Tumpe zawadi iliyo bora Freeman Mbowe

Hakuwekwa ndani kwa kudai katiba, kudai katiba ni haki ya wananchi ila kwa kufuata sheria na mda mwafaka. Sababu aliyosema Mama ndiyo husika, acha mahakana ifanye kazi yake.
Hoja hii ni kwaajili ya wenye akili. Wanaoweza kuona mambo hata yaliyo nyuma ya pazia.
 
Kwanza hongereni sana wale majasiri wote wa CHADEMA wanaofanya kazi takatifu ya kuwapa elimu wananchi juu ya haki yao ya kuwa na katiba bora itakayolenga kulinda haki zao.

Mheshimiwa Mbowe, yupo ndani kwa sababu ya kuongoza mapambano ya kupata katiba mpya. Waliomkamata Mbowe na kumfungia huko, matarajio yao ni kuwa wakimweka ndani huyu kiongozi shujaa, asiyeyumba na asiyerubuniwa, yale mapambano ya kutafuta katiba mpya yatakoma. UlYakikoma, watakiwa wamefanikiwa. Inatakiwa tuhakikishe hawafanikiwi, na kila dalili inaonekana, jitihada za kupata katiba mpya, zitashinda.

Kinachotakiwa sasa, ni wananchi tuidai katiba mpya kwa nguvu zaidi na kwa umoja zaidi. Hiyo ndiyo zawadi kubwa tunayoweza kumpa Mh. Mbowe. Mbowe atakapotoka huko walikomfungia, akikuta moto aliouwasha umekuwa mkali zaidi kuliko hata alivyouacha, atafarijika sana, na itakuwa ni zawadi kubwa kwake kuliko kitu chochote.

Tusilie wala tusihuzunike kwa Mbowe kubambikiwa kesi, bali tufanye kazi. Kubambikia watu kesi kulianza tangu enzi za Yusuf kule utmwani Misri. Bwana wetu Yesu Kristo, alibambikiwa kesi ya uchochezi na wayahudi.

Shetani hajawahi kuacha kufanya kazi. Shetani kama alivyofanya kazi enzi za Yusuf na enzi za Bwana wetu Yesu Masiha, ndivyo anavyofanya kazi sasa. Mh. Mbowe, hastahili kusikitika bali kufurahia kuona kuwa amepita kwenye njia ambayo watu wema waliowahi kubadilisha mataifa na Dunia, walipita.

Timu zile za CHADEMA digital zinafanya kazi iliyotukuka hasa, na kwa kweli, kwenye hili, naiona CHADEMA ikiwa mbele ya vyama vyote vya siasa. CHADEMA digital ipite kila mtaa, kila mji na kila kijiji ili kuwadhihirishia wale mawakala wa shetani kuwa ubaya hauwezi kuushinda wema.
Asante sana mleta uzi. Mko wangapi wa-Tanzania wa aina yako. Mungu awabariki sana. Haki ni asili ya mema yote, haina Chama wala Kabila wala Dini
 
Back
Top Bottom