Tumsaidie Rafiki...!!!!

Tumsaidie Rafiki...!!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,258
Reaction score
22,140
A friend of a friend is a friend.....
Salam wakuu wa mmu. Jana mida ya usiku nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu akiwa amepaniki na mwenye hasira nyingi. Tatizo aliliokua nao kwa kweli nilishindwa kumpa ushauri instantly (najijua na siasa zangu za mrengo wa kushoto) hivyo naomba nishee hapa jukwaani tuone tunamsaidia vipi ndugu yetu. Kwa kifupi jamaa ameoa na anapendana sana na mke wake na ndoa yao ina mwaka mmoja na miezi kadhaa. Wote wana successful careers ila tatizo lao kubwa ni kukosa mtoto. Hii imekua changamoto kubwa sana katika maisha yao na wamejaribu kwa kila jinsi kupata mtoto imeshindikana hali ambayo iliwalazimu kwenda hospitali ambapo wote walionekana hawana matatizo.
Kwa kweli swala la kukosa mtoto lilimsononesha sana rafiki yangu japo mke wake (kwa madai yake mwenyewe) alionekana kulichukulia kawaida na siku zote alikua akitoa jibu la "Mungu bado hajapanga tupate watoto). Sasa juzi jamaa wakati anatafuta charger yake ya simu chumbani baada ya kui misplace katika pekua pekua madroo akapigwa na butwaa baada ya kukuta 'contraceptive pills' kwenye droo mkewe akiwa amezificha. Anasema alishtuka sana ila alikausha adi mkewe aliporudi home ndo akaanza kumbana. Kumbana sana mwishowe mkewe akakiri kwa muda mrefu amekua akitumia contraceptive pills kuzuia aishike mimba kwa madai bado ni mapema sana naye ana mipango yake anataka kuaccomplish kwanza hivyo akizaa itaharibu mipango yake. Ndgu yangu amejisikia vibaya sana kwa jibu la mkewe huyo na amehitaji ushauri wa nini cha kufanya. Mimi kama nilivyosema siasa zangu za mrengo wa kushoto nimeshindwa kumpa ushauri kwani ungekua severe sana hivyo naomba basi wana mmu tuweze kutoa ushauri ambao tunahisoi utakua best solution kwa wanandoa hawa wawili. Asanteni sana.
Regards,
Don Lucchese.
 
Hiyo mipango ya shemeji yako ni mipango gani??
 
Inawezakana mke ana nia njema sana ila kwa kutomshirikisha mumewe imekua mbaya sasa, We fikiria mmehangaika hadi mahosipitali mmekwenda na mke huyo huyo, kumbe nyuma anakucheka tu na kuweka unafiki eti Mungu hajapanga.

Ni kosa tayari mkewe amefanya kwa kutomshirikisha na kukubaliana juu ya hilo, Ikiwezekana achukue kalikizo ata ka siku mbili tatu na mkewe watoke wakakae sehemu kwa muda, wagombezane vya kutosha, mwishowe wataelewana cha kufanya. Na Mungu awasaidie.
 
Mpe pole sana huyo rafiki yako! Kimsingi jambo alilomfanyia huyo jamaa yako ni la kusikitisha siyo siri tena akimpumbaza kwamba MUNGU bado hajaamua wao kuwa na watoto, jambo la kuwa na watoto naamini ndiyo moja ya ajenda kuu ya wanandoa kuungana na kuanzisha familia, kama huyo mwanamke hakuwa tiyari au labda aliona ni mapema sana kuzaa angemshirikisha mume wake lakini siyo kutumia njia mbadala ambazo siyo halali kuzuia jambo hilo ambapo tiyari ameshamuathiri mume wake kisaikolojia!! Kwa kifupi huyo mwanamke hayuko tiyari kuzaa na huyo rafiki yako kwa hiyo haina haja ya kuendelea kuishi na mwanamke wa aina hiyo!!
 
Si wakubaliane tu!
Ikishindikana walingalinishe hoja!!
Ikitokea hoja zipo sawa, ya Mume inaprivail!!!!!
 
Hiyo mipango ya shemeji yako ni mipango gani??

