Tumetumbukiaje shimoni na tunajiokoaje kama Taifa?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
Hili tope walilojipaka CCM katika uchaguzi huu watalisafishaje?

Hii mipango ya wizi wa kura nadhani ilifanywa kwa haraka katikati ya kampeni baada ya kupima kina cha maji na kuona kina ni kirefu.

Matokeo yake ndiyo haya kura zinakamatwa mitaani, na nje na ndani ya vituo vya kupigia kura.

Tanzania tumegeuka tumekuwa kichekesho cha dunia.

Tumejivua nguo wenyewe huku tukijiangalia kwenye kioo.

Ile "intellect," iliyokuwapo ndani ya enzi za "chama," haikurithishwa chini kwa vijana?

Nimejifunza kutia kicheko mahali pa kunipa majonzi.

Vinginevyo ningekuwa na huzuni ya kudumu.

Hivi kweli ndani ya CCM katika viongozi wakuu waliopita kweli hawaoni kama tunalo tatizo linalohitaji kurekebishwa?

Nina rafiki zangu CCM toka matokeo ya uchaguzi tukikutana wanashindwa kunitazama machoni.

Nahisi kama vile wamefedheheka wanaona aibu.

Kura zinastaajabisha.
IMG-20201030-WA0210.jpg
 
Kura zinastaajabisha.View attachment 1616336
Acha uongo? Wapinzani mmepoteana baada ya kuwa pingapinga! Kajipangeni upya, Bashiru aliwaambia "tunapambana na upinzani dhaifu haijawahi kutokea" magufuli alivyokua anapiga kampeni kuwa na connection wananchi tulimuelewa! Afu mda mwingi mlichokuwa mnaongea kwenye kampeni pumba tupu, wala ilani yenu hamkuinadi, sasa mlitaka nani awachague?
 
Shamba...
Nimekusoma.

Hapana niliyoandika si uongo kama ulivyoandika wewe si uongo ni fikra tu kama ulivyoona uchaguzi ulivyoendeshwa.
 
Bashiru ni nani Mkuu ?

Bashiru si lolote wala si chochote.

Hapo CCM yupo kwa kuwekwa tu kama sehemu ya Ajira, hana usemi wala maamuzi yoyote.

Aombe tu Mungu kukuche salama, maana Shetani hana rafiki.
 
Hili tope walilojipaka CCM katika uchaguzi huu watalisafishaje?

Hii mipango ya wizi wa kura nadhani ilifanywa kwa haraka katikati ya kampeni baada ya kupima kina cha maji na kuona kina ni kirefu.

Matokeo yake ndiyo haya kura zinakamatwa mitaani, na nje na ndani ya vituo vya kupigia kura.

Tanzania tumegeuka tumekuwa kichekesho cha dunia.

Tumejivua nguo wenyewe huku tukijiangalia kwenye kioo.

Ile "intellect," iliyokuwapo ndani ya enzi za "chama," haikurithishwa chini kwa vijana?

Nimejifunza kutia kicheko mahali pa kunipa majonzi.

Vinginevyo ningekuwa na huzuni ya kudumu.

Hivi kweli ndani ya CCM katika viongozi wakuu waliopita kweli hawaoni kama tunalo tatizo linalohitaji kurekebishwa?

Nina rafiki zangu CCM toka matokeo ya uchaguzi tukikutana wanashindwa kunitazama machoni.

Nahisi kama vile wamefedheheka wanaona aibu.

Kura zinastaajabisha.View attachment 1616336
Ebu tuachane na uzushi na hoja za kitoto.

Una masikio ukasikia kile kichonadiwa kwenye Ilani ya CCM/CHADEMA ya Uchaguzi, 2015

Una macho umeona kilichotekelezwa na Serikali ya CCM/ viongozi wa CHADEMA, 2015-2020.

Wananchi (ikiwa ni pamoja na wewe na mimi) wamepima matokeo na kufanya uamuzi.

Upuuzi wa kuibiwa kura tuondokane nao ili wewe na mimi tushiriki kwa pamoja kwa maendeleo yetu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla
 
Mwenengeso,
Kuna watu wengi wamekamatwa na kura za wizi.

Hili ndilo ninalozungumza.
 
Maamuzi ya wananchi yaheshimiwe, wameamua Magufuli anawatosha kwa miaka 5 mingine kwenye box la kura.

Hongera Magufuli, Hongera Mwinyi ,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA.
 
Maamuzi ya wananchi yaheshimiwe, wameamua Magufuli anawatosha kwa miaka 5 mingine kwenye box la kura.

