Tumsaidie huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumsaidie huyu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by makerubi, Jul 1, 2011.

 1. m

  makerubi Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa alioa mke kwa ndoa kanisani yapata miaka mitano iliyopita huko kijijini na kuhamia Dar kikazi, wakabahatika mtoto mmoja. mwanamke alianza kubadirika baada ya kufika mjini ugomvi ndani hauishi maelewano hamna kila mwanaume akijaribu kumrekebisha mkewe lakini ikashindikana tena kufikia hatua mwanamke kugombana hata na shemeji zake, wifi pindi wanaposuluhisha.

  Wakati mwingine mkewe huyo huchangia na mdogo wake wakike ambaye walikuwa wakiishi wote kumpiga pindi panapokosekana maelewano. Basi mwanaume akaona suluhisho ni kujali mtoto pindi atokapo kibaruani akijua amekula tu suluhisho ni kukimbilia Bar kupoteza machungu.

  Siku anatoka kazini, jamaa akakuta mwanamke kabeba kila kitu ndani na mtoto katimka hajui pakumtafutia akagundua baada ya siku tatu yakuwa aliuza vitu akaenda kuishi mkoa mwingine na jamaa mwingine ambaye mpaka hii leo wanaishi wote na kesha mfungulia miradi mbalimbali na gari kamnunulia na wameisha zaa watoto mapacha, lakini mtoto wa jamaa naye wanamlea.

  Jamaa akaamua kuondoa upweke akamtolea mahali msichana mwingine na wameshazaa mtoto mmoja lakini alimficha huyo msichana yakuwa hakufunga ndoa ya kanisani ila alizaa tu na kuishi naye yule mke wake, msichana anataka ndoa kwani mahali keshatolewa na wanaishi wote na mtoto pia wamezaa.

  Je afanyaje? anaruhusiwa kufunga kanisani? au mpaka Serikalini? anasema mwaka watano toka akimbiwe nayule mke wake,na yule mkewe ndo anaishi na mumewe huyo aliyemkimbilia. NIMELETA KWENU WANAJAMII TUMSAIDIE MSAADA WA KISHERIA AFANYAJE?? Kwani mke aliyenaye anahitaji ndoa.
   
 2. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  • Kwanza inabidi ahalalishe kuachana na mke wake wa kwanza yaani apate certificate of divorce hiyo inafanywa na mahakama.
  • Baada ya hapo kisheria atakuwa huru kuoa tena.
  Lakini kwa kuwa yeye ni mkristo na kiapo kilikuwa cha mke mmoja nadhani taratibu za dini yake haziruhusu. Hivyo itabidi afunge ya kiserikali, au namna yeyote atakayoona inafaa.
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  amwambie ukweli huyo binti then akiridhia ndoa waoane bomani baada ya kupata divorce mahakamani
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Moja ya ground za divorce ni uzinzi
  mke alikuwa na ndoa akaacha ndoa yake ikiwa bado haijavunjika akaenda kuolewa na mwamnaume mwngine. Hilo linamhalalishia jamaa kwenda mahakamani kuomba divorce kwa kuwa tayari mke wake kashaolewa na mwanaume mwingine na wamezaa watoto. afanye juhudi tuu za kuwasilisha maombi mahakamani ili ndoa hiyo ivunjwe na aruhusiwe kuoa mwanamke mwingine maana ile ndoa ya kwanza ni kama mwanamke kashakubali ivunjike na huwezi kuwasuluhisha tena

  Aende mahakamani hata kama ndo ani ya kikirsto aombe mahakama itengue ndoa yake ya kwanza ili aruhusiwe kuoa
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hata kanisani ndoa hiyo inavunjwa. Kumbuka Yesu alisema 'kwa sababu ya uzinzi' ndoa inavunjwa. Sasa kuna uzinzi zaidi ya huo? Ndugu yangu, nenda kwa Padre mmpe mkasa wote na tafuta ushahidi wa kuolewa na mtu mwingine. Hata kujua wapi ameolewa inatosha kwani kanisa lina parokia, vigango na jumuia kila mahali; hizo za mahali alipoolewa ndizo zitatoa taarifa kwa padre wako, then ndoa inavunjwa; unakuwa huru kufunga nyingine ya kikristo. Inaweza kuchukua muda kiasi, lakini utafanikiwa.
   
 6. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  kutokana na taratibu za dini ya kikristo huyo bwana anazo haki zote za kuoa tena, biblia inasema hairuhusiwi kumuacha mkeo ILA kwa UZINZI, kutokana na story kamili nadhani huyo bwana alihusisha kanisa lake kama kweli alikuwa akihudhuria. kama la. itakuwa ni vigumu. wandugu hapa inaonyesha umuhimu wa mtu kuwa mshirika anayetambulika katika kanisa fulani. pindi apatapo shida kama hii atakuwa akiwashirikisha viongozi wake wa kanisa na suluhisho ni rahisi kupatikana. KOSA umechukua binti wa watu ukaishi nae na kuzaa nae bila ya taratibu zozote za kikanisa, wewe huna tofauti na alilofanya mkeo ( tofauti ni kwamba yeye kaanza wewe ukamalizia, kamwaga mboga wewe ukamwaga ugali) sasa kama ulikuwa ukishiriki ibada mahali fulani nenda kawaone viongozi wako watakueleza yakupasayo kufanya. USISAHAU kachukue mtoto wako kama huwezi kuishi nae kampe mama yako mzazi.
   
Loading...