Tumetumbukiaje shimoni na tunajiokoaje kama Taifa?

Tumetumbukiaje shimoni na tunajiokoaje kama Taifa?

Hili tope walilojipaka CCM katika uchaguzi huu watalisafishaje?

Hii mipango ya wizi wa kura nadhani ilifanywa kwa haraka katikati ya kampeni baada ya kupima kina cha maji na kuona kina ni kirefu.

Matokeo yake ndiyo haya kura zinakamatwa mitaani, na nje na ndani ya vituo vya kupigia kura.

Tanzania tumegeuka tumekuwa kichekesho cha dunia.

Tumejivua nguo wenyewe huku tukijiangalia kwenye kioo.

Ile "intellect," iliyokuwapo ndani ya enzi za "chama," haikurithishwa chini kwa vijana?

Nimejifunza kutia kicheko mahali pa kunipa majonzi.

Vinginevyo ningekuwa na huzuni ya kudumu.

Hivi kweli ndani ya CCM katika viongozi wakuu waliopita kweli hawaoni kama tunalo tatizo linalohitaji kurekebishwa?

Nina rafiki zangu CCM toka matokeo ya uchaguzi tukikutana wanashindwa kunitazama machoni.

Nahisi kama vile wamefedheheka wanaona aibu.

Kura zinastaajabisha.View attachment 1616336
Hizo kura milioni 60 zimehesabiwa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone
 
Ebu tuachane na uzushi na hoja za kitoto.

Una masikio ukasikia kile kichonadiwa kwenye Ilani ya CCM/CHADEMA ya Uchaguzi, 2015

Una macho umeona kilichotekelezwa na Serikali ya CCM/ viongozi wa CHADEMA, 2015-2020.

Wananchi (ikiwa ni pamoja na wewe na mimi) wamepima matokeo na kufanya uamuzi.

Upuuzi wa kuibiwa kura tuondokane nao ili wewe na mimi tushiriki kwa pamoja kwa maendeleo yetu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla
Kushinda kwa kura feki na ilani ya uchaguzi kuna uhusiano gani?!
 
Kuna fake na original templates usisahau, Mkuu.
Mkuu kama ulipiga kura ni wazi zile karatasi ni very unique hardly to forge...na kama unaonelea zinaweza fojiwa basi ni kweli jamana walipata kazi ya kuziprint na wakazireplicate.... baada ya yote waambie hawa majamaa zako waachie mtandao sasa maana washamaliza aibu zao.
 
Wagombea kwenye maeneo hayo naamini wamechukua ushahidi kupinga matokeo. Huo ndio ustaarabu na siyo kubwabwaja kwenye mitandao ya kijamii.

Tusiishi kama wanyama wasiokuwa na kanuni?
Wacha jazba, aibu zenu mmezitafuta wenyewe.
 
Mkuu kama ulipiga kura ni wazi zile karatasi ni very unique hardly to forge...na kama unaonelea zinaweza fojiwa basi ni kweli jamana walipata kazi ya kuziprint na wakazireplicate.... baada ya yote waambie hawa majamaa zako waachie mtandao sasa maana washamaliza aibu zao.
Mkuu, inafojiwa ela ya Marekani yaani dola. Marekani inayojinasibu inateknolojia ya ya sasa kupeleka kiumbe hai Sayari ya Jupiter sembuse karatasi za Tume ya NEC!?
 
Maamuzi ya wananchi yaheshimiwe, wameamua Magufuli anawatosha kwa miaka 5 mingine kwenye box la kura.

Hongera Magufuli, Hongera Mwinyi ,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA.

