Tumfanyaje huyu dogo?

Tumfanyaje huyu dogo?

Hahaha Daaa jf watu wana mawazo ya kila aina aiseee anyway mi naona jaribu kuangalia upande mwingine Wa shilingi kikubwa tu msife Moyo kwa kuanzia anahitaji msaada Wa kisaikolojia Wa karibu sana hata nyinyi mnahitaji kupata ushauri ni hata gani mchukue unaweza kuwa ni phase tu au inaweza kuwa anataka attention amepoteza wazazi binadamu wana react tofauti sana anaweza kuwa na msongo Wa mawazo ..pengine mtaalamu Wa saikolojia anaweza shauri kama wadau walivyosema kwamba mumuache tu au mchukue hata Fulani huwezi jua mpaka uende kupata huo msaada kwanza ..ungeanzia hapa kabla ya hizo hatua nyingine of course usisahau na imani Mungu yupo ombeni sana !
 
Nina mdogo wangu mtoto wa mama yangu mkubwa alikua hivyo hivyo. Kamaliza fom4 kwa mbinde mzee wake akamfanyia mishe kampuni fulan akawa anapiga kaz na pesa nzuri tu. Akahama kwao akahamia kwa washkaji wake, siku zingine haendi kazini yaan taabu tu. Aliiba kwao tv,deck,king'amuz, mziki mnene wa Sony kiufupi aliiharibu sebule yao na pesa chumbani kwa mzee wake kama kilo kadhaa hivi akazamia Afrika Kusini. Lakini hakufika naskia walilala msitun huko mozambique wenzie wakamwibia kila kitu, baada ya muda km wiki 2 hv akarudi. Akaenda kuomba radhi ofisin kwao akawa anaendelea na kazi lakin kwao hakufika. Siku si nyingi akakamatwa wamekwapua simu ya mtu na mwenzie alipigwa sana lakini kuna wasamaria wakamuonea huruma wakampeleka kwao sababu ya heshima ya mzee wake mtaan kwao. Wakadai walipwe tu hasara yao, kumbuka mzee anahasira sebule imekua empty sababu ya mtoto huyo huyo. Alikaa kwao alipopona tu majeraha yake kasepa mazima mpka leo hii hajaonekana huu sasa karibu mwaka mzima. Wanadai yupo afrika kusini na kuna jamaa wa mtaan mara nyingi huenda na kurudi south afrika nafahamiana nae aliwah kuniambia mdogo wako nimemwona durban na akanipa na namba ya simu ya kumpata.
Ushaur wangu, mwambien azamie kwa madiba atawapunguzia stress. Huyo dogo yupo tu huko anaunga unga maisha atleast akiwa kwny ardhi ya watu atapata akili. Lakini kumbuka uhai ndio upo rehani hapo
 
Back
Top Bottom