zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,835
Habari wana JF.
Imenibidi nirudishe kumbukumbu zangu tangu sasa hadi miaka 59 nyuma.
Na tarehe iliyo nijia kichwani ni tarehe 9.12.1961 ambayo machozi ya furaha yalibubujika na sauti za kusherekea kupatikana kwa uhuru zilisikika Tanzania nzima.
Kongole zimfikie muasisi wa taifa hili na kiongozi makini dhabiti aliyefanikisha mapambano yetu kuelekea Uhuru na si mwingine ni Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Lakini Mwalimu aliwahi kusema maadui wakubwa wa maendeleo ya Taifa la Tanzania ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.
Kwa sasa taifa lina miaka ya 59 toka tupate Uhuru
Je, unafikiri ni vitu gani au maendeleo gani tumeweza kuyafikia tangu miaka hiyo hadi sasa?
Je, tumeweza kupambana vilivyo na Maradhi, Ujinga na Umaskini?
Je, unaiona wapi Tanzania katika miaka ijayo?
Vijana na vizazi vijavyo vitamuenzi Mwalimu na kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa na uzalendo uliotukuka ?
Tukumbushe mambo unayoyafahamu kuhusu Uhuru wetu na jitihada za kuupata!
Tukumbushe mbio zetu tokea Uhuru hadi sasa.
Hizi ni baadhi ya nukuu za Mwalimu Nyerere.
"Kila Mtu anataka maendeleo lakini si kila mtu anaelewa na kukubali mahitaji muhimu kwa ajili ya maendeleo.Cha muhimu ni kufanya kazi kwa bidii"
"Kwa hali yeyote ile kutegemea kubaya kupita kote ni kutegemea mtu kwa mawazo yake kunakunyima uhuru wewe"
"Elimu siyo njia ya kuepuka umaskini bali ni njia ya kupigana na umaskini"
"Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"