Zile kura zilizokamatwa ndo wananchi waliamuwa kabla hata ya siku ya uchaguzi hii nchi mtu akiwa mjinga anadhani na wengine wajinga kama yeye sijui ni kwanini
 
Je, kuna mtu yeyote amekamatwa na hizo kura na kwamba huyo mtu anahusika na walioshinda?
Je, kuna ushahidi wowote wa sanduku la kura kuwa na kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura?
Ni vizuri mnapoongea kuhusu wizi wa matokeo muwe logical, muongee katika namna ambayo inaeleweka bila kuacha maswali. Yaani mseme hizo kura bandia zimeingiaje kwenye kura za ushindi wa washindi?
Mbona simple sana, kura zimewekwa kwenye masanduku kabla hata watu hawajaanza kupiga, saa moja asubuhi huko Kigoma Zitto alisema anashangaa aliona sanduku linatolewa eti limeshajaa, wakati wapiga kura ndio kwanza wanaanza kujitokeza vituoni.

Mawakala hawakuwepo vituoni, kituo changu palikuwepo na Mwenyekiti wa S/M na watendaji wake, hawa wote ni CCM, wataachaje kukibeba chama chao kwenye mazingira ya uwepo wa kura nyingi feki zilivyokuwa zimezagaa mitaani zikiwa tayari zimewekwa tiki wagombea wa CCM nafasi ya Udiwani, Ubunge, na Urais.

Nyingine zikafichwa vituo vya polisi, nyingine wakapewa wasimamizi wa uchaguzi wakazificha kwenye mabegi meusi wakaingia nazo vituoni, usipoamini haya utakuwa na matatizo ya akili.
 
Wagombea kwenye maeneo hayo naamini wamechukua ushahidi kupinga matokeo. Huo ndio ustaarabu na siyo kubwabwaja kwenye mitandao ya kijamii.

Tusiishi kama wanyama wasiokuwa na kanuni?
Mwengezo,
Tujadili tu kiungwana hapana haja ya lugha zinazokaribia matusi.

Mitandao ya kijamii ni barza tunajadili mambo yetu.
 
Mkuu, inafojiwa ela ya Marekani yaani dola. Marekani inayojinasibu inateknolojia ya ya sasa kupeleka kiumbe hai Sayari ya Jupiter sembuse karatasi za Tume ya NEC!?
Mkuu am resting my case...mmelitia najisi taifa kila kona ya dunia inatuzodoa
 
Ukweli udhibitika kwa kutumia ushahidi usiotiliwa shaka. Hili nadhani Mkuu unalijua barabara. Kwa tuhuma hizi, Mkuu, bila ushahidi usiotiliwa shaka wengi wetu tunaweza kukushuku kuwa unataka kuleta mfarakano nchi, Mwenyezi Mungu aepushe mbali kadhia hiyo.

Mkuu, sasa jitetee.
Tujitegemee,
Nani chanzo cha farka?

Yule aliyekamatwa mfuko wa kura nje ya kituo au yule aliyetuarifu tukio au mwandishi hapa barzani?
 
Mkuu am resting my case...mmelitia najisi taifa kila kona ya dunia inatuzodoa
At the moment, I guess for you, that is the best way of gentlemanly accepting the defeat in the " battle of arguments ".
 
Je, kuna mtu yeyote amekamatwa na hizo kura na kwamba huyo mtu anahusika na walioshinda?
Je, kuna ushahidi wowote wa sanduku la kura kuwa na kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura?
Ni vizuri mnapoongea kuhusu wizi wa matokeo muwe logical, muongee katika namna ambayo inaeleweka bila kuacha maswali. Yaani mseme hizo kura bandia zimeingiaje kwenye kura za ushindi wa washindi?
Tindi...
Habari za kuibiwa kura ziko nyingi na tumetazama hadi video clips.

Lakini ikiwa unaona si habari zenye ithibati unataka ushahidi wa mahkama hapana neno.
 
Bashiru ni nani Mkuu ?

Bashiru si lolote wala si chochote.

Hapo CCM yupo kwa kuwekwa tu kama sehemu ya Ajira, hana usemi wala maamuzi yoyote.

Aombe tu Mungu kukuche salama, maana Shetani hana rafiki.
Kweli shetani hana rafiki, kawafanya mpigwe kipigo cha mbwa koko! Laana ya lissu alivyosema kupambana na korona kwa maombi ni ujinga!
 
Back
Top Bottom