Tumetumbukiaje shimoni na tunajiokoaje kama Taifa?

Tumetumbukiaje shimoni na tunajiokoaje kama Taifa?

Ebu tuachane na uzushi na hoja za kitoto.

Una masikio ukasikia kile kichonadiwa kwenye Ilani ya CCM/CHADEMA ya Uchaguzi, 2015

Una macho umeona kilichotekelezwa na Serikali ya CCM/ viongozi wa CHADEMA, 2015-2020.

Wananchi (ikiwa ni pamoja na wewe na mimi) wamepima matokeo na kufanya uamuzi.

Upuuzi wa kuibiwa kura tuondokane nao ili wewe na mimi tushiriki kwa pamoja kwa maendeleo yetu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla
Biafsi sikatai udhaifu wa wapinzani vivyo hivyo sikubaliani na uhuni wa CCM. Wizi wa kura si upuuzi kama unavyotaka tuamini, wizi ni halisi umefanyika na walioshirikishwa kufanikisha ni miongoni mwetu, ni ndugu zetu wanasema, matukio mengine tumeyaona mubashara.
Kwanini CCM hamjiamini kiasi cha kulitia taifa letu aibu?
 
Acha uongo? Wapinzani mmepoteana baada ya kuwa pingapinga! Kajipangeni upya, Bashiru aliwaambia "tunapambana na upinzani dhaifu haijawahi kutokea" magufuli alivyokua anapiga kampeni kuwa na connection wananchi tulimuelewa! Afu mda mwingi mlichokuwa mnaongea kwenye kampeni pumba tupu, wala ilani yenu hamkuinadi, sasa mlitaka nani awachague?
Jibu hoja, mnaenda kuogea mto gani Hilo tope? Hujausikia huo mwangwi unaotoka huko duniani?
 
Habari za kuibiwa kura ziko nyingi na tumetazama hadi video clips.
Mzee wangu,
Zipo pia habari nyingi na video clips ambazo zinadai uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Kwa nini umechagua kuamini hizo za kuibiwa kura?
Karatasi za kura ni karatasi kama karatasi nyingine, mtu yeyote anaweza kutengeneza, akaziwekea vema kwa namna inavyomfaa na kujishikisha kama ushahidi.

Tupate ushahidi wa hayo maboksi aliyoyaona Zitto, kwa kuanzia...
 
Mas
Je, kuna mtu yeyote amekamatwa na hizo kura na kwamba huyo mtu anahusika na walioshinda?
Je, kuna ushahidi wowote wa sanduku la kura kuwa na kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura?
Ni vizuri mnapoongea kuhusu wizi wa matokeo muwe logical, muongee katika namna ambayo inaeleweka bila kuacha maswali. Yaani mseme hizo kura bandia zimeingiaje kwenye kura za ushindi wa washindi?
Acha kuuliza maswali ya kipumbavu basi,msimamizi wa kituo akikutwa na kura za bandia tueleweje ni za nani? Na hizo kura za bandia zote zimepigia kura chama furani kwa wagombea wote,Rais,Bunge na diwani. Kwa akili ya kawaida kabisa ukiulizwa mwenye mzigo ni nani utashindwa kutambua.
 
Mzee wangu,
Zipo pia habari nyingi na video clips ambazo zinadai uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Kwa nini umechagua kuamini hizo za kuibiwa kura?
Karatasi za kura ni karatasi kama karatasi nyingine, mtu yeyote anaweza kutengeneza, akaziwekea vema kwa namna inavyomfaa na kujishikisha kama ushahidi.

Tupate ushahidi wa hayo maboksi aliyoyaona Zitto, kwa kuanzia...
Hata mi nawashangaa mkuu wanolalamika,mkuu alisema mkurugenzi atakaemtangaza mshindi mpinzani anamtumbua.sasa sijui wanashangaa nini?.karatasi za kura kwani kitu gani mkuu eti.
 
Mzee wangu,
Zipo pia habari nyingi na video clips ambazo zinadai uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Kwa nini umechagua kuamini hizo za kuibiwa kura?
Karatasi za kura ni karatasi kama karatasi nyingine, mtu yeyote anaweza kutengeneza, akaziwekea vema kwa namna inavyomfaa na kujishikisha kama ushahidi.

