Namsaidiaje mdogo wangu huyu angalau awe msafi?

Troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
19,882
38,512
Hello members!

Ni mdogo wangu wa mwisho wa kiume miaka 17+ Nashindwa kuelewa ni malezi au nini. Ila mbona sie wengine ndugu zake hatuko hivyo. Naanza kuhofia asije kuona namnyanyasa.

Yaani unaweza kurudi home unakuta kakaa na mavyombo machafu hana habari. Vitu viko hovyo, kupangilia kila kitu kiwe pahala pake, mfano amekula mavyombo kaacha hapo. Kupika anajua ila usafi wa pale anakopikia ni hadi umkumbushe wee naniii embu safisha safisha kidogo hapo sehemu ya kupikia.

Hapo nje anaingia na kutoka ndani, unarudi unakuta mamchanga yamejaa, kabla sijaingia ndani nafanya kuyafagia kidogo mazingira ya nje. Unaweza kuta kitanda hakijatandikwa na yupo tu kashinda nyumbani sijui ni uvivu au ndio uchafu wenyewe.

Siku narudi naingia chumbani nakuta kitanda kiko vururuvururu alivyoamka ndivyo hvyo hivyo,(kidogo nimzabe makofi) hapa alijirekebisha. Mbaya zaidi kila siku namsema. Sio kwamba me ni msafi saaana ila kiukweli me angalau.

Kuhusu usafi wake binafsi hana shida sana.

Nashindwa kuelewa kimalezi mzee alifariki akiwa bado mdogo kama 2-3yrs hivi. Alilelewa zaidi na mama pekee. Nawaza labda malezi ya mzazi mmoja ndio sababu.

Sasa naanza kuona huyu dogo labda anaona tu broo wake nina nongwa.😄
 
Mwelekeze kwa vitendo hakikisha anafanya kwa kumuonesha kwa vitendo huyo bado ni mdogo kwa umri huo wanaume asilimia kubwa tunakuwa na tabia kama huyo kuhusu usafi-.... murlekeze atabadilika taratibuna atakuelewa!

Bado mdogo huyo usife moyo mfundishe usiache!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom