Tumetengwa katika siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumetengwa katika siasa za Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AridityIndex, Mar 27, 2011.

 1. A

  AridityIndex Senior Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heshima Mbele Wanajamvi

  Hii ni hoja yangu namba moja, katika mfululizo wa hoja nitakazokuwa nazitoa hapa jamvini. pamoja na U-junior wangu kama member lakini nakuhakikishieni kuwa kwa muda wa miaka 3 sasa nimekuwa nikitembelea Jamvi hili na kujionea mijadala mingi inayolihusu taifa letu.

  Nitaeleza kwa kifupi katika hoja yangu sababu za kuchelewa kujiunga. Sababu ni nyingi lakini kubwa zaidi ni hii hali ya kutengwa kwa eneo langu na siasa za Tanzania zinazoendelea. Naomba nieleze bayana kuwa hoja kubwa katika jukwaa hili ni pamoja na hizi hapa.
  1. Umeme-dowans, kiwira, richmond, mgao wa umeme maji kukauka nk
  2. Ufisadi - meremeta, kiwira nk
  3. Udini na malumbano kati ya christian and Muslims
  4.Mbiyo za urais

  kwa bahati mbaya sana huku kwetu nilikozaliwa na ninakoishi haya mambo ni kama vile hayatugusi sana naomba nielezee kila moja.

  Kuhusu Umeme - sisi huku kwetu tuna umeme wa gesi ambao inakadiliwa kuwa tutatumia kwa miaka 300 na wala hakuna mgao wala hakuna kukauka maji kwa hiyo sikuwa na hoja kwa kweli kwenye mijadala ya umeme.

  Kuhusu Ufisadi- hapa tumetofautiana kwa kiasi kikubwa sana kimtazamo mwanzoni tuliamini sana suala
  hili lakini mijadala ilipoamua kumtumbukiza na BWM ambaye sisi tunaamini hataweza kutokea Rais bora zaidi katika nchi hii na tukiamini kuwa yeye ni zaidi ya maraisi wa awamu zote wengine wanamtusi hapo tukabaki kinywa wazi.

  Udini na malumbano ya dini- yaani hapa ndo hatumo kabisa kwetu sisi watu wote tuna ndugu wa dini nyingine kwenye koo zao. Labla niwaeleze kilichotokea ni kwamba katika makabila yetu wale wote waliobaki upande mwingine yaani nchi yetu ya asili ni christian na waliovuka kuja Tz ni muslim lakini koo zetu lugha yetu utamaduni wetu undugu wetu umebaki kama ulivyo na ndiyo maana ukija kwetu utakutana akina anthony omari, Juma Joseph, Rose Abdalah nk. kwa hiyo hapa Watanzania wenzetu mmetuacha mbali kweli.

  Mbiyo za Urais - kwetu sisi tunayemuona kuwa anafaa na tunayeamini kuwa atatenda haki ni Membe Tu sasa akitajwa kwenye mijadala anatukanwa. wakati ukweli ni kwamba ni yeye tu ndiye mwenye uwezo wa kuwaponyesha makovu yenu ya hapo juu amekulia kwenye eneo lisilo na makundi ya kikabila na kidini, siyo fisadi na hana tatizo la umeme.

  Wakati tukiwa na hamu ya kushirikiana na waTZ wengine katika mabadiliko hoja zetu kama soko la uhakika la korosho, Maji, Uvuvi na shule havipewi umuhimu na viongozi wa mageuzi ya kitaifa je tufanyeje?. Tuendelee kujitenga?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Aridity Index,
  Karibu sana jukwaani. Kwa kadri ulivyojieleza ndivyo ulivyobainisha jinsi ulivyo mkabila, ukanda, au mtu mwenye kupendelea na kuona kuwa eneo lake tu ndilo linaloweza kutoa mtawala mzuri. Hii imejidhihirisha jinsi ulivyomtetea Mkapa, licha ya ufisadi aliowatendea Watanzania wote na kugawa madini yetu kwa "wawekezaji" kwa bei ya chee, na jinsi unavyotuarifu kuwa Membe peke yake ndiye anayefaa kuwa rais.Hata hivyo nakukaribisha kwenye jamvi ketu hili la JF.
   