Kiukweli hata mimi sifahamu ila sijui dunia hii ni mipango gani ambayo eti kwa kuzaa itaharibika. I find it more like an excuse
 
Mpe pole sana huyo rafiki yako! Kimsingi jambo alilomfanyia huyo jamaa yako ni la kusikitisha siyo siri tena akimpumbaza kwamba MUNGU bado hajaamua wao kuwa na watoto, jambo la kuwa na watoto naamini ndiyo moja ya ajenda kuu ya wanandoa kuungana na kuanzisha familia, kama huyo mwanamke hakuwa tiyari au labda aliona ni mapema sana kuzaa angemshirikisha mume wake lakini siyo kutumia njia mbadala ambazo siyo halali kuzuia jambo hilo ambapo tiyari ameshamuathiri mume wake kisaikolojia!! Kwa kifupi huyo mwanamke hayuko tiyari kuzaa na huyo rafiki yako kwa hiyo haina haja ya kuendelea kuishi na mwanamke wa aina hiyo!!

Ki ukweli hata mimi nimewaza hivyo mkuu, ila leo unamshauri mtu labda amuache huyo mwanamke then baadae wana reconcile halafu mtu unaonekana mbaya kiukweli sijui inakuaje yaan.
 
Inawezakana mke ana nia njema sana ila kwa kutomshirikisha mumewe imekua mbaya sasa, We fikiria mmehangaika hadi mahosipitali mmekwenda na mke huyo huyo, kumbe nyuma anakucheka tu na kuweka unafiki eti Mungu hajapanga.

Ni kosa tayari mkewe amefanya kwa kutomshirikisha na kukubaliana juu ya hilo, Ikiwezekana achukue kalikizo ata ka siku mbili tatu na mkewe watoke wakakae sehemu kwa muda, wagombezane vya kutosha, mwishowe wataelewana cha kufanya. Na Mungu awasaidie.

Kweli mkuu, ndomana sometimes naona sijui kuoa mwanamke literate ni majanga??
 
Yaani anatumia contraceptive na huku anakuambia Mungu hajapanga Mungu gani huyo sasa atakayepanga wakati wewe ushamzuia kufanya kazi yake
mwanaume anajipinda anajua hapa mambo mswano kumbe mwanamke kashazuia kila kitu
Kutomshirikisha Mume katika hiyo mipango yake ni kosa maaana alipaswa amshirikishe mume kwamba sina mpango wa kupata mtoto kwa sasa kutokana na A, B, C zangu na nitakuwa tayari kupata mtoto muda fulani na mume nae atoe wazo lake sio kukaa kimya na kujipangia mipango yako na then mipango ya nyie kuwa familia unaiweka kando
Alipaswa atambue kuwa yumo ndani ya ndoa na yale mambo ya kusema nina mipango yangu au sijui nimejipangia hili na hili una muda wake na ushirikishwaji wa mume au mke katika mipango ya familia ni wa muhimu sana
Kama alivyosema mdau hapo juu hili litakuwa limemuumiza sana jamaa na kwa kweli litaondoa nafasi ya uaminifu baina ya wawili hao ni muhimu kwa sasa wakakaa waongee na wajue ni nini mustakabali wa ndoa yao
 
Kiukweli hata mimi sifahamu ila sijui dunia hii ni mipango gani ambayo eti kwa kuzaa itaharibika. I find it more like an excuse

Unajua nimekuuliza lile swali ili nipime sababu ya huyo mwanamke...

Upande wa pili wa shilingi si ajabu rafiki yako ni mbabe na anataka kila aamualo liwe hilo ndio maana shemejiyo akatumia hiyo njia...

Pia tungelijua katika mipango ya baada ya kuoana ni lini walitarajia kuanza kupata watoto, tungekuwa na namna nzuri zaidi ya kutoa shauri zetu.
 
Kweli mkuu, ndomana sometimes naona sijui kuoa mwanamke literate ni majanga??

Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?
 
Mkuu watu8 hata kama jamaa ni mbabe anataka kile anachoamua kifanyike kitendo cha mama kutumia contraceptive tena kwa kificho bila kumwambia mume na huku mume anahangaika anajua wana matatizo na hospital wameenda na anamuona mume anavyohangaika na kumuacha haileti maana yoyote mkuu
Whether hiyo mipango ina manufaa kwa familia au haina au whether itawasaidia wnafamilia wote ila ilipaswa washirikishane na wasifichane kitendo cha mwanamke kukaa na mipango yake kimya bila mume kujua na huku mume anatarajia mama siku yoyote atapata mimba ni kitendo kibaya na wala hakileti maana kwa kweli
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wanawake wako waired differently na namna ya kukaa nao (awe amesoma au hajasoma) ni kutumia akili sana vinginevyo ukiwakariri umeumia.

