Undugu wa damu ungekuwa unakatizwa nadhani ningekuwa wa kwanza kuomba huduma hiyo. Wadau huyu dogo nahisi ni adhabu tuliyoachiwa na marehemu wazazi (sijui tulikosa nini).. Naomba mjaribu kunisaidia mawazo aisee.
Huyu dogo alipomaliza form 4 (kwa mbinde) hakufanya vizuri sana akajiunga na jeshi la polisi, hakumaliza akatimuliwa huko ccp. Kuna mzee mmoja rafiki wa marehemu mzee akatufanyia mpango dogo akaingia jwtz, dogo akaenda akakimbia depo aftr several weeks. Akaja home, akatafutiwa kazi tanesco akafanya kazi siku mbili. Tukashauriana kwamba aende veta nako akafukuzwa vile vile kwa vurugu. Hakuna ambacho hatujajaribu kwa huyu kiumbe na kuna bro kawahi kumuweka asimamie mradi mmoja hivi kaharibu.. Akiachwa hivi hivi anakuwa ni kero tupu, hapo hom kashauza kila chenye maana. Akija kwa kaka zake ndio ugomvi kila siku cheni, simu na vipochi vya shemeji zake haviponi. Kesi za kutapeli kila siku. Tumewaza hadi tunakaribia kukufuru waungwana.