Tumsaidie Rafiki...!!!!

Tumsaidie Rafiki...!!!!

A friend of a friend is a friend.....
Salam wakuu wa mmu. Jana mida ya usiku nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu akiwa amepaniki na mwenye hasira nyingi. Tatizo aliliokua nao kwa kweli nilishindwa kumpa ushauri instantly (najijua na siasa zangu za mrengo wa kushoto) hivyo naomba nishee hapa jukwaani tuone tunamsaidia vipi ndugu yetu. Kwa kifupi jamaa ameoa na anapendana sana na mke wake na ndoa yao ina mwaka mmoja na miezi kadhaa. Wote wana successful careers ila tatizo lao kubwa ni kukosa mtoto. Hii imekua changamoto kubwa sana katika maisha yao na wamejaribu kwa kila jinsi kupata mtoto imeshindikana hali ambayo iliwalazimu kwenda hospitali ambapo wote walionekana hawana matatizo.
Kwa kweli swala la kukosa mtoto lilimsononesha sana rafiki yangu japo mke wake (kwa madai yake mwenyewe) alionekana kulichukulia kawaida na siku zote alikua akitoa jibu la "Mungu bado hajapanga tupate watoto). Sasa juzi jamaa wakati anatafuta charger yake ya simu chumbani baada ya kui misplace katika pekua pekua madroo akapigwa na butwaa baada ya kukuta 'contraceptive pills' kwenye droo mkewe akiwa amezificha. Anasema alishtuka sana ila alikausha adi mkewe aliporudi home ndo akaanza kumbana. Kumbana sana mwishowe mkewe akakiri kwa muda mrefu amekua akitumia contraceptive pills kuzuia aishike mimba kwa madai bado ni mapema sana naye ana mipango yake anataka kuaccomplish kwanza hivyo akizaa itaharibu mipango yake. Ndgu yangu amejisikia vibaya sana kwa jibu la mkewe huyo na amehitaji ushauri wa nini cha kufanya. Mimi kama nilivyosema siasa zangu za mrengo wa kushoto nimeshindwa kumpa ushauri kwani ungekua severe sana hivyo naomba basi wana mmu tuweze kutoa ushauri ambao tunahisoi utakua best solution kwa wanandoa hawa wawili. Asanteni sana.
Regards,
Don Lucchese.
That woman is drab!!!!she is not a wife material, alafu bila aibu ana mpakazia Mungu eti "Mungu ajapanga" duh, vry bad huyo, mwanamke wa siri namna iyo anaeshindwa hata kumshirikisha mume katika maswala ya uzazi hafai, mke wa namna iyo anaweza hata akaja kukuua akiamua,,sasa nini maana yake kupotezeana wakat kwenda ma hospitali kupima,aaaaaaaaaaghhhhhhhhhhhh shit!!!Ebu amwambie kama hataki yeye anaenda kuzaa nje.
 
Baadhi ya wanaNDOA ni Pasua kichwa kwakweli Ndomana cc wengine tunasema ukiwa na MKE labda na mtt 1 Hesabu na MKEO ni mtt wa pili manake kuna cku anaweza kufanya Jambo Mwanaume ukabaki unajiuliza huyu ni m2 mzima mwenzangu? Kwa issue ya huyo Dada huenda ameolewa 7bu2 awe na MUME Lkn kuna m2 wake anaempenda ameahidi kuzaa nae labda yuko Nje ya NCHI anamsubiri arudi amdakishe MIMBA! kwamm akili Inagoma kuelewa 7bu zakijinga kabisa hzo Mwambie jamaa yako yy ni m2 mzima aamue mwenyewe cz Mapenzi hayana MSHAURI!
 
najiuliza unawezaje kuolewa na mtu ambaye huwezi kupanga naye maisha yenu?
swala la kupata watoto ni lenu wote wawili, mnaamua kwa pamoja, kila mtu anajua majukumu yake kama mzazi. kama mama anaona muda huo hawezi kutimiza majukumu yake ya uzazi kwa nini ashindwe kuongea na mwenzie? kama sababu zake ni genuine anaogopa nini kumshirikisha mwenzie?
nakumbuka tofauti ya mtoto wangu wa kwanza na wa 2 ni miaka 8, hatukuwa na tatizo lolote kiafya lakini mimi nilikuwa nina mambo mengine ya kufanya, na tukaongea kwa pamoja tukakubaliana tusitishe kuongeza watoto mpaka tutakapokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. wote wawili tulijua nini kinaendelea kwa hiyo hakuna aliyekuwa anasumbuka kuhusu upatikanaji wa watoto, na maisha yalikuwa mazuri tu.
huyo dada kweli kamkosea mumewe. hata kama mume ni mbabe basi angeongea naye kwanza ili mume akatae. hiyo ingemfanya mume asihangaike mahospitali kutafuta mtoto.
Huyo rafiki yako kama bado anampenda mkewe na yupo tayari kumsamehe basi akae kwa utulivu kuongea naye. amsikilize sababu za yeye kutokata kuzaa kwa sasa, kama zina uzito basi amsikilize...... watoto watakuja tu hapo baadae.

FP umeongea ukweli mtupu shida ni kwamba wengi hawajui madhara ya hizi dawa za uzazi wa mpango wengine vimewafanya tasa asije kumbuka shuka asubuhi akawa anakodolea macho watoto wa wengine yeye ikawa ndoto.
 
Back
Top Bottom