Tumetengwa katika siasa za Tanzania

Tumetengwa katika siasa za Tanzania

Aridity Index,
Karibu sana jukwaani. Kwa kadri ulivyojieleza ndivyo ulivyobainisha jinsi ulivyo mkabila, ukanda, au mtu mwenye kupendelea na kuona kuwa eneo lake tu ndilo linaloweza kutoa mtawala mzuri. Hii imejidhihirisha jinsi ulivyomtetea Mkapa, licha ya ufisadi aliowatendea Watanzania wote na kugawa madini yetu kwa "wawekezaji" kwa bei ya chee, na jinsi unavyotuarifu kuwa Membe peke yake ndiye anayefaa kuwa rais.Hata hivyo nakukaribisha kwenye jamvi ketu hili la JF.

He managed to speak his heart; amekuwa mkweli lakini je ukweli wake ndiyo wetu? Hapo tu ndo tunatofautiana naye afadhali angeamua kutumia mmoja kati ya Membe na Mkapa kuondoa bias aliyokuwa nayo. Kwavile ni junior mwenzangu basi acha nimpe moyo, karibu jamvini. Mi mwenzako Babu waloliondo ndo alinifanya niunge unachama maana niliona kondoo wangu wanapotea kumbe nikagundua hawapotei kiroho tu hata kimwili pia wanapotezwa na ufisadi basi nikaamua kuwa permanent japo wakati najiunga nilidhani dumu kwa siku moja tu.
 
Mkandara,

Ahsante sana kwa mchango wako wa kina na mapana katika hii hoja, kimsingi nakubaliana na fikra zako lakini nisichoamini ni ile kubadilisha suala la ufisadi kuwa ndiyo msingi wa maendeleo. Mimi najaribu kufikiri zaidi ya hicho kikomo nakumbuka ulikuwepo mjadala humu uliowalaumu wahitimu wa Chuo kikukuu cha Dar kuwa ni wasemaji na walalamishi zaidi kuliko kuwa wabunifu wa kutoa suluhisho la matatizo kwa mtazamo huo nilikuwa najaribu pia kulinganisha mchango wa hao mafisadi kama akina Lowasa BWM na RA kwa taifa hili ukilinganisha wa wale tunaowaita wasafi. ni dhahiri hawa wanaoitwa mafisadi wanasifa ya utendaji zaidi kuliko ile sifa ya wale wana UDSM. Na kwangu mimi nadhani utendaji ndiyo utatufikisha pazuri zaidi kuliko ulalamishi.

Kuhusu kuangalia maendeleo ya mtu mmoja mmoja nadhani hapa pia kuna tatizo ni kama taifa halijuwi tunachokifanya kwa sababu tayari tulishakubaliana kuwa uchumi wetu utaendeshwa na private sector na serikali itasimamia tu na kukusanya kodi. Na hapa ndipo tunapokosa utashi tunasema tusichokijua na kutekeleza madudu tu yasiyojulikana. Mkandara mimi naamini kuwa bado tuko kwenye stage ya kutegemea maendeleo kutokana na rasilimali moja kwa moja (land, water, mining, wildlife) hivi vitu vimetofautiana kutoka kanda moja kwenda nyingine, mbaya zaidi hatuwezi kujenga nyumba hewani bila kutumia vema rasilimali hizi.

Nakataa kujadili suala la maendeleo ki-utaifa labla tujadili foreign affairs, ulinzi wa mipaka, nk. nadhani nilikumbusha sehemu flani kuwa hii mijadala ina-exclude korosho na ufuta na mihogo lakini pia uvuvi sasa mimi sioni wapi tutapenya kufikia maendeleo.Hakuna anayejadili matumizi sahihi ya umeme ule uliojaa mnazi bay.Tuanzie hapa ili tuliendeleze eneo hili na taifa la Tanzania.Siasa ziwe kwa ajili ya maendeleo msiendelee kututenga.

Lakini pia mkuu nadhani unakumbuka jinsi tulivyoangukia pua tulipojaribu kuendelea kwa pamoja kupitia vijiji vya ujamaa na mashirika ya umma, je unashauri tujaribu tena? iwapo tulishindwa hata wakati aliyeanzisha hayo mawazo yupo sembuse sasa hayupo tena!!!!.