 3. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Mkuu wewe ni nani katika chama cha akina makamba? mpaka tayari kwa nafsi yako uliyoifanya kwa wingi. Mie sioni tabu yeyote kuwa Rais, ili mradi achaguliwe kwa haki na wananchi walio wengi. Mkuu umesema Membe hana matatizo ya umeme hapo umekusudia nini?
   
 4. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Mkuu maoni yako si ya kweli mimi nimekaa lindi mjini,nachingwea mtwara mjini Mingoyo na maeneo ya Masasi na Kilwa kivinje ukweli ni kuwa ukiondoa masasi maeneo mengine udini ni mkubwa kuna mihadhara mingi inaukashifu ukristo kwa kiasicha kutisha,Kuna kanda za mahubiri ya kashfa dhidi ya ukristo ziko mitaani zinauzwa kama njugu,Tafadhari kuwa mkweli.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  AridityIndex,
  Mkuu karibu sana JF na hakika mawazo yako yamepokelewa na bila shaka yatakuwa mchamgo mkubwa ktk janvi hili..
  Sasa kukawia kujiunga kwako kwa miaka mitatu nikiashirio wazi kwamba wewe ndio ulijitenga na wananchi wenzako kwa sababu matatizo ya nchi yetu unayatazama kwa mipaka ya maeneo au uzawa..

  Na nakuhakikishia kwamba Udini, Ukabila na hata umajimbo hutokana na watu kuwa wabinafsi..Kutazama tu maslahi yao kama ndio halali ya yenye maana kwao na sii matatizo ya nchi nzima au hata dunia nzima.

  Swala la umeme:-
  Kwa ujumla wa tatizo hili haliwagusi wananchi kwa sababu ya generator hizo zinafungwa Dar - laa hasha isipokuwa ni kodi yako wewe, mimi na wananchi wengine wote walipa kodi zao kwa shirika feki ambalo limeundwa na viongozi wetu kwa maslahi yao binafsi, tukizingatia ukosefu wa kiutendaji ambao umeshindwa kuanzisha miradi mipya ya umeme kwa zaidi ya miaka 35.

  Kumbuka tu kwamba Tanzania ni Taifa changa ambalo baada ya uhuru halikuwa na miundombinu ya kutosha kukimu mahitaji yake ya kimaendeleo.
  Na changamoto la kujenga miundombinu ilikwisha mara tu baada ya mwalimu kuondoka madarakani na tumekuwa tukifikiria kwamba imetosha na kinachotakiwa sasa ni mfumo bora wa kisiasa na kiuchumi..

  Ni kutokana na ufinyu huo wa kifikra ndio maana wewe na watu wengine wachache wanafikiria mafanikio ya Mkapa ambaye hakuwa na vision nje ya kurekebisha mfumo wa kiutawala ktk ukusanyaji wa fedha na kuuza mashirika yetu..
  Kifupi Mkapa alikuwa DALALI wa maliasili zetu na hivyo sifa zako zinakoma ktk maandalizi mazuri ya Udalali wa Mkapa..

  Sidhani kama unaweza kunambia ni miundombinu gani aliijenga Mkapa na labda turudi toka Mwinyi hadi leo hii tukiwa na JK..nadhani hakuna..

  Sasa kama taifa ni changa ambalo linahitaji kwanza kuwa na miundombinu inayotosheleza mahitaji ya uzalishaji ili tupate maendeleo na viongozi wote waliopita wameshindwa kuliona isipokuwa kujijenga ktk mazingira aloacha mwalimu, ndipo matatizo yote mengine yanapojitokeza..

