Hoja zako hakika ni fikirishi. Wengi wetu humu tutashangilia au kuhuzunika kwa uamuzi wowote wa Lowassa. Lakini ukweli unabaki kwamba ni maisha yake Lowassa kama Lowassa, ambayo katu hayagusi maisha yetu na familia mmoja mmoja.Umepangilia hoja zako vizuri.... Je nikisema tena wakati utaamua kutakuwa na ubaya wowote? I mean nimeandika nawe umeandika! Ni haki yetu sote so long hatuvunji sheria na taratibu za JF na tunabishana kwa hoja.. Ni wakati sasa wa kusubiri kuona muda utatuletea nini
Siasa ni mchezo mchafu! Hakuna msafi awezae kushiriki mchezo huoNasikitika kuona kwamba mpaka leo wengi wetu hatujui maana ya siasa ndio maana tubakuwa vibaraka wa vyama flani.
Kama uko smart na unawaza mbali huwezi kuchezewa kama mpira, niliona haya mambo miaka 2 ilopita na sasa nachekelea tu ninavoona yakitimia, sina kihoro kabisa japo nawasikitikia watanzania wengi ambao bapo gizani bawana utashi juu ya maisha yako wanadhani kiongozi flan anaweza kuwapa faraja.
Ushauri wangu think beyond what u see with ua normal eyes.
who wrote this? alikuwa emotional hasa na emeelezea kila kitu. Thanks for sharing bro, kudos
Sijui kama comment hii itaonwa, kusomwa na kueleweka. Pengine ndiyo comment bora na yenye uhalisia kuliko zote hapa. Asante sana mkuu !!!Kama kuna kitu ambacho kinagharimu upinzani hivi sasa ni kutoambiana ukweli. Badala ya kumlaumu Mbowe kwa kuwaingiza mkenge hakuna anayerudi nyuma kutadhimini ahadi zake na jinsi alivyopuuza ushauri wa katibu mkuu hatua za kuchukua kwa hawa wageni wanaohamia kabla ya kuwapa nafasi walizopewa. Mnajadili tukio la sasa! Kwanini CCM wasiendelee kutawala kwa hizi akili? Mlipigwa ganzi wakati ule na mnapigwa ganzi nyingine. Hivi kuna ugumu gani kuona Dr Slaa alikuwa sahihi na nyie hamkuwa sahihi mkajisahihisha ili mfute makovu mambo yasonge? Inafikia mahali hadi viongozi wakubwa wanasema Lissu tu akiondoka ndio watasikitika ila takataka zingine ziende!!!! Lissu akiondoka Chadema ndio ife? Kuna taasisi hapo? Mkiendelea kushipaza shingo mnaenda kubaki na Chadema kama NCCR ya Mbatia! Akina Lissu wametokea NCCR iliyokufa ....wao watapata platform nyingine siasa ziendelee .....tutajenga upinzani mpya hadi lini? Mbona mnasahau haraka?
mshana jr, Hoja ya pili, niliyonukuu hapo, juu ni dhaifu kwa kuwa dhana yake ni kwamba Lowassa ndiye mwamuzi wa mwisho wa siasa za nchi hii
mshana jr kumbuka kuwa jina la Lowassa lilipokatwa CCM, ikafiatutiwa na sekeseke mkutano wa NEC wengi, nadhani na wewe, uliamini CCM ndiyo mwisho, mbendembende kifo cha mende. Matokeo unayajua.
mshana jr, hoja ya mwisho, nukuu hapo juu, nakubaliana na wewe ila nakukumbusha kuwa, nje ya ndani ya uongozi wa CCM (kwa maana ya vikao vyake), kila mwanachama ana nguvu. Lakini ndani ya chama, nguvu ya mwanachama mmoja mmoja haipo. Mwanachama anakihitaji chama kuwa na nguvu na chama hakimhitaji mtu mmoja mmoja kuwa na nguvu.
Hitimisho ni kwamba kurejea au kutokurejea kwa Lowassa CCM kuna tija/hasara kwa Lowassa kama Lowassa, BASI. Rejea hotuba zake zote ndani na nje ya CCM. Ila nina uhakika CHADEMA itaathirika sana akirejea CCM na sababu ziko nyingi km amewezesha kupata wabunge wengi - na Team Lowassa. Lakini CCM mpya, kama Lowassa hakujipanga vizuri jinsi ya kurejea, Team Lowassa itasambaratIka.
NI MAONI YANGU TU
hizi mambo ndio zinafanya TZ izidi na kuendelea kuwa maskini, waTZ watu wa matukio hasa yasiyo na kichwa wala miguu..
saa hizi watu wanawaza innovations za kukabiliana na baridi/winter ili lisidhuru utendaj kaz na uzalishaji....waTZ badala ya kuwaza cha kufanya kutatua matatzo yenu hasa hayo ya mafuriko wanabaki kununuana na kuhamahama vyama tuu,
yaani its too rubish...media coverage zimejaa huo upuuzi tu!
aibu sana kwakweli.[emoji24]
Mkuu vijana wengi wanaojifanya wapambanaji kama upo JF muda kidogo utagundua tatizo kubwa kwao. Inatugharimu mno! Wao wanarukia kila tukio na hawahoji viongozi wao. Ndio maana ni rahisi kuchezewa kijinga na siasa za kutiana moyo while viongozi wamefanya blunders. Haina tofauti na Simba na Yanga ....umebaki ushabiki tu hadi kwa viongozi! Nafikiri umeona comment ya Meya wa Chadema bwana Boniface Jacob ....huoni tatizo hapo la kukemea? Wao kazi yao wamefundishwa kumsema Rais aliye madarakani tu!!!Sijui kama comment hii itaonwa, kusomwa na kueleweka. Pengine ndiyo comment bora na yenye uhalisia kuliko zote hapa. Asante sana mkuu !!!