sasa ni lazima viwe ni vitu vya heshima visiwe vitu vya kejeli ili tusionekane kabisa tunamdharau. Sasa kwa vile haya ni maamuzi ya wananchi wenyewe hayahitaji kibali kwani kama jina la mahali likishazoeleka sana ndivyo linavyokuwa na baadaye kutambulika hivyo.
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Hivi wewe jamaa utaacha lini kuandika pumba? Unashindwa hata na Kubenea kwa kujenga hoja ingawa mpaka sasa hajui aliyemmwagia tindikali. Jitahidi kupunguza porojo mkuu!
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,590
116,755

Hastahili kuenziwa bora tumuenzi yule mama mmiliki wa kondoo mwenye baka leupe la ajabu ubavuni.
 
Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,878
3,725
Hivi wewe jamaa utaacha lini kuandika pumba? Unashindwa hata na Kubenea kwa kujenga hoja ingawa mpaka sasa hajui aliyemmwagia tindikali. Jitahidi kupunguza porojo mkuu!

Umepoteza muda wako mwingi wa maisha yako kusomea uandishi lakini taaluma imekutupa umebakia kuwa mercenary!! Ningekuita MALAYA kwani utamtumikia yeyote atakayelipa dau lako.!!
 
Xyln

Content Manager
Nov 27, 2007
2,739
168
Kama ni Wakatoliki na jengo hilo lina hadhi ya Kipapa tunaweza kuita "Kikwete Basilica of Our Lady of Fatima"

Fascinating !
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
:flypig:
MMM you mean this to be............"The Palliative Substance That We All Need When Inflicted In One Way Or Another!"

Nina wasiwasi huo!!!!!!!!!!!

Ningependekeza pia shirika letu la ndege likifufuka na likawa na ndege, ndege zote zinazokwenda nje ya nchi ziandikwe kwa maandishi makubwa ambayo hata ikiwa angani sisi ardhini tutayasoma na yasomeke "Jakaya Kikwete Airlines" ili kuenzi na kuutambua umaarufu wake wa kupaa angani na kusafiri nje ya nchi
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
:flypig:
MMM you mean this to be............"The Palliative Substance That We All Need When Inflicted In One Way Or Another!"

Nina wasiwasi huo!!!!!!!!!!!

Ningependekeza pia shirika letu la ndege likifufuka na likawa na ndege, ndege zote zinazokwenda nje ya nchi ziandikwe kwa maandishi makubwa ambayo hata ikiwa angani sisi ardhini tutayasoma na yasomeke "Jakaya Kikwete Airlines" ili kuenzi na kuutambua umaarufu wake wa kupaa angani na kusafiri nje ya nchi

Nina uhakika mkubwa kwamba hii inaweza ikafufuka within a month... nimeipenda!
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
na kwa kuheshimu mchango wake hasa kwenye michezo tuwaite taifsa stars = kikwete wanderers

Unajua hii nadhani imechelewa kwa kweli. Jinsi alivyotuletea kocha toka Brazil na kufanya vizuri sana kwa timu hiyo baada ya kuifunga Togo kwa uhakika ni muhimu kutambua mchango wake. Sijui kwanini hakuna viongozi wa michezo waliofikiria hili. Natumaini hili baraza jipya la michezo lililundwa na Nchimbi majuzi litafanya kazi yake.

Timu ya Olympic iitwaje?
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Hivi wewe jamaa utaacha lini kuandika pumba? Unashindwa hata na Kubenea kwa kujenga hoja ingawa mpaka sasa hajui aliyemmwagia tindikali. Jitahidi kupunguza porojo mkuu!

Nyinyi ndio maadui wa taifa letu; Kikwete amekukosea nini hutaki kumuenzi mchango wake mkubwa kwa Taifa? Unafikiri Tanzania inaweza kupata tena kiongozi kama Kikwete? Nina uhakika hata wazo la kumuongezea muda zaidi ni wazo zuri.
 
tito majala

Member
Sep 4, 2011
25
3
Mie sijaona alichofanya jk toka aingie madarakani mpaka apewe yote hayo na historia itamuhukumu siyo kwa kupigiwa debe
 
Mwita25

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
3,836
1,164
Nyinyi ndio maadui wa taifa letu; Kikwete amekukosea nini hutaki kumuenzi mchango wake mkubwa kwa Taifa? Unafikiri Tanzania inaweza kupata tena kiongozi kama Kikwete? Nina uhakika hata wazo la kumuongezea muda zaidi ni wazo zuri.

Sarcastically spoken!
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,443
Unajua hii nadhani imechelewa kwa kweli. Jinsi alivyotuletea kocha toka Brazil na kufanya vizuri sana kwa timu hiyo baada ya kuifunga Togo kwa uhakika ni muhimu kutambua mchango wake. Sijui kwanini hakuna viongozi wa michezo waliofikiria hili. Natumaini hili baraza jipya la michezo lililundwa na Nchimbi majuzi litafanya kazi yake.

Timu ya Olympic iitwaje?
nadhani tatizo lipo kwa watanzania zaidi, tuko very slloooooww kutafakari;

hebu imagine na pale jangwani tupaite kikwete "falling square" ni memorable kabisa tunaweka na mnara kabisa kama wa bismin... imagine tukiita tanesco pia kikwete electric supply company ltd (Kikwesco) --- itaendana na zile kumbukumbuku za queen ruweij

we are really slow sometimes....

Kuhusu timu ya olympic, hii kutokana na uchanga wake wa miaka hamsini tu tungu tupate uhuru, na pia kwakuwa tumejitahidi, tumeweza na tutafanya zaidi, basi tuiite Ridhwani Kiwete olympic team representing the Kikwete united republic of accidents and emergency
 
Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,432
18,126
Hivi wewe jamaa utaacha lini kuandika pumba? Unashindwa hata na Kubenea kwa kujenga hoja ingawa mpaka sasa hajui aliyemmwagia tindikali. Jitahidi kupunguza porojo mkuu!
we ndo uliyemwagia kubenea tindikali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

9 Reactions
Reply
Top Bottom