  Kifupi, kiuchumi Tanzania inafanya biashara zake kama muuza chips vumbi, yaani kila tunaloweza kufanya ni kwa mapana ya karai la kuunguza viazi na kuku, hivyo tumeshindwa kujiandaa kutoka kutumia mkaa, kuongeza kuku na mayai na kufikiria mbele zaidi ktk matumizi ya gas au umeme na kwa kiwango gani kinachohitajika leo,kesho na miaka 20 ijayo...

  Ndio maana tunaambiwa ni asilimia 15 tu ya watanzania wanapata huduma ya umeme na sijui ni asilimia ngapi wanapata huduma ya gas, maji, barabara zenye kiwango cha rami, njia za maji taka na kadhalika....

  Kwa hiyo matatizo yote uliyowahi kuyasoma hapa JF ni matatizo ambayo mwandishi amekuwa na ushahidi au kayasoma mahala na kuyaleta hapa kijiweni ili sote tuyajadili kwa mapana ya athari zake hata kama halituhusu sote moja kwa moja..

  Umemzungumzia Membe kuwa ni kiongozi bora ambaye wewe unamwona kama rais mtarajiwa, lakini pamoja na ubora wake ni lazima utazame mazingira aliyopo..

  Membe kama Membe nayemjua mimi hawezi kushindana na mafisadi, hana ubavu huo hata kidogo na sidhani ktk vision yake anafikiria kukomesha Ufisadi, jambo ambalo wewe unaliona sio deal..

  Mimi nitakwambia tu kwamba:- PAKACHA LINALOVUTA KAMWE KALIWEZI KUJAA...hata kama una nguvu na bidii za mitume.

  Maadam kuna mirija imewekwa kufyonza pato la nchi hatuwezi kuendelea kwa kufikiria kwamba tukiweka bidii kubwa ktk uzalishaji kukidhi shida zetu tutaendelea.. Maendeleo hayapatikani kwa kufuta shida zetu ila malengo yanayotazama mbele ya shida hizi..maendeleo hayapatikani kwa kutafuta riziki ya tumbo na kusubiri kwenda msalani, kisha ule tena..

  Haya ndio makosa ya Jk na viongozi wengine wote wanaopinga kukomesha Ufisadi na kwa bahati mbaya sasa hivi mizizi yake imefika hadi huko makwenu na wanaofurahia haya ni wale waliotegesha mirija yao ktk mfuko wa pato la nchi ili kukidhi njaa zao za tumbo..

  Nitamalizia kwa kusema kwamba Tanzania haiwezi kuendelea ikiwa haitakomesha Ufisadi na pili kujenga miundombinu bora kwanza kabla ya kukimbilia kuongeza hesabu ya mkaa na makarai pasipo kuwekeza ktk miundombinu mipya ati kwa kufikira wananchi wana njaa ya tumbo..

  Wananchi wana kiu na njaa ya Maendeleo na sii jaa ya Tumbo.
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Tunaomba tupe ushahidi japo wa maandishi wa kukashifiwa bibilia maana isiwe inajikashifu yenyewe halafu wewe kwa kuwa huijuwi useme ina kashifiwa? Usipake matope kama unaweza kupaka m**i ukiamuwa kupaka, paka ki ukweli. Leta ushahidi.
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Shit! Mada nzuri inageuka udini. BTW Membe in action
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Mtu akidai bibilia imekashifiwa bila kutoa ushahidi wa ilivyo kashifiwa huyo ndie anapaka matope, huoni kuwa ni bora atoe ushahidi wa uhakika na awe kaipaka hiyo "shit"?
   
