Tumeshinda vita dhidi ya Ujinga, Maradhi na Umaskini miaka 59 tangu tupate Uhuru?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,563
2,000
Habari wana JF.

Imenibidi nirudishe kumbukumbu zangu tangu sasa hadi miaka 59 nyuma.

Na tarehe iliyo nijia kichwani ni tarehe 9.12.1961 ambayo machozi ya furaha yalibubujika na sauti za kusherekea kupatikana kwa uhuru zilisikika Tanzania nzima.

Kongole zimfikie muasisi wa taifa hili na kiongozi makini dhabiti aliyefanikisha mapambano yetu kuelekea Uhuru na si mwingine ni Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Lakini Mwalimu aliwahi kusema maadui wakubwa wa maendeleo ya Taifa la Tanzania ni Ujinga, Maradhi na Umasikini.

Kwa sasa taifa lina miaka ya 59 toka tupate Uhuru

Je, unafikiri ni vitu gani au maendeleo gani tumeweza kuyafikia tangu miaka hiyo hadi sasa?

Je, tumeweza kupambana vilivyo na Maradhi, Ujinga na Umaskini?

Je, unaiona wapi Tanzania katika miaka ijayo?

Vijana na vizazi vijavyo vitamuenzi Mwalimu na kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa na uzalendo uliotukuka ?

Tukumbushe mambo unayoyafahamu kuhusu Uhuru wetu na jitihada za kuupata!

Tukumbushe mbio zetu tokea Uhuru hadi sasa.

Hizi ni baadhi ya nukuu za Mwalimu Nyerere.
"Kila Mtu anataka maendeleo lakini si kila mtu anaelewa na kukubali mahitaji muhimu kwa ajili ya maendeleo.Cha muhimu ni kufanya kazi kwa bidii"

"Kwa hali yeyote ile kutegemea kubaya kupita kote ni kutegemea mtu kwa mawazo yake kunakunyima uhuru wewe"

"Elimu siyo njia ya kuepuka umaskini bali ni njia ya kupigana na umaskini"

"Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,391
2,000
Nchi gani haina magonjwa, maradhi na haina maskini. Wewe uko wapi
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,850
2,000
Inashangaza sana kuna vitu wakoloni wa kijerumani waliotawala 1880-1920 wakirudi leo hii watashangaa sana kuona vitu hivyo vipo vilevile walivyoviacha au vimeharibika zaidi mfano ni reli zetu. Miji yetu ilikuwa mizuri zaidi na yenye mipango madhubuti mwaka 1910 kuliko sasa. Kweli waafrika lazima tujifikirie tunashindwa wapi.
 
Ndekrepha

JF-Expert Member
Jun 4, 2020
1,502

Uko sawa!..... Uko sawa kabisaaa.
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
2,417
2,000
Sasa hivi yameongezeka maradhi mapya kwa vijana wanaita upungufu wa nguvu za kiume
 
Kashaulo

JF-Expert Member
Jun 14, 2019
2,771
2,000
59 Years Old!
Adjustments.jpg
 
Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
338
500
Inashangaza sana kuna vitu wakoloni wa kijerumani waliotawala 1880-1920 wakirudi leo hii watashangaa sana kuona vitu hivyo vipo vilevile walivyoviacha au vimeharibika zaidi mfano ni reli zetu. Miji yetu ilikuwa mizuri zaidi na yenye mipango madhubuti mwaka 1910 kuliko sasa. Kweli waafrika lazima tujifikirie tunashindwa wapi.
Acha unafiki! Toa mfano maana huo wa reli ni kama umejitoa fahamu.
 
mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,745
2,000
Nikwambie hatujawashinda adui zetu na wala hatuwezi kuwashinda kwasababu kubwa hizi
1.Wanaotuongoza wanawajua maadui kwa majina lakini si kwa sura hivyo kila tukienda vitani tunashindwa kuwaangamiza kwakuwa hatuwaoni
2.Tumewakaribisha maadui tukawafanya ndugu zetu kwa kuwaoa (tumefunga nao ndoa za kansani)
3.Tumechoka na tukodhaifu hatukotayari kwa vita

Ningetamani moja aelewe nilichoandika sema ndio hivyo nimeshindwa kupreasent kwa simple language
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,850
2,000
Acha unafiki! Toa mfano maana huo wa reli ni kama umejitoa fahamu.
Hapo hapo kwenye reli: Mwaka 1912 reli ya kaskazini kutoka Dar-Tanga-Moshi-Arusha ilikuwa inafanya kazi na ilikuwa bize na nzuri sana ikiwa na vituo vingi vya kupandia abiria na watu na mizigo mingi ilipita katika reli hii. Na reli hii iliunganiswa na Mombasa na Nairobi hivyo enzi hizo za kale zilizokuwa nzuri mtu alikuwa anasafiri kwa treni kutoka Dar hadi Nairobi kupitia Moshi. Leo hii hayo hayapo, ndio watu wanaanza kuchimbua reli iliyojichimbia ardhini na kilichofanyika ni hicho, zile stesheni na majengo yake hayafai yameoza wanaishi panya na nyoka. Tumerudi nyuma miaka 110, angerudi Karl Peters angeshangaa mpaka mwisho.
 
Nimekuambia reli inajengwa upya au huoni to a mfano wa kitu kingine.
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,192
2,000
Nchi gani haina magonjwa, maradhi na haina maskini. Wewe uko wapi
Nchi ambayo haina magonjwa na maradhi na maskini.. ni nchi iliyopo mbinguni tu.
Kama ni hapa hapa duniani hakuna nchi isiyo na hivyo vitu.
Hata ulaya wenye mifumo mziru ya afya na uchumi mzuri. Bado wagonjwa wapo na maskin wapo. Kinachotofautiana ni level ya wagonjwa na maskin.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,155
2,000
Nchi gani haina magonjwa, maradhi na haina maskini. Wewe uko wapi

Mbona kama umepaniki hivi!! Ukisoma hiyo mada kuanzia mwanzo mpaka mwisho, utagundua jambo muhimu sana! Mtoa mada hakutoa hitimisho.

Alichokifanya ni kuichokonoa tu mada yake huku akituwekea nukuu kadhaa za Baba wa Taifa. Tunachotakiwa ni kushindana sasa sisi kwa sisi, kwa hoja iwapo hao maadui watatu bado wapo au hawapo! takribani miaka 59 sasa tangu tulipopata Uhuru.

Binafsi naona hao maadaui watatu bado wametamalaki nchini mwetu! Hivyo kuna umuhimu wa kuiondoa/kuipumzisha CCM madarakani kwa nia njema kabisa, ili tu na wengine waje na mawazo na mtazamo mpya wa kuitoa nchi yetu kutoka hapa ilipo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom