Tumesahau alichofanywa Dkt. Ulimboka, Mwangosi na Said Kubenea. Nchi hii ni ya kinafiki sana

Huwa nawatafakari sana Watanzania wa kizazi hiki wanaoimba kikwete alikuwa anapenda demokrasia. Najiuliza je Dr. Ulimboka au Mwangosi naye anasema hivyo hivyo Marehemu huyu?

Najiuliza waliouawa kwenye chaguzi ya Igunga nao wanasema hivyo hivyo au lile bomu lililolipuliwa kule Arusha kwenye Mkutano wa Chadema? Akina Alphonse Mawazo nao wanakubaliana na hoja hii?

Haya yalitokea katika Utawala wa kikwete. Kumwagiwa Tindi Kali na Kinusurika kuuawa Dr. Ulimboka baada ya kutupwa katika Msitu wa Mabwe pande.

Katika miaka kadhaa Tanzania haikuwahi kuwa salama. Isipokuwa Watanzania ni wanafiki kwa kiwango kikubwa. Kwani ni lini kauli za kuanza kusema Chadema itakufa zilianzishwa?

Kwani Dkt. Slaa na mkewe walipopigwa na kuvunjwa mkono Dr. Slaa ilikuwa lini? Mpaka Dr. Slaa kununuliwa kusaliti wapinzani ilikuwa Utawala upi?

Yaani tumesahau Richmond,Iptl,Tegeta Escrow na kashfa nyingi za kutisha? Madawa ya kulevya na ufisadi mkubwa na kisha Rais kuja sema wahusika wakikamatwa nchi itayumba akicheka mbele za umma wa watanzania?

Watanzania ni wanafiki kwa kiasi kikubwa sana. Ni watu wa kuogopwa sana. Kilichomfanya kikwete aonekane ni bora pia ni unafik wake wa kuweza kuuma na kupuliza.

Dkt. Magufuli hakuweza kupuliza. Aliuma na kuacha maumivu yaendelee kubak. Utawala wake ulikuwa ni ule ule wa Ubabe akilazimisha alichoamini kuwa ni maendeleo. Hakutaka kupingwa.

Jamani tumesahau Makonda alipewa zawadi ya Ukuu wa Wilaya baada ya kufanya kitendo gani cha kishujaa? Uhuni uliofanyika katika mchakato hewa wa Katiba na Mabilion ya pesa yaliyotumika?

Tunasahau kwa kuwa angalau wapinzania walikuwa wakipewa poshi kutulizwa n.k akina Zitto Kabwe na Mbowe mara kadhaa walipokuwa wakimbana sana kikwete alikuwa anaonana nao wanayamaliza.

Magufuli alikuwa hashirikiani nao katika misingi hiyo. Aligoma hata aliposhauriwa kuwa awe anaonana nao "kuwatoa kiaina" yeye aliwatenga kabisa. Hapa alikosea.

Leo hii ungewachukua akina Dr. Ulimboka, akina Mwangosi n.k ukawaambia Kikwete alikuwa mwanademokrasia wataangua kilio kikubwa. Aliyetuhumia kuhusika na hujuma ile ya Dr. Mwangosi alisemekana kuwa Ikulu. Hakushtakiwa akapewa zawadi ya Cheo.

Hili wanasiasa wengi hawazungumzi sababu Dr. Mwangosi hakuwa mwanasiasa. Kumbe angekuwa mwanasiasa angekuwa Tundu Lissu wa miaka ile. Tumesahau Madawa ya kulevya yalivyokuwa moja ya biashara kubwa nchini. Na vijana wetu wengi kuharibika mitaani wakiwemo wasanii.

Watanzania tutabadilisha nchi ikiwa tutaacha unafiki na kuamua kwa dhati kupambana na tawala zote dhalimu. Tupambane Katiba iweze tenga Nguvu kubwa wanayopewa marais juu ya kila sheria na kila mtu kufanya wapendavyo.

Tukiendelea na ubinafsi kuangalia watu kimaslahi, kidini na kikabila. Kila mwaka tutagawanyika kwa misingi hiyo na maadui watatutawala. Kama tutaendelea kusema moyoni huyu ni wa kwetu sisi. Nchi hii itasimama hapa huku wabunge wakitaka waongezewe mishahara bila woga kabisa.

Mimi nmeasi chama. Nmebaki na Utanzania wangu. Tumeona madhara ya kuwa na Katiba Mbovu sasa tuililie katiba mpya. Tunaweza jisahau kwa kulambishwa asali wakati tunaumwa Kansa na mguu unaoza. Tutapewa dawa ya usingizi tukija shtuka mwili wote umeoza kwa kansa.
Umeongea mambo ya msingi sana lakini chuki kubwa kwa watu wengi ni swala la magufuli kugusa watu wenye vyeti vyeki ukisikia kelele nyingi za watu huwa zinabebwa na wahanga wa hili kundi .ukisikia magufuli alikuwa katili ukichunguza ni mhanga wa kutumbuliwa kutoka cheti feki au mriji umekatwa kutoka sehem flani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwangosi aliuawa na askari kwa sababu ya mob psychology tu ya maaskari, huwezi kumtuma askari akaue mtu kwa bomu la machozi.