 9. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Unataka ushahidi upi fafanua mkuu nakueleza kitu nilichoexpirience kwa miaka kadhaa niliokaa huko what u want sasa..!cjampaka mtu matope
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu hapo kwenye Blue nadhani ni vizuri ungekuja na Source kuliko kutumia akili yako
   
 11. A

  AridityIndex Senior Member

  #11
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mkandara
  Kwa mchango wako mzuri kwenye thread hii, ni kweli ulichosema kuhusu u-biasness wangu kuhusu ukanda lakini mimi ni Mtaalamu wa kilimo ambacho naamini kuwa hadi leo ndiyo sector inayoajiri waTZ wengi. Hakuna uniformed national strategy inayoweza kufanya kazi katika kilimo lakini si sector hiyo tu hata zingine zinazogusa maendeleo na maisha ya watu zinapaswa kuwa specific and compartible to environment, ethnics and culture zao. Kwa minajiri hiyo nilidhani siasa inajadiliwa au inatekelezwa ili kuleta maendeleo hivyo kama issue ni uchumi wetu na maendeleo ya wananchi wetu suala la ukanda halikwepeki mipango ya jumla itaendelea kutufukalisha na hapa ndiyo maana nikaona tumetengwa maana hata Hapa tumejikita kwenye kujadili mipango ya Ujumla ambayo kamwe haihusiani na maendeleo.

  Kuhusu ufisadi- bado mijadala haitoi mwelekeo sahihi ndiyo maana siyo issue kwangu maana watendaji wenye kuthubutu na at least wamefanya vitu tangible kama alivyo mkapa na Lowasa au aliyefanikiwa katika private sector kama RA wote wanaitwa mafisadi na waliowasafi kama alivyo Pinda na Kikwete hakuna wanachofanya wapo tu kama hawapo vile. Kwa hiyo utaona ni jinsi gani mmetuengua wengi katika mijadala hii.

  Kuhusu membe inawezekana asiwe mzuri kwa mtazamo huu wa kutaka watu wakamatwe ovyo, lakini mapendekezo yangu yaliangalia kwenye issue ya usalama pia, kupitia humu JF nimejionea jinsi taifa lilivyo na makundi mbalimbali na ni hatari kwa awamu ijayo kuwa na kiongozi ambaye tayari amejinasibisha na makundi kama yule aliyetoa 10,000,000 kuchangia uzinduzi. wa kanda ya muziki. ni dhahiri anaweza kuleta mfarakano zaidi baina yetu Watz Ni Mtazamo.
   
 12. A

  AridityIndex Senior Member

  #12
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu unahitaji source ya sisi kuamini kuwa mkapa ni bora zaidi ni hivi atleast ameweza kutuunganisha na sehemu nyingine za dunia kama ilivyo mozambique na Dar es salaam, hakuna tatizo la umeme, zahanati na hospitari pamoja na mashule na vyuo vimeanzishwa wakati wake ni kinyume na wakati wa Mwalimu na Mh. Mwinyi. Na huyu wa sasa ndiyo kama vile hayupo tu. inawezekana hata wewe umeanza kuitambua kusini baada ya juhudi hizi za huyu Bingwa.

  Unabishia kuhusu asili ya watu wetu naomba usafiri kuja kwetu na sasa barabara inapitika hadi kule kwenye nchi yetu nyingine, kwa bahati mbaya historia yetu haikuandikwa kwani tulitengwa tangu kipindi hichooooo hivyo sitakupa internet link.
   
 13. A

  AridityIndex Senior Member

  #13
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo sahihi mkuu labla wewe ulitka kuwaambukiza hiyo kitu, maana nina ushahidi katika jimbo langu hiyo imani ni 98% lakini hadi leo mbunge mwenye sifa na aliyependwa ni stephen na kama hali ingekuwa kama ulivyoona wewe nadhani hata uungaji mkono wa vyama vya kisiasa ungekuwa hivyo lakini no. na hali hii ya ku-base kwenye malumbano ambayo ndiyo imegeuka siasa ya Tanzania ndiyo inatutenga zaidi maana sisi hatumo humo Baba Muslim mama christian, shangazi christian binamu Muslim, Nyumba kubwa christian nyumba ngogo muslim mwendo ndiyo huo.
   
