Tumsaidie Rafiki...!!!!

Tumsaidie Rafiki...!!!!

I was only tryin to cogitate...this's a one side story

hebu mkuu watu8 toka nje ya pandora box and think deeply what will be your reaction kama itatokea kwako
 
Last edited by a moderator:
du! babu naona unatoa karipio la nguvu.....
ila hata mimi nadhani ningemshauri hivyo kama hana sababu nzito ya kumfanya asizae kwa sasa.
Unajua kuna mabinti wengi tu huwa nawasikia wakisema wanataka kwanza kufaidi maisha baada ya ndoa wakae angalau miaka 2 bila kuzaa. hii inapendeza tena sana tu ila kwa makubaliano ya wote wawili. nani anataka shuruba za kukesha usiku na mtoto siku chache baada ya kuanza kuishi na mpenzi wake? lakini inapofikia kuwa mwenzio anahangaika kutafuta mtoto lakini wewe kontena hutaki kuhifadhi huyo mtoto kwa nini asitafute kontena jingine ambalo lipo tayari?

Daahh hata mimi naskia hivyo mkuu
 
najiuliza unawezaje kuolewa na mtu ambaye huwezi kupanga naye maisha yenu?
swala la kupata watoto ni lenu wote wawili, mnaamua kwa pamoja, kila mtu anajua majukumu yake kama mzazi. kama mama anaona muda huo hawezi kutimiza majukumu yake ya uzazi kwa nini ashindwe kuongea na mwenzie? kama sababu zake ni genuine anaogopa nini kumshirikisha mwenzie?
nakumbuka tofauti ya mtoto wangu wa kwanza na wa 2 ni miaka 8, hatukuwa na tatizo lolote kiafya lakini mimi nilikuwa nina mambo mengine ya kufanya, na tukaongea kwa pamoja tukakubaliana tusitishe kuongeza watoto mpaka tutakapokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. wote wawili tulijua nini kinaendelea kwa hiyo hakuna aliyekuwa anasumbuka kuhusu upatikanaji wa watoto, na maisha yalikuwa mazuri tu.
huyo dada kweli kamkosea mumewe. hata kama mume ni mbabe basi angeongea naye kwanza ili mume akatae. hiyo ingemfanya mume asihangaike mahospitali kutafuta mtoto.
Huyo rafiki yako kama bado anampenda mkewe na yupo tayari kumsamehe basi akae kwa utulivu kuongea naye. amsikilize sababu za yeye kutokata kuzaa kwa sasa, kama zina uzito basi amsikilize...... watoto watakuja tu hapo baadae.

Ni kweli unenayo mkuu, na hili linachangia ku raise suspicion kwamba kama hili la mtoto kanificha hivi je kuna mengine gani ambayo pia anayafanya kimya kimya? Sometimes I tend to agree kwamba women are complicated creatures.
 
Mtu unajidedicate kutafuta mafanikio huku na kule ili familia iwe katika misingi imara kumbe mwenzako hana wito wa kuzaa.
 
du! babu naona unatoa karipio la nguvu.....
ila hata mimi nadhani ningemshauri hivyo kama hana sababu nzito ya kumfanya asizae kwa sasa.
Unajua kuna mabinti wengi tu huwa nawasikia wakisema wanataka kwanza kufaidi maisha baada ya ndoa wakae angalau miaka 2 bila kuzaa. hii inapendeza tena sana tu ila kwa makubaliano ya wote wawili. nani anataka shuruba za kukesha usiku na mtoto siku chache baada ya kuanza kuishi na mpenzi wake? lakini inapofikia kuwa mwenzio anahangaika kutafuta mtoto lakini wewe kontena hutaki kuhifadhi huyo mtoto kwa nini asitafute kontena jingine ambalo lipo tayari?

Mi ndo maana bibi yenu huyu kitu kiliweka kambi tumboni ndo nikatangaza ndoa.
 
A friend of a friend is a friend.....
Salam wakuu wa mmu. Jana mida ya usiku nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu akiwa amepaniki na mwenye hasira nyingi. Tatizo aliliokua nao kwa kweli nilishindwa kumpa ushauri instantly (najijua na siasa zangu za mrengo wa kushoto) hivyo naomba nishee hapa jukwaani tuone tunamsaidia vipi ndugu yetu. Kwa kifupi jamaa ameoa na anapendana sana na mke wake na ndoa yao ina mwaka mmoja na miezi kadhaa. Wote wana successful careers ila tatizo lao kubwa ni kukosa mtoto. Hii imekua changamoto kubwa sana katika maisha yao na wamejaribu kwa kila jinsi kupata mtoto imeshindikana hali ambayo iliwalazimu kwenda hospitali ambapo wote walionekana hawana matatizo.
Kwa kweli swala la kukosa mtoto lilimsononesha sana rafiki yangu japo mke wake (kwa madai yake mwenyewe) alionekana kulichukulia kawaida na siku zote alikua akitoa jibu la "Mungu bado hajapanga tupate watoto). Sasa juzi jamaa wakati anatafuta charger yake ya simu chumbani baada ya kui misplace katika pekua pekua madroo akapigwa na butwaa baada ya kukuta 'contraceptive pills' kwenye droo mkewe akiwa amezificha. Anasema alishtuka sana ila alikausha adi mkewe aliporudi home ndo akaanza kumbana. Kumbana sana mwishowe mkewe akakiri kwa muda mrefu amekua akitumia contraceptive pills kuzuia aishike mimba kwa madai bado ni mapema sana naye ana mipango yake anataka kuaccomplish kwanza hivyo akizaa itaharibu mipango yake. Ndgu yangu amejisikia vibaya sana kwa jibu la mkewe huyo na amehitaji ushauri wa nini cha kufanya. Mimi kama nilivyosema siasa zangu za mrengo wa kushoto nimeshindwa kumpa ushauri kwani ungekua severe sana hivyo naomba basi wana mmu tuweze kutoa ushauri ambao tunahisoi utakua best solution kwa wanandoa hawa wawili. Asanteni sana.
Regards,
Don Lucchese.

