Tumuamini Nani, Chadema Au Zitto Kabwe?

Ni kuishiwa na kufilisika kwa hoja kurudia mada iliyo humu JF. Kaka Fred Mpendazoe,wewe nawe sasa umekuwa kituko. Ni kama Mchange ambaye kila uchao huwa ni wa kulambalamba watu kwa uchu wa ngawira na madaraka

Iko wazi,kaka Mpendazoe umefulia vya kutosha. CHADEMA huwa inajidhalilisha kupokea na kuwaamini watu kama wewe na Mchange. Kazi yenu ni uanasiasa tumbo tu!

Tuombe tu Mungu hawa Ccm,Chadema na Act waache uanasiasa tumbo maana hata hatujui tukiamin chama gani.
 
Nimeona ninukuu sehemu ya hoja ya mtanzania mmoja aliyeeleza yafuatayo. Hoja hiyo ni mhimu kwa watanzania wazalendo

"......Kwa msingi wa hoja zao kuwa Zitto ni kigeugeu na kwamba haaminiki Leo anaweza akapinga jambo na kesho akageuka, nadhani CHADEMA ndio wanaongoza kwa kuwa na sifa hiyo.

Kama hiyo ndio Hoja, basi Kwa sasa, Chadema ndio chama ambacho hakipaswi na hakiwezi kuaminiwa Mara 1000 zaidi kulinganisha na Zitto alivyo.

Nitatoa mifano Michache.

Mwaka 2013/2014, Freeman Mbowe akiwa kiongozi wa upinzani na mbunge wa Hai, aliwaongoza wabunge wenzake kupinga bajeti ya wizara ya Ujenzi iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Magufuli, mbowe aliipinga bajeti hiyo na kupiga kura ya hapana pale Bungeni, na kusema hawezi kuunga mkono serikali ya CCM.

Mungu si Athumani, mwaka huo huo Dkt Magufuli akaenda jimboni kwa Mbowe Hai, kisha au kabla alikwenda jimboni Rombo kwa Joseph Selasini, huwezi amini aisee,

Sifa alizozipolomosha Mbowe kwa Magufuli na Kikwete (aliyekuwa Rais) hazifikii hata Robo ya zile alizozitoa Zitto Kigoma, ndio maana ilimbidi mpaka Magufuli achukue link ya YouTube na kwenda nayo Bungeni katika bajeti iliyofata na kuwaambia wabunge na watanzani jinsi serikali ya CCM inavyochapa kazi kiasi cha kusifiwa hadharani na Freeman Mbowe. - NANI Tumuamini sasa, Chadema au Zitto?.

Naongeza, Kabla ya tarehe 15-09-2007, msamiati wa neno FISADI haukuwa maarufu hapa nchini Tanzania.

Unamjua aliyeuibua sawa sawa?.

Ni Chadema kupitia Tundu Lissu,

Ndio, Tundu Lissu akiwa Mwanachadema na mwanasheria machachali, tarehe 15-00-2007 pale viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es salaam, akishirikiana na Mbowe, na viongozi wengine wa upinzani akiwemo Dkt. Slaa, Maalim Seif , Mbatia na Wengine. Lissu alisoma Orodha ya Watanzania kumi na moja wanaolifilisi Taifa hili la Tanzania, tena akasema watu hawa hawanastaha ya kuitwa jina lingine zaidi ya MAFISADI, Lissu akasoma Orodha ya Mafisadi akisindikizwa na vifungu kibao vya Sheria.

Katika Timu ya watu 11 waliotajwa na Lissu kama mafisadi wanaoliumiza Taifa mtu NAMBA 9 aliyetajwa na Lissu na Chadema ni *EDWARD LOWASSA* Kwamba kwa mujibu wa Lissu na Chadema LOWASSA ni miongoni mwa Wafilisi 11 wa nchi hii, Leo LOWASSA yuko wapi, na Lissu yuko wapi na anasemaje?. - Tuwaamini Chadema?.

Naongeza, Mwaka 2011/2012 kule Arumeru palikuwa na Uchaguzi wa Marudio, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema, alisimama Jukwaani na Kuwashukuru wananchi kuwa walimzomea Mzee LOWASSA. Nitayarejea baadhi ya maneno yake

*"Jana mmemzomea LOWASSA, ni Heshima kubwa kwa Mungu Kumzomea Mwizi, LOWASSA ni FISADI*" Huyo ni God bless lema wa Chadema, Leo LOWASSA yuko wapi na Lema yuko wapi?, anasema nini?..- TUWAAMINI CHADEMA?.

Niongeze?... Msigwa alimtukana LOWASSA, akasema atakayemnadi na kumshabikia LOWASSA akapimwe akili yake, nani alimnadi LOWASSA 2015, ni Zitto au Msigwa?. - Tuwaamini Chadema?

Mwaka 2010 katika kampeni za Uchaguzi mkuu Moja kati ya Sera za Chadema ilikuwa ni Kurudisha viwanda vyote vilivyobinafsishwa na kugeuzwa maghala, Chadema wakasema watavirudidha kwa wananchi, Mbowe akasema lazima virudi, Leo mwaka 2017 Mbowe yule yule anasema serikali imekosea kutoa tamko la kuvirudisha viwanda vile vile walivuotaka kuvirudisha wao mwaka 2010. Tuwaamini Chadema?...

Mwaka 2010 mpaka 2013 mwanzoni, CUF waliitwa CCM B na CHADEMA, Nccr wakaitwa Washirika wa CCM, miezi michache mbele CCM B na washirika wa CCM wakaungana wakaitwa UKAWA. tuimini Chadema?

Mifano iko mingi mingi mingi sana.