 14. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umeingia jamvini ukiwa na agenda maalumu-ukanda na rais ajaye (membe via bwm). Karibu bali umeanza vibaya kwa kujionesha utakuwa bias!!
   
 15. A

  AridityIndex Senior Member

  #15
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Naamini alijaribu kufanya jambo lakini akakosea sawa na yule wa mwanzo aliyejaribu kuanzisha african socialism ikakwama. lakini je utamlinganisha na ambaye hafanyi chochote. Ni dhahiri huyu asiyefanya chochote hatakosea chochote na atakuwa akikana kila jambo kuwa siyo yeye maana ni kweli yeye hafanyi chochote. Kuhusu membe bado ni bora kwa mtazamo wangu kwa kuwa ni mtu anayejali utawala wa sheria ni mstaarabu, na si mwanachama wa makundi hatarishi yaliyo sasa TZ amekulia katika jamii isiyokinzana kimakundi kama ilivyo sehemu zingine za TZ.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  AridityIndex,
  Mkuu unanisikisha sana unaposhindwa kuelewa thamani ya maendeleo ktk uhalisia wake badala yake unatazama nani kaleta mboga mezani..

  Watu kama wewe wapo wengi sana na pasipo kujali picha halisi wanakubali kupokea kile walichoandikiwa na sii halali yao.

  Na fikra kama hizi bila shaka unajiuliza sana kwa nini tulimwondoa mkoloni ambaye alituletea maendeleo zaidi ya viongozi wetu weusi, pasipo kujali ni mali gani waliiba ili kuzijenga nchi zao..

  Sasa mtu kama mimi naelewa umuhimu wa kuwa huru hata kama viongozi wetu wataboronga, lakini sipo radhi kuona viongozi wetu wakigeuka kuwa wakoloni weusi yaani yale yote tuliyoyakataa kwa mkoloni mzungu yanafanywa na viongozi wetu weusi...

  Kwa maana hiyo ndio maana unatuona tukiwashambulia kina Mkapa, Lowassa, Rostam and the likes kwa sababu malengo yao na mkoloni hayana tofauti..

  Hicho kidogo unachokiona wewe sii maendeleo ya nchi na kwa uhakika tazama Tanzania tumesimama wapi ktk index ya maendeleo duniani leo tofauti na miaka 40 iliyopita utagundua kwamba tumeshuka daraja wakati magorogha ndio ya azidi kujengwa... Kwa lugha ya gu husema haya ni makuzi ya kimwili hayana maana tuna afya nzuri au tunaendelea kiuchumi..Hata mtoto mdogo anavyokua hutoka ktk stage za kutumia diapers na akaanza kuvaa kaptula na hata suruali haina maana kipato chake kimeongezeka au kiafya ana afya bora zaidi..

  Sasa kama atadai tumeendelea imekuwaje tushuke daraja tena chini ya nchi ambazo sisi wenyewe tuliwasaidia sana kisiasa na kiuchumi miaka ya nyuma...

  Nadhani mwisho wa siku utagundua kwamba maendeleo ya nchi hutazamwa kwa picha kubwa zaidi ya utajiri na nguvu ya mtu mmoja au sehemu moja..bali taifa zima kwa ujumka wake..

  Na sii hekima kabisa kusifia nguvu na jitihada za mhalifu ktk vielelezo vya maendeleo ya mtu ama nchi na ndio maana sisi tunawakemea kina Mkapa,Lowassa, ukoloni na hata ukoloni mamboleo kwani mafanikio yao yanatokana na kumdidimiza mwingine..
  Kwa hiyo unajenga mabaka zaidi kiasi kwamba kwa kila kumjenga tajiri mmoja ni lazima uwashushe watu elfu kama sii mamillioni...
  Ndio mfumo waliotumia wakoloni na ndio umetumiwa na viongozi wengi wa kiafrika kiasi kwamba hesabu ya maskini inazidi kuongezeka badala ya kuwatoa maskini ktk hatua hiyo na kuwaweka ktk ngazi ya kati yaani middle class...

