Umeongea mambo ya msingi sana lakini chuki kubwa kwa watu wengi ni swala la magufuli kugusa watu wenye vyeti vyeki ukisikia kelele nyingi za watu huwa zinabebwa na wahanga wa hili kundi .ukisikia magufuli alikuwa katili ukichunguza ni mhanga wa kutumbuliwa kutoka cheti feki au mriji umekatwa kutoka sehem flani hiviHuwa nawatafakari sana Watanzania wa kizazi hiki wanaoimba kikwete alikuwa anapenda demokrasia. Najiuliza je Dr. Ulimboka au Mwangosi naye anasema hivyo hivyo Marehemu huyu?
Najiuliza waliouawa kwenye chaguzi ya Igunga nao wanasema hivyo hivyo au lile bomu lililolipuliwa kule Arusha kwenye Mkutano wa Chadema? Akina Alphonse Mawazo nao wanakubaliana na hoja hii?
Haya yalitokea katika Utawala wa kikwete. Kumwagiwa Tindi Kali na Kinusurika kuuawa Dr. Ulimboka baada ya kutupwa katika Msitu wa Mabwe pande.
Katika miaka kadhaa Tanzania haikuwahi kuwa salama. Isipokuwa Watanzania ni wanafiki kwa kiwango kikubwa. Kwani ni lini kauli za kuanza kusema Chadema itakufa zilianzishwa?
Kwani Dkt. Slaa na mkewe walipopigwa na kuvunjwa mkono Dr. Slaa ilikuwa lini? Mpaka Dr. Slaa kununuliwa kusaliti wapinzani ilikuwa Utawala upi?
Yaani tumesahau Richmond,Iptl,Tegeta Escrow na kashfa nyingi za kutisha? Madawa ya kulevya na ufisadi mkubwa na kisha Rais kuja sema wahusika wakikamatwa nchi itayumba akicheka mbele za umma wa watanzania?
Watanzania ni wanafiki kwa kiasi kikubwa sana. Ni watu wa kuogopwa sana. Kilichomfanya kikwete aonekane ni bora pia ni unafik wake wa kuweza kuuma na kupuliza.
Dkt. Magufuli hakuweza kupuliza. Aliuma na kuacha maumivu yaendelee kubak. Utawala wake ulikuwa ni ule ule wa Ubabe akilazimisha alichoamini kuwa ni maendeleo. Hakutaka kupingwa.
Jamani tumesahau Makonda alipewa zawadi ya Ukuu wa Wilaya baada ya kufanya kitendo gani cha kishujaa? Uhuni uliofanyika katika mchakato hewa wa Katiba na Mabilion ya pesa yaliyotumika?
Tunasahau kwa kuwa angalau wapinzania walikuwa wakipewa poshi kutulizwa n.k akina Zitto Kabwe na Mbowe mara kadhaa walipokuwa wakimbana sana kikwete alikuwa anaonana nao wanayamaliza.
Magufuli alikuwa hashirikiani nao katika misingi hiyo. Aligoma hata aliposhauriwa kuwa awe anaonana nao "kuwatoa kiaina" yeye aliwatenga kabisa. Hapa alikosea.
Leo hii ungewachukua akina Dr. Ulimboka, akina Mwangosi n.k ukawaambia Kikwete alikuwa mwanademokrasia wataangua kilio kikubwa. Aliyetuhumia kuhusika na hujuma ile ya Dr. Mwangosi alisemekana kuwa Ikulu. Hakushtakiwa akapewa zawadi ya Cheo.
Hili wanasiasa wengi hawazungumzi sababu Dr. Mwangosi hakuwa mwanasiasa. Kumbe angekuwa mwanasiasa angekuwa Tundu Lissu wa miaka ile. Tumesahau Madawa ya kulevya yalivyokuwa moja ya biashara kubwa nchini. Na vijana wetu wengi kuharibika mitaani wakiwemo wasanii.
Watanzania tutabadilisha nchi ikiwa tutaacha unafiki na kuamua kwa dhati kupambana na tawala zote dhalimu. Tupambane Katiba iweze tenga Nguvu kubwa wanayopewa marais juu ya kila sheria na kila mtu kufanya wapendavyo.
Tukiendelea na ubinafsi kuangalia watu kimaslahi, kidini na kikabila. Kila mwaka tutagawanyika kwa misingi hiyo na maadui watatutawala. Kama tutaendelea kusema moyoni huyu ni wa kwetu sisi. Nchi hii itasimama hapa huku wabunge wakitaka waongezewe mishahara bila woga kabisa.
Mimi nmeasi chama. Nmebaki na Utanzania wangu. Tumeona madhara ya kuwa na Katiba Mbovu sasa tuililie katiba mpya. Tunaweza jisahau kwa kulambishwa asali wakati tunaumwa Kansa na mguu unaoza. Tutapewa dawa ya usingizi tukija shtuka mwili wote umeoza kwa kansa.
Sent using Jamii Forums mobile app