Hatimaye kilio cha wadau wa demokrasia nchini kimesikika, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutangaza kuajiri watumishi wake wa kudumu kuanzia bajeti ijayo ya serikali ya mwaka 2012/2013, kwa ajili ya kusimamia uchaguzi na kuachana na utaratibu wa sasa wa kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri za nchini.
Kwa muda mrefu, wadau hao na baadhi ya wananchi wamekuwa wakipaza sauti zao wakitaka wakurugenzi waondolewe katika kusimamia chaguzi kwa madai kuwa hawatoi haki.
Hata hivyo, serikali imekuwa ikishikilia msimamo wake na kusema kwamba itaendelea kuwatumia kwa kuwa wao ni sehemu ya watumishi wake na kupuuza vilio vya wadau hao wakiwemo wanaharakati na wapinzani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, baada ya kufungwa mkutano wa siku mbili wa viongozi wa Tume za Uchaguzi za nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva, alisema hatua hiyo inalenga kuweka uwazi na kupanua demokrasia.
Hawa watumishi tutakaowaajiri katika kila wilaya na manispaa hapa nchini watakuwa na ofisi za kudumu na kufanya kazi ya kusimamia chaguzi mbalimbali bila kuingiliwa na mtu yeyote, alisema Jaji Lubuva.
Alisema kwa sasa unafanyika mchakato wa kuhakikisha Nec inapata watumishi hao kulingana na sifa watakazoziweka na kwamba baada ya kupata fedha katika bajeti ijayo itawaajiri
Source:Nipashe