  Labda nikukumbushe tu kwamba Nigeria imefikia hapo ilipo pamoja na kuwa na utajiri mkubwa sana wa rasilimali watu na maliaaili kubwa lakini wamedata ktk umaskini..

  Wasomi wanasema utajiri wa nchi hiyo umeshikwa na mafisadi asilimia mbili, na maskini ni zaidi ya aslimia 80 ikiongezeka kila mwaka...

  Mfumo wao mzima ni ule wa porini yaani mwenye nguvu mdiye atakula nyama na hakika, Nigeria leo ili mtu atoke kwenye umaskini ni lazima awe tapeli, jambazi au dhulmati kutokana na Ufisadi wa ngazi za juu za kiutawala kushuka hadi kwa walalahoi..

  Hii sio sifa nzuri kabisa na wala sii njia ya kufikia maendeleo ya nchi au kwa mipaka ya majimbo na sidhni kama tunataka kwenda walikofika Nigeria..

  Matatizo yote yanayozikumba nchi za kiarabu na Afrika magharibi yanatokana na kuwepo na matabaka ya walionacho na wasionacho pamoja na kwamba nchi za magharibi zinatumia pia nafasi hiyo ya mgawanyiko kueneza siasa za chuki baina yao...
  Ni rahisi sana kwa nchi tajiri kuwaghiribu watu wenye njaa ya maendeleo kuliko nchi yenye maskini machache...
   
 17. A

  AridityIndex Senior Member

  #17
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkandara,

  Ahsante sana kwa mchango wako wa kina na mapana katika hii hoja, kimsingi nakubaliana na fikra zako lakini nisichoamini ni ile kubadilisha suala la ufisadi kuwa ndiyo msingi wa maendeleo. Mimi najaribu kufikiri zaidi ya hicho kikomo nakumbuka ulikuwepo mjadala humu uliowalaumu wahitimu wa Chuo kikukuu cha Dar kuwa ni wasemaji na walalamishi zaidi kuliko kuwa wabunifu wa kutoa suluhisho la matatizo kwa mtazamo huo nilikuwa najaribu pia kulinganisha mchango wa hao mafisadi kama akina Lowasa BWM na RA kwa taifa hili ukilinganisha wa wale tunaowaita wasafi. ni dhahiri hawa wanaoitwa mafisadi wanasifa ya utendaji zaidi kuliko ile sifa ya wale wana UDSM. Na kwangu mimi nadhani utendaji ndiyo utatufikisha pazuri zaidi kuliko ulalamishi.

  Kuhusu kuangalia maendeleo ya mtu mmoja mmoja nadhani hapa pia kuna tatizo ni kama taifa halijuwi tunachokifanya kwa sababu tayari tulishakubaliana kuwa uchumi wetu utaendeshwa na private sector na serikali itasimamia tu na kukusanya kodi. Na hapa ndipo tunapokosa utashi tunasema tusichokijua na kutekeleza madudu tu yasiyojulikana. Mkandara mimi naamini kuwa bado tuko kwenye stage ya kutegemea maendeleo kutokana na rasilimali moja kwa moja (land, water, mining, wildlife) hivi vitu vimetofautiana kutoka kanda moja kwenda nyingine, mbaya zaidi hatuwezi kujenga nyumba hewani bila kutumia vema rasilimali hizi.

  Nakataa kujadili suala la maendeleo ki-utaifa labla tujadili foreign affairs, ulinzi wa mipaka, nk. nadhani nilikumbusha sehemu flani kuwa hii mijadala ina-exclude korosho na ufuta na mihogo lakini pia uvuvi sasa mimi sioni wapi tutapenya kufikia maendeleo.Hakuna anayejadili matumizi sahihi ya umeme ule uliojaa mnazi bay.Tuanzie hapa ili tuliendeleze eneo hili na taifa la Tanzania.Siasa ziwe kwa ajili ya maendeleo msiendelee kututenga.