Hongera Mgufuli, Hongera Mwinyi ,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA.
Huyu kiumbe wa Lumumba hata Twitter mmejaa, yaani mmekariri namna ya kumalizia hapo chini. Na mna ID's kibao
 
Hili tope walilojipaka CCM katika uchaguzi huu watalisafishaje?

Hii mipango ya wizi wa kura nadhani ilifanywa kwa haraka katikati ya kampeni baada ya kupima kina cha maji na kuona kina ni kirefu.

Matokeo yake ndiyo haya kura zinakamatwa mitaani, na nje na ndani ya vituo vya kupigia kura.

Tanzania tumegeuka tumekuwa kichekesho cha dunia.

Tumejivua nguo wenyewe huku tukijiangalia kwenye kioo.

Ile "intellect," iliyokuwapo ndani ya enzi za "chama," haikurithishwa chini kwa vijana?

Nimejifunza kutia kicheko mahali pa kunipa majonzi.

Vinginevyo ningekuwa na huzuni ya kudumu.

Hivi kweli ndani ya CCM katika viongozi wakuu waliopita kweli hawaoni kama tunalo tatizo linalohitaji kurekebishwa?

Nina rafiki zangu CCM toka matokeo ya uchaguzi tukikutana wanashindwa kunitazama machoni.

Nahisi kama vile wamefedheheka wanaona aibu.

Kura zinastaajabisha.View attachment 1616336
Kuna msukuma mmoja ukimkuta anavyotetea ujambazi wa Ccm unabaki kujiuliza huyu mtu ana ubongo kichwani au ubongo wake umeoza
 
Shamba...
Nimekusoma.

Hapana niliyoandika si uongo kama ulivyoandika wewe si uongo ni fikra tu kama ulivyoona uchaguzi ulivyoendeshwa.
Ukweli udhibitika kwa kutumia ushahidi usiotiliwa shaka. Hili nadhani Mkuu unalijua barabara. Kwa tuhuma hizi, Mkuu, bila ushahidi usiotiliwa shaka wengi wetu tunaweza kukushuku kuwa unataka kuleta mfarakano nchi, Mwenyezi Mungu aepushe mbali kadhia hiyo.

Mkuu, sasa jitetee.
 
Binafsi ninajivunia sana kuiheshimisha Katiba ya Jamhuri. niliamka asubuhi, nikaenda kupanga foleni. nikahudumiwa na Makarani wa Uchaguzi. nikapiga kura yangu kadiri ya sera za wagombea nikaendelea na shughuli zangu.

kilichofuata baada ya hapo ni aibu.

kura kwenye mabegi? duuh! kichefuchefu. kinyaa. fedheha.
 
Consequences za huu ubakaji tutaziona miaka miwili inayokuja, kuna wasiwasi wa kulima na meno.
Kama Lengo ni kulinda na kuiimarisha Tanzania kimaendeleo kwa kila nyanja, tupo Tayari. Tusisahau " mchumia juani 'ulia' kivulini "! Sasa kama unataka kuchumia kivulini ujue utalishwa kivulini kwa mipiria kupitia puani ukiwa umelazwa kitandani!!! Nina imani waelewa hatakubali kuchumia kivulini.
 
binafsi ninajivunia sana kuiheshimisha Katiba ya Jamhuri. niliamka asubuhi, nikaenda kupanga foleni. nikahudumiwa na Makarani wa Uchaguzi. nikapiga kura yangu kadiri ya sera za wagombea nikaendelea na shughuli zangu.

kilichofuata baada ya hapo ni aibu.

kura kwenye mabegi? duuh! kichefuchefu. kinyaa. fedheha.
Maccm na mwenyekiti wao shetani ni kizazi chenye laana
 
Huyu kiumbe wa Lumumba hata Twitter mmejaa, yaani mmekariri namna ya kumalizia hapo chini. Na mna ID's kibao
Kufurahia MAENDELEO imekuwa ni dhambi?

Acha hii awamu ya Tano tusonge mbele kimaendeleo halafu 2025 ndio tufanye siasa za Mipasho au Taarab za mwambao kwasasa nchi inahitaji watu serious kama Magufuli.

Hongera Mgufuli, Hongera Mwinyi ,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Matokeo yake ndiyo haya kura zinakamatwa mitaani, na nje na ndani ya vituo vya kupigia kura.
Je, kuna mtu yeyote amekamatwa na hizo kura na kwamba huyo mtu anahusika na walioshinda?
Je, kuna ushahidi wowote wa sanduku la kura kuwa na kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura?
Ni vizuri mnapoongea kuhusu wizi wa matokeo muwe logical, muongee katika namna ambayo inaeleweka bila kuacha maswali. Yaani mseme hizo kura bandia zimeingiaje kwenye kura za ushindi wa washindi?
 
Back
Top Bottom