''1 Petro 3 : 7 - Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu''

Kweli mkuu, ndomana sometimes naona sijui kuoa mwanamke literate ni majanga??
 
Kama hali ndivyo ilivyo(tumesikia upande mmoja tu) huyo dada hafai ....ni mipango gani hiyo hadi hataki kuzaa!
 
Jambo alofanya huyo mwanamke si la busara kabisa maana sasa nimekumbuka ule uzi ulokuwa ukijadiliwa kuhusu mwanamke kukubali vile anavyotaka mwanaume and at the same anafanya yale ayatakayo yeye yaani kwa kifupi anajihalalishia maovu yake.Angelikuwa hayupo tayari kuzaa angemshirikisha tu mumewe walijadili hilo then wafikie maamuzi muafaka.Bila shaka imani ya rafiki yako kwa mkewe imetoweka na itachukua muda sana mpaka hali irejee kuwa kama awali.Inabidi huyo mdada ajishushe tu na plans zife,hivyo vidonge vya uzazi wa mpango avisahau na waanze na mipango ya kuzaa kwasababu hapo ameshaharibu,na hana excuses kwa kweli na hata kama anazo hazina uzito kwa jinsi alivyolikoroga!!!
 
Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?

mh!babu Mkali wewe!!! Utaua mtu!
 
najiuliza unawezaje kuolewa na mtu ambaye huwezi kupanga naye maisha yenu?
swala la kupata watoto ni lenu wote wawili, mnaamua kwa pamoja, kila mtu anajua majukumu yake kama mzazi. kama mama anaona muda huo hawezi kutimiza majukumu yake ya uzazi kwa nini ashindwe kuongea na mwenzie? kama sababu zake ni genuine anaogopa nini kumshirikisha mwenzie?
nakumbuka tofauti ya mtoto wangu wa kwanza na wa 2 ni miaka 8, hatukuwa na tatizo lolote kiafya lakini mimi nilikuwa nina mambo mengine ya kufanya, na tukaongea kwa pamoja tukakubaliana tusitishe kuongeza watoto mpaka tutakapokuwa na nafasi ya kufanya hivyo. wote wawili tulijua nini kinaendelea kwa hiyo hakuna aliyekuwa anasumbuka kuhusu upatikanaji wa watoto, na maisha yalikuwa mazuri tu.
huyo dada kweli kamkosea mumewe. hata kama mume ni mbabe basi angeongea naye kwanza ili mume akatae. hiyo ingemfanya mume asihangaike mahospitali kutafuta mtoto.
Huyo rafiki yako kama bado anampenda mkewe na yupo tayari kumsamehe basi akae kwa utulivu kuongea naye. amsikilize sababu za yeye kutokata kuzaa kwa sasa, kama zina uzito basi amsikilize...... watoto watakuja tu hapo baadae.
 
si sawa kabisa ajatenda haki huyo mama yani anamwangalia mumewe anavyoangaika hospital yawezekana na maombi huku kumbe yeye ndo kizibo cha hiyo mimba jamani huyu mama ni 'muuaji' kuhukumu si sawa lakini amna hoja ya msingi hapo. hiyo mipango ambayo mimba itaharibu labda ufuska ila ka ya kiuchumi nadhani mimba siyo sababu
mwanamke kakosea,

amsamehe amwone ka mtoto kakosoe na hapo amchape kitu sasa cha ukweli kupunguza jazba,
 
Mwanamke kama huyo ni kumtafutia nyumba ndogo unazaa nayo. By the time anakuja kuwa tayari kupata mtoto we unawahi kufanya vasectomy. Anageuka mama mlezi wa wanao. Pambaf zake, hayuko tayari kuzaa kiherehere cha kuolewa alikitoa wapi?
du! babu naona unatoa karipio la nguvu.....
ila hata mimi nadhani ningemshauri hivyo kama hana sababu nzito ya kumfanya asizae kwa sasa.
Unajua kuna mabinti wengi tu huwa nawasikia wakisema wanataka kwanza kufaidi maisha baada ya ndoa wakae angalau miaka 2 bila kuzaa. hii inapendeza tena sana tu ila kwa makubaliano ya wote wawili. nani anataka shuruba za kukesha usiku na mtoto siku chache baada ya kuanza kuishi na mpenzi wake? lakini inapofikia kuwa mwenzio anahangaika kutafuta mtoto lakini wewe kontena hutaki kuhifadhi huyo mtoto kwa nini asitafute kontena jingine ambalo lipo tayari?
 
I was only tryin to cogitate...this's a one side story

Back
Top Bottom