  Lakini pia mkuu nadhani unakumbuka jinsi tulivyoangukia pua tulipojaribu kuendelea kwa pamoja kupitia vijiji vya ujamaa na mashirika ya umma, je unashauri tujaribu tena? iwapo tulishindwa hata wakati aliyeanzisha hayo mawazo yupo sembuse sasa hayupo tena!!!!.

  Kwa bahati mzuri nimeishi Asia kwenye nchi zinazoendelea, Europe kwenye nchi zilizoendelea na Afrika hasa TZ ambako tumesimama tu hatuendelei. Kwa mtazamo wangu nahisi tumejisogeza zaidi katika sera za kundi la walioendelea na ku-skip stage hii ya wa-Asia wanaoendelea. Bado kwangu mimi mtu mwenye hulka kama za EL, BWM na RA ndiyo wanafaa kuongoza.

  Mara Nyingine nitaelezea jinsi mkuu wa mkoa wetu alivyobuni mbinu za kuiba pesa kutokana na mfumo wa uuzaji mazao, lakini akawa amesaidia kwa kiasi kikubwa sana kupandisha thamani na kuboresha masoko ya korosho.

  Once again thank you for valuable contribution.
   
 18. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  sa wewe unatuchanganya, post yako inaonesha wewe si raia wa apa na chimbuko lako ni tata. Pia unamtaka membe ndo awe rais wako wakati membe yupo mserikalini kitambo na kama amefanya jambo kuu la kukumbukwa ni kumsindikiza rais ktk mikutano ya kimataifa kama msindikizaji bila kujali cheo chake pia akifika mikutano mikubwa ansinzia wakati kwenye ndege anatembea ktk executive Class ambako anapumzika vya kutosha, rejea mkutano wa ivi karibuni alipokwenda na rais na picha zake za kulala fofofo mkutanoni zipo hapa jf? uyu atakuwa rais gani? ila kuytokana na hesabu za probability kila raia akipewa nafasi ya kumchagua rais amtakaye kati ya rais mil.30 wapiga kula, wote million 30 wataqualify.
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  majimshindo darasani ulikuwa unakuwa wa ngapi kama uelewi ivi? jamaa kasema kukashifu ukristo wewe unadakia kukshifu biblia? au ndo kazi yako iyo?au unaona kila kitu sawa? nashindwa kupata taswira ya fikra zako!
   
 20. A

  AridityIndex Senior Member

  #20
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana mimi ni raia wa hapa, ila siyo muumini wa mipaka ya kisiasa na kikoloni ni muumini wa mipaka ya kimaendeleo.

  Kulala siyo tatizo kwani hujuwi siku hizi watu wakilala wanaoteshwa suluhisho la matatizo ya watanzania? umesahau ndoto ya Ambilikile kule Loliondo?kwkwkwkw (joke).

  Narudia tena Membe anatufaa kwa sababu katika maeneo yenu tayari mna makundi na hamuaminiani tena yeye hayumo kwenye hayo makundi ingawa yuko serikalini. Na kuhusu suala la maendeleo yetu tunahitaji kujipanga vyema kimikakati tena mikakati iliyo mahusi kwa kila kanda siyo kutegemea state house tena is crazy!!!!!Tukijadili kwa mitazamo ya namna hii hamtatutenga tena. Kwa sasa mmetutenga hatujuwi pa kuanzia, na si vema tukashabikia tu mambo kama tunavyoshabikia arsenal na manchester United. Lazima tuguswe kwani siyo wote tunaoishi hapo Dar.

  Nadhani tutumie vema fursa hii ya kuunda katiba mpya kuondoa huu upuuzi wa kutegemea state house, na ndiyo maana naona membe anafaa kuongoza nchi maana kinachohitajika sasa ni kuwasuluhisha tu matajiri wawapende masikini na masikini wawapende matajiri, wasomi wapende wasiosoma, middle class wawapende upperclass.
   
Loading...