Tupate ushahidi wa hayo maboksi aliyoyaona Zitto, kwa kuanzia...
Mtu yeyote anaweza kutengeneza karatasi za kura? Kwa hiyo mtu yeyote pia anaweza kutengeneza hela? Hujui huo ni zaidi ya uhaini jambo ambalo laweza kugarimu maisha ya watu analisemea kizembe namna hiyo,mlipoam iwa jamana wanachaoisha karatasi za kura mlichukua hatua gani,mngeambiwa chadema au ACT Wana talling center mngeacha kuvamia,
 
Mtu yeyote anaweza kutengeneza karatasi za kura?
Ndiyo, not authentic though!
Karatasi za kupigia kura zilikuwa chini ya uangalizi na kwamba hizo unazoziona kwenye mitandao wamazitengeneza wenyewe kwa makusudi yao na kina Amsterdam...
 
mkuu alisema mkurugenzi atakaemtangaza mshindi mpinzani anamtumbua.
Pia alisema alisema uchaguzi utakuwa huru na wa haki! Na ndiyo maana mkatafuta wagombea na mkafanya kampeni, kwenye boksi la kura wananchi wakawakataa...
 
Mwanakulitafuta Ni mwanakulipata,.
Watu wengi wanaishia mitandaon ila kura hawapigi..
 
Mzee wangu,
Zipo pia habari nyingi na video clips ambazo zinadai uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Kwa nini umechagua kuamini hizo za kuibiwa kura?
Karatasi za kura ni karatasi kama karatasi nyingine, mtu yeyote anaweza kutengeneza, akaziwekea vema kwa namna inavyomfaa na kujishikisha kama ushahidi.

Tupate ushahidi wa hayo maboksi aliyoyaona Zitto, kwa kuanzia...
Tindi...
Mimi nimetoa fikra zangu.
Ikiwa huamini niliyosema hakuna shida.
 
Promota wa udini mohammed said
USSR,
Una haki na unavyonisoma na kunielewa.

Hadi kufikia leo nimeandika vitabu 10 vingi katika hivi ni historia ya Waislam na juhudi walizofanya katika kupambana na ukoloni kuanzia enzi za Wajerumani.

Pamoja na vitabu hivi nimeandika makala sijui idadi yake.

Sababu ya kufanya hivi ni pale nilipotambua kuwa historia hii ilikuwa ikihujumiwa kwa nia ya kuifuta.

Kitabu changu cha kwanza ni maarufu sasa nilipoandika maisha ya Abdulwahid Sykes na jinsi alivyounda chama cha TANU chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika.

Wako ambao hawakupendezewa na hili kwani tayari walikuwa na historia yao.

Mmoja wa walioghadhibishwa na ukweli katika yale niliyoyarejesha katika historia ya Tanganyika nadhani ni wewe na ndiyo hapo unaniandika kwa kejeli "Promota wa Udini."

Kwa kuhitimisha napenda nikufahamishe kuwa ni kutoka na kitabu cha Abdul Sykes na ukweli nilioeleza ndipo ikaonekana yaandikwe maisha ya Julius Nyerere ili ielezwe na yeye nini mchango wake alipokuwa kazungukwa na kundi lile la Waislam waliopigania uhuru ws Tanganyika wazalendo kama Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Sheikh Rashid Sembe, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Titi Mohamed kwa kuwataja wachache.
 
Ebu tuachane na uzushi na hoja za kitoto.

Una masikio ukasikia kile kichonadiwa kwenye Ilani ya CCM/CHADEMA ya Uchaguzi, 2015

Una macho umeona kilichotekelezwa na Serikali ya CCM/ viongozi wa CHADEMA, 2015-2020.

Wananchi (ikiwa ni pamoja na wewe na mimi) wamepima matokeo na kufanya uamuzi.

Upuuzi wa kuibiwa kura tuondokane nao ili wewe na mimi tushiriki kwa pamoja kwa maendeleo yetu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla
mkuu mwambie basi baba yenu arudishe intaneti kama zamani kazi zinakwama huku makazini maana speed ya kinyonga kama ushindi si ashajipa
 
Ndiyo, not authentic though!
Karatasi za kupigia kura zilikuwa chini ya uangalizi na kwamba hizo unazoziona kwenye mitandao wamazitengeneza wenyewe kwa makusudi yao na kina Amsterdam...
Harafu serikari ika hukua hatua gani?
 
Back
Top Bottom