Kwa bahati mzuri nimeishi Asia kwenye nchi zinazoendelea, Europe kwenye nchi zilizoendelea na Afrika hasa TZ ambako tumesimama tu hatuendelei. Kwa mtazamo wangu nahisi tumejisogeza zaidi katika sera za kundi la walioendelea na ku-skip stage hii ya wa-Asia wanaoendelea. Bado kwangu mimi mtu mwenye hulka kama za EL, BWM na RA ndiyo wanafaa kuongoza.

Mara Nyingine nitaelezea jinsi mkuu wa mkoa wetu alivyobuni mbinu za kuiba pesa kutokana na mfumo wa uuzaji mazao, lakini akawa amesaidia kwa kiasi kikubwa sana kupandisha thamani na kuboresha masoko ya korosho.

Once again thank you for valuable contribution.
mkuu nimekusoma na pengine unachoshindwa kuelewa ni vipi tunazungumzia maswala mengu ya Kitaifa.

Kwanza budget ya serikali ni moja na ina cover area zote unazozungumzia hivyo maendeleo ya mkoa mmoja au jimbo yatategemea mipango iliyotoka serikali kuu.

Pili, sheria na taratibu za biashara ni za kitaifa, hivyo tunapozungumzia kilimo kwanza haina maana tunazungumzia ukulima wa mahindi na mananasi tu bali wigo pana zaidi la ukulima wa kisasa ikiwa ni pamoja na mazao ya kusini iwe korosho au tumbaku kutoka Bukoba..

Hivyo maendeleo ya ujumla kitaifa hayana maana ya Ujamaa, kwani ujamaa unaozungumziwa ni ule serikali inapohodhi njia zote za kiuchumi... Na sidhani kama ndilo tunalozungumzia hapa...

Tatu, yaonyesha wewe unapendekeza sana serikali za majimbo kama zinavyopendekezwa na Chadema lakini kabla hujafika hatua hiyo ni vizuri sana kuzitazama athari zake...kisha tumejiandaa vipi kukabiliana nazo..

Kwa mfano, nchi za wenzetu wenye kutumia mfumo huo wanajitosheleza ktk kila jimbo kiutawala kabla ya kuingia ktk jumuiya ya kitaifa yaani walikuwa nchi yenye utawaka wake mapema kabla ya kujiunga na majimbo mengine..
Chunguza sana utakuta kila jimbo lilikuwa nchi yenye kujitawala wakiwa na vitambulisho vya makazi tofauti na jimbo jingine, wana TIN number tofauti na hata namba plate za magari, yaani kila moja yao inajitegemea kiutawala ila wamekuja ungana kwa sababu maalum iwe ya kiusalama au kindugu kama tulivyoungana na Zanzibar..

Mimi naamini kabisa kwamba Tanzania hatuna uwezo wa kujite ganisha kimajimbo baada ya kuwepo Taifa tayari labda kwa kutumia yaliyopo na mtazamo finyu wa kimkoa.

Hatuna uwezo kifedha, kitaalam na tulijaribu wakati wa madaraka mikoani tukashindwa..

Kuunda majimbo ndani ya muungano ulokwisha kamilika kama chungwa linavojitegemea ingawa ndani yake limegawanyika vipande ndio maumbile ya Tanzania yetu, haikujengwa na Nyerere wala Ujamaa..

Hivyo, kuvamia mfumo kwa sababu wataalam wa uchumi wanasema hakuna maendeleo ya kitaifa ila kwa mmoja mmoja, naomba waulize mbona nchi inapofilisika huwa ni swala la kitaifa?

Ni majuzi tu tumesikia financial breakdown ya mataifa makubwa kiasi kwamba Obama akayasaidia mashirika ya magati ya Michigan, wananchi wa Texas au Georgia hawakusema haituhusu.. mabenki makubwa ya kimarekani yalikombolewa na hata yanayomilikiwa na watu kutoka nje kama Citi bank na kadhalika,leo tunatangaziwa hali nzuri kiuchumi imeanza kujitokeza kwa nchi nzima na sii sehemu moja au jimbo moja....

Hii yote ni kutuonyesha wazi kwamba utajiri wa mtu mmoja unaweza tu kuwa na manufaa kwa mwingine ikiwa haki na taratibu za misingi bora itafuatwa na wananchi wote..
Na inapotokea kundi la watu kutafuta utajiri huo kibinafsi basi malengo huwa sii kupata maendeleo ya jamii bali fahari ya utajiri.ambayo huathiri pia aendeleo ya nchi..

