Tumesikia kilio cha Wapinzani,wakurugenzi mwisho kusimamia Uchaguzi-Lubuva

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Hatimaye kilio cha wadau wa demokrasia nchini kimesikika, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutangaza kuajiri watumishi wake wa kudumu kuanzia bajeti ijayo ya serikali ya mwaka 2012/2013, kwa ajili ya kusimamia uchaguzi na kuachana na utaratibu wa sasa wa kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri za nchini.
Kwa muda mrefu, wadau hao na baadhi ya wananchi wamekuwa wakipaza sauti zao wakitaka wakurugenzi waondolewe katika kusimamia chaguzi kwa madai kuwa hawatoi haki.
Hata hivyo, serikali imekuwa ikishikilia msimamo wake na kusema kwamba itaendelea kuwatumia kwa kuwa wao ni sehemu ya watumishi wake na kupuuza vilio vya wadau hao wakiwemo wanaharakati na wapinzani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, baada ya kufungwa mkutano wa siku mbili wa viongozi wa Tume za Uchaguzi za nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva, alisema hatua hiyo inalenga kuweka uwazi na kupanua demokrasia.
“Hawa watumishi tutakaowaajiri katika kila wilaya na manispaa hapa nchini watakuwa na ofisi za kudumu na kufanya kazi ya kusimamia chaguzi mbalimbali bila kuingiliwa na mtu yeyote,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema kwa sasa unafanyika mchakato wa kuhakikisha Nec inapata watumishi hao kulingana na sifa watakazoziweka na kwamba baada ya kupata fedha katika bajeti ijayo itawaajiri

Source:Nipashe

Yaani huyu mzee kama anataka ajipatie ujiko, atekeleze hiki. Maana magambas wanakera sana, siku ya kuhesabu kura hawa jamaa huwa wanapokea maagizo kutoka juu! Shame on them!
 
Mwanzo mzuri kwa huyu mzee.Tumwombee asipitiwe na mapepo yakamvuruga akili yake
 
sasa kama tume inachakachuliwa itakuwa hawa wakurugenzi wa kudumu wa tume? BTW let's hope for the best
 
Oooh my!! Umenikonga moyo mwanaharakati mwenzangu kwa kauli murua na ya kipiganaji kama hiyo. Big up sana pia kwa Mhe Tundu Lissu na wabunge wote waliomuunga mkono kwa hoja hii kule bungeni.

Hakuna vita ya haki inayoshindwa!!
 
Kama itakuwa kweli kheri, lakini wasiwasi wangu wanaompa hiyo bajeti ni walewale wanaofaidika na mfumo huu uliopo.

Ngoja tumpe muda labda anaweza kuweka historia ya pekee katika hii NEC.
 
Hatimaye kilio cha wadau wa demokrasia nchini kimesikika, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutangaza kuajiri watumishi wake wa kudumu kuanzia bajeti ijayo ya serikali ya mwaka 2012/2013, kwa ajili ya kusimamia uchaguzi na kuachana na utaratibu wa sasa wa kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri za nchini.
Kwa muda mrefu, wadau hao na baadhi ya wananchi wamekuwa wakipaza sauti zao wakitaka wakurugenzi waondolewe katika kusimamia chaguzi kwa madai kuwa hawatoi haki.
Hata hivyo, serikali imekuwa ikishikilia msimamo wake na kusema kwamba itaendelea kuwatumia kwa kuwa wao ni sehemu ya watumishi wake na kupuuza vilio vya wadau hao wakiwemo wanaharakati na wapinzani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, baada ya kufungwa mkutano wa siku mbili wa viongozi wa Tume za Uchaguzi za nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva, alisema hatua hiyo inalenga kuweka uwazi na kupanua demokrasia.
"Hawa watumishi tutakaowaajiri katika kila wilaya na manispaa hapa nchini watakuwa na ofisi za kudumu na kufanya kazi ya kusimamia chaguzi mbalimbali bila kuingiliwa na mtu yeyote," alisema Jaji Lubuva.
Alisema kwa sasa unafanyika mchakato wa kuhakikisha Nec inapata watumishi hao kulingana na sifa watakazoziweka na kwamba baada ya kupata fedha katika bajeti ijayo itawaajiri

Source:Nipashe

Kuajiri wafanyakazi wapya haiwezi kuifanya Tume kuwa huru.Hoja ya msingi ni kuwa na Tume huru ya uchaguzi isiyofungamana na ofisi ya Rais ikiwa ni pamoja na nafasi yake yeye mwenyewe.Hiyo nafasi yake aliyopewa na Rais ni mbaya zaidi ya hao wakurungenzi.
 
Ni mapema sana kumkubali (appreciate) katika hilo, ngoja tumpe muda tuone kama litatekelezeka; likiwezekana kudos kwake. Nia yake hiyo isije ikachakachuliwa tu na hao waonao maboresho yoyote katika tume ya uchaguzi ni mwanzo wa kiama chao!
 
Nasubiri kuona hilo likitokea maana tumeona jinsi hawa wakurugenzi wanavyotishwa na hata kupata matatizo kazini kwa kufukuzwa ama kuhamishwa vituo pale wanaposimamia haki bila kukipendelea chama tawala.
Hongera Lubuva ila tunasubiri vitendo maana tumechoka na maneno matupu.
 
Siaminishwi na maneno matupu ya magamba. Luvuba ni gamba. Ameteuliwa kutetea haki za magamba. sidhani. Pia, CCM bado ni chama dola, kitaingilia mfumo wa uchaguzi tu mpaka hapo tutakapokuwa na Tume huru.
 
ni mapema sana kumsifu kwa hilo, hiyo ni mipango tuu, muda ukifika serikali ya sisiemu itasema haina hela
 
kuna wakurugenzi wengine hata majumbani kwao wanaenda na kuishi kwa woga kwasababu ya hili jukumu walilopewa la kukandamiza demokrasia kwa njia ya kupiga kura
 
CONTRADICTION!mbona upinzani majuzi umetaka wakurugenzi wasimamie mchakato wa maoni katiba mpya?
 
Back
Top Bottom