Ndiyo tatizo la kuoa mwanamke under 30 years, hawa wa miaka sijui 20 mpaka 29 ni wasumbufu sana katika ndoa maana wanaamini eti bado muda unawaruhusu.Nakuambia ukioa mwanamke kuanzia miaka 30 huyo anakuwa ameshapigwa vibuti vya kutosha sana kwa hiyo akimpata mwanaume lazima anyenyekee maana ishakua jioni ati.Kwa hiyo hakutakuwa na sijui mipango wala nini maana hapo ana miaka 10 mpaka 15 ya kuzaa kwa hiyo lazima hatataka kusikia habari za kusema eti nataka kuacomplishi unaacomplish nini kilichokushinda huko nyuma,so kwa kifupi ndiyo hivo jamaa yako ameoa hawa watoto wa under 30.
Kuna mwandishi alishawahi kuandika kuwa the age of reasoning kwa mwanamke inaanzia miaka 30 kwa hiyo kwa nyie waoaji jitahidi kutafuta kufuatana na miaka hiyo wala hamtajutia kumjua mwanamke
 
mh!babu Mkali wewe!!! Utaua mtu!

Si ukali mjukuu wangu, vitu vingine vinakera. Unakuta jamaa anachochea kama stovu huku akisali sala zote apate mtoto aitwe baba kumbe janamke linamchora tu.

Hivi unafikiri kustorongo ni kazi rahisi eh?
 
duh... mpe pole huyo mshikaji....
 
hebu mkuu watu8 toka nje ya pandora box and think deeply what will be your reaction kama itatokea kwako

Hahaha...
Kitendo alichofanya huyo mwanamama pasi na shaka ni cha ubinafsi...
Ningelifanya nini? inategemea na malengo yetu ya awali yalivyokuwa...
 
Last edited by a moderator:
Labda mumewe ana IQ ndogo sana mke anaogopa kuzaa form four failure anasubiri mumewe awe na akili ndio wazae....
 
Ni kweli unenayo mkuu, na hili linachangia ku raise suspicion kwamba kama hili la mtoto kanificha hivi je kuna mengine gani ambayo pia anayafanya kimya kimya? Sometimes I tend to agree kwamba women are complicated creatures.
Dont go there.....
we are all complicated, even men
 
Mi ndo maana bibi yenu huyu kitu kiliweka kambi tumboni ndo nikatangaza ndoa.
lol!
ila huyo dada ni kilaza sana. kama unataka kuficha yaani katika njia zote za mpango kaamua kutumia vidonge? ambavyo mtu akipekua kidogo tu kaviona. kwa nini asichome tu sindano inabaki kuwa wanajua yeye na daktari tu? vidonge? halafu anaficha chumbani? kama siyo kilaza basi alitaka tu mumewe avione kwa muda wake
 
"Mipango ya Mungu" kumbe huku kizani unatumia vidonge vya uzazi, kweli dunia hadaa..
 
Unajua nimekuuliza lile swali ili nipime sababu ya huyo mwanamke...

Upande wa pili wa shilingi si ajabu rafiki yako ni mbabe na anataka kila aamualo liwe hilo /ndio maana shemejiyo akatumia hiyo njia...

Pia tungelijua katika mipango ya baada ya kuoana ni lini walitarajia kuanza kupata watoto, tungekuwa na namna nzuri zaidi ya kutoa shauri zetu.

Kweli kuna uwezekano huyo mume ni mtu wa command ivo mke kashndwa kukaa chini kupanga mipango nae akaamua afanye maamuz yake..
This make sense
 
Kama alivyosema watu8..inawezekana jamaa ni mtu wa command sn hawez kukaa na mke wake na kuelewana,lakini mwanamke nae alikua hajawaza aisee,what if mwanaume angeamua kupga mech nje na kuibuka na mtoto wa nje,mdada angeshndwa kumlaumu mkaka maana nae kachangia.
Wakae tu waongee though huyo mwanaume atashndwa kumuamini mdada tena..
 
Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?

Tuna mawazo sawa
 
AAh kakosea bhana huyo jamaa..analalamika nini sasa!! Kama asingetaka kunywewa mavidonge hayo angemmimba kabla ya kumuoa tuone kama angetmia mavidonge yake...
 
Dah! hapo hakuna kitu..huyo ni wa kupiga chini fasta tu!
Hata akisubiri yawezekana binti hana mpango wa kuzaa naye..bado hata akipata ujauzito anaweza kutoa makusudi,..si Mungu hajapenda!!!!!
 
Back
Top Bottom