Sasa kina Mkapa na kundi la Mafisadi unalolisema kuwa ni wachapa kazi,ni wao ndio wamettufikisha hapa tulipo..na huwezi kusema afadhali ya wao ktk jitihada za kujiendeleza ikiwa ktk nguvu zao wamedhulumu au kudanganya ili wafanikiwe wao, hali kitendo hicho hicho ningekifanya Mkandara ningesota Segerea maisha..Mhalifu mara nyingi hutafuta utajiri kwa njia haramu na sii kutafuta maendeleo..

Kinachogomba hapa ni mamlaka tulowapa wanapoyatumia vibaya kwa faida zao binafsi, na sidhani kama unaona fahari kubwa kumsikia mtawala kama Mubarak kukamatwa na Mabillioni ya fedha hali wananchi wake wanasota..

Na ndiyo yanayoendeleana Nigeria na nchi za Afrika Magharibi kiasi kwamba utawala unapoondoka madarakani hutokea vita kubwa baada ya wananchi kugundua jinsi viongozi hao walivyojitajirisha na mwisho kuwaengua..

Kwa hiyo kuwachukia kina Mkapa,Lowassa na kina RA ni haki yetu sasa hivi mapema ili kuepuka hasira ya wale walionyonywa kufikia mahala wanalilia kuwatoa roho zao....

Leo hii CCM wanahofia maandamano ya Chadema lakini mimi ningewaomba wahofie zaidi wizi wao na ujenzi wa tabaka la walionacho kwani kila siku hao walalahoi huzidi kujenga hasira,machungu na chuki zaidi dhidi yao..siku ya siku itafika hakuna muamana na ndipo nchi itaingia pabaya zaidi..

Kuhusu utendaji kazi wa wahitimu wa vyuo vikuu na watu kama kina Lowassa,Mkapa na RA..kumbuka tu kwamba hawa kina Mkapa,Lowassa na RA walipomaliza shule walikuta ajira zao mezani tayari kuanza kazi tofauti na vijana wa keo ambao CV yao ndio kioo. Cha ajira zao.

Ha hao pia walipitia ngazi hizi hizi za wahitimu kupiga kelele kupinga hali ya maisha magumu wakati wa Nyerere na ndivyo inavyokuwa kwa kila hatua ya maisha ya mtawaliwa..

Sasa wao walipoacha kupiga kelele ni pale walipokoma kutawaliwa na kufanya kazi za kihalali wakawa wao ktk nafasi za kujineemesha..Utagundua kwamba lengo lao lilikuwa utajiri na sii maendeleo..

Na mkuu, hata siku moja huwezi kumsikia mwenye shibe akipiga miayo labda iwe ya uvivu..

Hawa woote wanaowalalamikia wahitimu wa vyuo vikuu ni kwa sababu wao wameshiba na hivyo hushangaa kilio cha mwenye njaa, wamekwisha sahau kwamba hata wao walikuwa hivyo kabla ya kupata madaraka.....

Na sii kweli kufanya kazi kwa nguvu ndio kufanikiwa bali kufanya kazi kwa akili na malengo ndio ufanishi wa kile ulichokusudia...Hatutafuti utajiri bali tunataka maendeleo...

Kama hawa wahitimu wanalalamika ili kuwaelimisha wananchi jinsi wanavyoibiwa na viongozi wao basi kipimo cha kelele zao kitakuwa baada ya kupima mwamko wa wananchi wenyewe ktk kudai haki zao...
Na bila shaka wamefanikiwa sana na ndio maana Mafisadi wanahaha sasa hivi na kuhamisha fedha zao nje wakijihusisha na madawa ya kulevya, money laundary na hata kupandisha bei ya dhahabu chafu kuwa ghali kuliko soko la dunia..

Na hakika kukua kwa demokrasia kudao sheria, haki na elimu ya uraia ni bora zaidi ya utajiri wa mali haramu...

Mwisho usiwaone hawa wasomi wetu hawafanyi kitu kwa kutumia mzani wa vibaba vya mchele kwani kwa kila neno lao moja huwatajirisha millioni 40 kifikra..Leo hii hakuna mtu asiyechukia Mafisadi...
 
Back
Top Bottom