Tumia WhatsApp na Apps nyingine katika Kiswahili

Tukudzi

Member
Jun 22, 2019
40
17
Hapa ningependa kuonyesha jinsi ya kubadilisha lugha ya simu yako ili uweze kutumia apps nyingi kupitia lugha yetu ya Kiswahili.

Nimerekodi video ya njia ya kufuatwa ili lugha ibadilishwe, iwapo ungependa kutazama jinsi inavyofanywa.

Kwa anayependa kufuata maelezo badala ya kutazama video:
  1. Nenda Settings
  2. Bonyeza System
  3. Bonyeza Language & input
  4. Bonyeza Language & region
  5. Add language
  6. Chagua Kiswahili
    • Iwapo huioni Kiswahili kwenye orodha ya lugha, songa chini utaona mahali imeandikwa Update Language List. Bonyeza hapo, kisha utapata Kiswahili. Bonyeza Update.
  7. Utakapoulizwa Are you sure you want to change your language to Kiswahili, bonyeza OK/Change.
  8. Ngoja kidogo ili lugha ibadilishwe kwenye simu nzima.
  9. Tumia simu bila shida.

Kwa kutumia picha, maelezo ndiyo haya:

1591231440633.png

1591231487205.png

1591231525099.png

1591231557373.png

1591231591203.png

1591231629057.png

1591231672918.png

Matokeo ni haya:

1591231338938.png

1591231723233.png

Apps zako sasa zinapatikana katika Kiswahili.

Mwenye maswali ako huru kuuliza.
 
Attachments

  • badiliLugha.mp4
    7.3 MB
Mkuu ya kwangu mimi ni bora ibaki katika lugha ya kiingereza maana kiswahili hapo ni kigumu hapo kwenye simu.
 
Mkuu ya kwangu mimi ni bora ibaki katika lugha ya kiingereza maana kiswahili hapo ni kigumu hapo kwenye simu.
Wajerumani hutumia simu zao katika Kijerumani.
Wachina hutumia zao katika Kichina.
Warusi vilevile.
Sisi je? Hili ni jambo nisilolielewa.

Mwanzoni, nilipoanza kutumia Kiswahili kwenye simu na tarakilishi, nilipata changamoto nyingi. Lakini baada ya muda, nikazoea. Nakusihi ujaribu, hata kidogo, kufanya hivyo pia.

Muongozo mzuri ila ungeongeza kisehemu cha faida zake na hasara zake
Faida: lugha ni yetu; tunapoitumia, tuna uwezo wa kuiimarisha pia. Hasara: sio apps zote zinazopatikana katika Kiswahili. Ukalimani unahitajika kuifanya app itumie lugha yetu.
 
Yaani umenikumbusha hii option niliwahi kujaribu kuweka kiswahili kwenye windows phone , bora kiingereza tu maana inachosha na sometimes inachekesha

From JF App
 
Ivi ni Kwa nini kiswahili cha kwenye Simu ni cha ajabu ivi
Wakenya wanazingua kuweka tafsiri za hovyo kwenye google na makampuni ya kichina yanategemea sana google translate badala ya kuajiri mswahili kama mashirika makubwa ya ndege yanavyofanya. Napendaga sana ile mpendwa mteja... afu upo kwenye lidege likubwaaa afu wahudumu wote watasha
 
Sivyo. Umenoa.

Tafsiri si za ovyo. Katika utafsiri/ukalimani wa programu za simu au tarakilishi, makampuni hutumia misamiati ya kiteknolojia. Misamiati hii hutokana na kamusi ya taminolojia mbalimbali, mojawapo ikiwa ile ya Microsoft ambayo iliundwa na wataalamu kutoka Zanzibar, Tanzania, Kenya, Uganda... yaani kutoka jumuiya yetu nzima. Wengine pia walitoka Kongo.

Kama unahisi kuwa lugha kwenye programu si sahihi, uko huru kujitolea kurekebisha tafsiri hiyo. Hujazuiliwa. Kumbuka pia kuwa binadamu hufanya makosa, hata kwenye ukalimani. Kwa hivyo, kama lugha inayotumiwa ni ngumu sana, pengine ni makosa; na unaweza kutoa marekebisho. Kwa mfano, unajua kuwa unaweza rekebisha Google Translate?

Ivi ni Kwa nini kiswahili cha kwenye Simu ni cha ajabu ivi
Kwa sababu lugha ya kiteknolojia sio sawa na lugha ya mazungumzo ya kila siku. Kwa mfano, tuchukue neno Two-Factor-Authentication. Hii sio msemo unaotumika kwenye mazungumzo ya kila siku. Basi? Tafsiri yake itakuweje rahisi. Lenyewe hata kwa Kiingereza sio neno la kila siku. Basi tafsiri yake ikafanywa kuwa kitu kinachoeleweka na wataalamu wa teknolojia - Uhalalishaji wa Hatua Mbili. Kama hutumii teknolojia hiyo kila siku, hutaipata kwenye matumizi yako ya simu.

Asante kwa maelezo mazuri.
Karibu sana.

Yaani umenikumbusha hii option niliwahi kujaribu kuweka kiswahili kwenye windows phone , bora kiingereza tu maana inachosha na sometimes inachekesha

From JF App
Wakati huo wa Windows Phone utafsiri wa Kiswahili haukuwa umeendelea kama leo. Jaribu tena uone mabadiliko.
 
Askwambie mtu, hamna lugha ngumu kama kiswahili hasa katika hizi operating system kama windows, mac na android.. baada ya kuona viswahili sivielewi elewi kwenye options nikarudisha kiingereza fastaa!
 
Askwambie mtu, hamna lugha ngumu kama kiswahili hasa katika hizi operating system kama windows, mac na android.. baada ya kuona viswahili sivielewi elewi kwenye options nikarudisha kiingereza fastaa!
Hiyo basi iwe maoni yako. Anayetaka kuweka Kiswahili iwe lugha ya kifaa chake, basi na aweke. Usimkataze kwa kuwa hukufaulu.
 
Back
Top Bottom