Tumezidi ushamba

Mkuu ule ulikuwa ni uhalifu, kwa hiyo ni sawa waandamane kulaani vitendo hivyo vya kihalifu. Hivi unafikiri wangekuwa ni watu waliokutwa na hatia na kustahili adhabu ya kifo hao wanaigeria wangeandamana?? Suala la ndege kukamatwa ni la kisheria, tunadaiwa na anayedai alishinda kesi ya madai dhidi ya serikali yetu. Sasa hao walioandamana wanataka serikali ya SA itengue uamuzi/hukumu ya mahakama!!. Nchi za wenzetu wanaheshimu utawala wa sheria.
 
Hata hapa TZ sheria inaruhusu kukamatwa mali za mdaiwa. Umesahau yaliyompata Mbowe?
 


Hapa Tz katiba inaruhusu watu au vyama ya siasa kuandamana kupinga au kuishinikiza serikali jambo fulani, lakini ni nani anaweza leo kuandamana kwa mujibu wa katiba??!!, kinyume chake Watz wanaandamana kupinga hukumu ya Mahakama wakati jambo hilo ni lazima lipingwe kwa kufuata taratibu za ki-mahakama. Ni ujinga mkubwa wameuonyesha.
 
Hoja yako ya Al Bashiri na ndege yetu ina mambo mawili. Moja linafanana na jingine ni tofauti kabisa. Linalofanana ni hukumu ya mahakama, KUKAMATA. La pili ambalo linaleta tofauti hapo ni kwamba Al Bashiri ni Binadamu na ile ndege yetu ni Asset. Kesi ya Al Bashiri na ya Ndege yetu hazifanani. Moja ni kesi ya jinai na nyingine ni kesi ya madai.
 
hayo maandamano lazima gavana wa darisalama ana mkono wake!.
 
Na jamaa yangu huwa hueleweki kabisa, mara umsifie Magu na kuponda upinzani, unashangaa watu kuandamana? Mbona hukushangaa walipoipokea ndege kwa ngoma?
Mikononi mwa CCM, hutaona Tanzania iliyoendelea isipokuwa Tanzania iliyochakaa.
Serikali huwa haifanyi Biashara, zaidi ya kukusanya kodi, US hata Lockheed Martin ni ya watu binafsi na serikali ya US hununua silaha zake hapo
Ili nchi iendelee ni lazima uchumi uwe mikononi mwa watu na siyo serikali.
 
Wale wabeba mabango hata pa kuingilia airport hawapajui. Mamluki tu wale.
 
Wasukuma /wakazi wa kanda ya ziwa na ushamba ni sawa na pipa na mfuniko
 

Ni hivi;

Siyo kwamba sieleweki. Ni kwamba wewe na wenzako walio kama wewe ndo hamnielewi na sidhani kama mna uwezo wa kuelewa.

Mmeshazifunga akili zenu. Mnadhani ni lazima mtu awe na upande mmoja tu, basi.

Mimi sipo hivyo. Siangalii wala siegemei upande.

Nasimamia kile ninachokiamini na ninachokiona kuwa ndicho kilicho sahihi bila kuangalia rangi wala itikadi za vyama.

Hakuna ugumu wowote hapo katika kuuelewa msimamo wangu.

Kuhusu upokewaji wa ndege, ni ama umesahau au hujui. Kitendo hicho nilikiponda.

Sasa sijui hukuona au umeamua tu kuifunga akili yako.
 
Mkuu na wewe si umeongeza ukubwa wa kundi la washamba? Mpaka ukakaa na wewe ukaanzishe thread ya ndege una tofauti gani na hao 'washamba' walioandamana?
 
Hapo walimaanisha watupe ndege bure bure bila kufuata sheria kwa kuwa tumewasaidia sana enzi za kupigania haki yao..kwa kweli huu ushamba unazidi kutuaibisha kimataifa tunaonekana ni nchi ya wapumbavu
Ushamba Gani HAPO Sasa Acha Kutuaminisha Ujinga,, Kama Wewe Ndiye Mjanja Hamia Kwa Wajanja Wenzako Kwani Umelazimishwa Kuishi Hapa Tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…