USHAURI

nawashauri viongozi na wanachama wa Chadema waachane na Zitto, wajenge Chadema yao, wamuache Zitto na ugeu geu wake na chama chake, watu makini wanafahamu kwamba Chadema ni kikundi cha watu wasaka madaraka tu na sio chama cha siasa.

Chama makini chochote cha siasa hakivunji wala kukiuka misingi yake iliyojiwekea,

Chama makini cha siasa hakiwezi badili Gia angani, lakini kikundi cha wasaka madaraka kinaweza Fanya lolote lile ilimradi tu kipate madaraka.

Wamuache Magufuli afanye kazi ya kuleta maendeleo aliyoahidi, maendeleo hayana chama, maendeleo hayana dini maendeleo hayana Kabila.

Kama Zitto alimpinga Magufuli Jana, sio kigezo cha kpongeza Leo kama amefanya vizuri na wala sio kizingizi cha kutokumkosoa kesho akifanya vibaya, hiyo ndio huitwa siasa ya masuala.

Ndio maana LOWASSA hamsimangi Lissu aliyemwita Fisadi namba Tisa hapa nchini,

Ndio maana LOWASSA hamsimangi Lema aliyekesha akimtukana katika mikutano ya kisiasa

Ndio maana LOWASSA hamsimangi msigwa, hamsimangi Mbowe aliyemkejeli kuwa ni dhaifu na baadae kumpokea wala hamsimangi yeyote, anafanya siasa zenye kukipigania anachokiamini atakipata anataraji kukipata.

Vijana, viongozi na wanachama wa Chadema kuhangaika na kina Zitto, Kitila mkumbo na Anna Mgwira ni kujidharirisha kwa kuonyesha kiwango kidogo cha uelewa wa masuala ya siasa.

Nawapongeza sana baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema wanaojikita kila uchao kuhangaika kutafuta suluhu ya changamoto za wananchi wao kama MEYA Boniface Jacob, John Mnyika, David Silinde Mwita Waitara nakadharika.

Muhimu kujua ni kwamba Zama zimebadilika, siasa zimebadilika, siasa za Leo si sawa na siasa za miaka mitano iliyopita.

Siasa za Leo zinahitaji wanasiasa wanaoleta majawabu kwa wananchi wao kuliko kutukanana kila uchao. Mmesha tukanana imetosha sasa wapeni majawabu wananchi.

Ndimi,
Habibu Mchange
0762178678
Mwananchi wa kawaida."

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe Mpendazoe na Mchange wote mnaongozwa na njaa na sasa mnaonekana mnasumbuliwa na utapia mlo
 
Feledi, cha kufanya sasa hivi ni kupiga kimya weeee halafu mtafute hata katibu wa lumumba wa tawi fulani hivi halafu mnong'oneze, bwana ee mie bwana huku kwingine naona miyeyusho tu naomba nifanyie mitkasi mie nirudi nyumbani. yale nlofanya ule mwaka 2014 yalikuwa makosa na nnatubu na sirudii tena na ndugu zangu wanielewe hivyo. halafu mtoe huyo katibu tawi kiaina, hata buku 7 hivi maana wale wanakulaga. halafu tulia kimyaaa subiri majaliwa. nani ajuaye, zali linaweza kukuanguankia come 2025 maana majimbo yote saa hizi yamejaa ingawa kuna tetesi majimbo mapya yakaanzishwa karibu na bupandagila
 
Nani kukudanganya wewe?unataka kutwambia hata Jk Nyerere naye unamuingiza kwenye hawa wapuuzi?

In God we trust

Achana na Mwalimu Nyerere huyo mzee huwezi mweka kundi moja na wanasiasa wa mwendokasi.

Hawa wanasiasa wenu wa kizazi kipya hawatofautiani.

Ukitaka kuona jamaa alichoongea ni kuntu.badala ya KUJADILI mada,wote mmejikita kumjadil mtoa mada. Na hizi mbinu hutumika sana ktk siasa pale upande flani unaposhindwa kukabiliana na hoja iliyopo. Wengi hujikita kwenye personality attacks.Hii katika fallacy tunaita ARGUMENT AGAINST THE PERSON.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
hakuna hoja ya kujadili hapo,yote yalishajibiwa,hivi huyo kiazi unamuona mzima huyo!!!!
 
Msaka tonge bado yupo kazini, ongeza speed ila wilaya zote zina ma-dc tyr. utasubiri sana sana! labda awamu ijayo!
 
Huyu alishaambiwa ni ng'ombe asie na mkia hatuna muda wa kupoteza kwa mada zilezile zizowahijibiwa hapa tena kwa kina.
 
Ni kuishiwa na kufilisika kwa hoja kurudia mada iliyo humu JF. Kaka Fred Mpendazoe,wewe nawe sasa umekuwa kituko. Ni kama Mchange ambaye kila uchao huwa ni wa kulambalamba watu kwa uchu wa ngawira na madaraka

Iko wazi,kaka Mpendazoe umefulia vya kutosha. CHADEMA huwa inajidhalilisha kupokea na kuwaamini watu kama wewe na Mchange. Kazi yenu ni uanasiasa tumbo tu!
Oh eti sina chama.
 
We have a long journey to go!

Kama uelewa wenyewe wa mambo ndiyo huu, ccm itaendelea kututawala muda mwingi sana.

Ni sifa mbaya sana na wanaokamatwa hovyo hovyo na serikali za kidikteta uchwara na kikaburu km vile Lissu na Mandela siyo majemedari.

Sifa nzuri ni kuwa rafiki na raisi dikteta uchwara na mwenyekiti wa chama tawala kilichokataza vyama vingine kufanya shughuli zao za kisiasa.

Seems una tatizo la low iq na mnufaikaji wa juma pumba mashudu
 
Back
Top Bottom