Ulimboka huyo alipewa kibano kidogo tu cha kumshikisha adabu maana alikuwa anaendesha migomo isiyokoma ya madaktari ya kuparalyse huduma za Afya kwa wananchi, kwanza alipaswa ashitakiwe kwa kusababisha vifo vya watu wengi sana sababu ya kuendesha migomo kinyume cha taaluma ya utabibu

Sasa tuambie hawa wafuatao
Maiti za kwenye viroba
Ben Saananei yuko wapi
Simon Kanguye yuko wapi
Kamanda mawazo vipi?
Aliyempiga risasi tundu Lisu
Aliyemteka Roma mkatoliki
Aliyemteka Mo
Achilia mbali waliokufa kwa presha sababu ya uporaji wa pesa zao
Au waliokufa kwa mshtuko wa moyo kwa kuvunjiwa nyumba zao
Au waliokufa kwa msongo wa mawazo kwa kuporwa korosho zao
chuki kubwa kwa watu wengi ni swala la magufuli kugusa watu wenye vyeti vyeki ukisikia kelele nyingi za watu huwa zinabebwa na wahanga wa hili kundi .ukisikia magufuli alikuwa katili ukichunguza ni mhanga wa kutumbuliwa kutoka cheti feki au mriji umekatwa kutoka sehem flani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wengine humu jf kipindi cha uongozi wa kikwete walikuwa hawajazaliwa...utakuta li-mtu linakomaa kwamba kipindi cha mwendazake tuliokota maiti kwenye viroba,kama vile hayo mambo hayakuwepo kabla ktk nchii hii
Umeongea mambo ya msingi sana lakini chuki kubwa kwa watu wengi ni swala la magufuli kugusa watu wenye vyeti vyeki ukisikia kelele nyingi za watu huwa zinabebwa na wahanga wa hili kundi .ukisikia magufuli alikuwa katili ukichunguza ni mhanga wa kutumbuliwa kutoka cheti feki au mriji umekatwa kutoka sehem flani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna watu wamekaa na kutufanya kama hatuna akili, mambo ya watu kutekwa, kuuawa na kuteswa yalianza awamu ya nne kwa hiyo wasijifanye kutuambia heri ya fulani sisi ndio tunajua nani mzuri nani mbaya
Umeongea mambo ya msingi sana lakini chuki kubwa kwa watu wengi ni swala la magufuli kugusa watu wenye vyeti vyeki ukisikia kelele nyingi za watu huwa zinabebwa na wahanga wa hili kundi .ukisikia magufuli alikuwa katili ukichunguza ni mhanga wa kutumbuliwa kutoka cheti feki au mriji umekatwa kutoka sehem flani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JK hakuwa msafi 100% lakini alikuwa na ubinadamu sn, dikteta yeye ni risasi mwanzo mwisho.
Acha ujinga! Dr mvungi wa katiba mpya aliuawa wakati wa kikwete na mabomu kule arusha wananchi waliuawa! Kwa hiyo huyo Lisu kageuka kuwa Luku ni binadamu sana kuliko wengine?
 
Mwangosi aliuawa na askari kwa sababu ya mob psychology tu ya maaskari, huwezi kumtuma askari akaue mtu kwa bomu la machozi.

Ulimboka huyo alipewa kibano kidogo tu cha kumshikisha adabu maana alikuwa anaendesha migomo isiyokoma ya madaktari ya kuparalyse huduma za Afya kwa wananchi, kwanza alipaswa ashitakiwe kwa kusababisha vifo vya watu wengi sana sababu ya kuendesha migomo kinyume cha taaluma ya utabibu

Sasa tuambie hawa wafuatao
Maiti za kwenye viroba
Ben Saananei yuko wapi
Simon Kanguye yuko wapi
Kamanda mawazo vipi?
Aliyempiga risasi tundu Lisu
Aliyemteka Roma mkatoliki
Aliyemteka Mo
Achilia mbali waliokufa kwa presha sababu ya uporaji wa pesa zao
Au waliokufa kwa mshtuko wa moyo kwa kuvunjiwa nyumba zao
Au waliokufa kwa msongo wa mawazo kwa kuporwa korosho zao
Hivi ung'olewe meno kwa koleo na kucha, kupigwa na kubanwa na bisibisi unasema kilikuwa kibano kidogo? Mtu kupigwa hadi kuzirai wakajua kafa na kumtupa mabwepande wewe unasema aliguswa guswa. Hivi uliona hali yake wakati anapelekwa kutibiwa Afrika kusini.

Mwangosi hivi uliona picha za mwandishi huyu? Alianguka chini akaonesha kasarenda kwa kuinua mikono juu. Lakini askari akiwa amemrenga tumboni na kulipua bomu la machozi tumboni mwa Mwangosi. Picha zilionesha utumbo umesambaa. Hakuwa Mwangosi tena. Mwili ulisambaratika. Mauaji ya kikatiri. Wewe unakuja hapa kuhalalisha kifo kuona hakuna shida na kulinganisha na hayo usemayo. Watu wengine ni rafiki na ndugu. Inauma. Acha ushabiki.

Mabomu ya Arusha watu walipoteza ndugu na rafiki wa karibu, wewe unaona sawa.
Hivyo kama unahalalisha vifo vya Arusha, Igunga, Morogoro, na Mwangosi basi kihistoria
Tanzania hii watu kukutwa wamekufa na kutiwa katika viroba yamekuwa yanatokea na hasa kwa watu waishio ufukweni uona mengi. Nikiwa mdogo niliyaona sana hayo, na nikauliza kwa nini. Nilielezwa.

Nakumbuka Diwani mmoja alipigwa risasi na kuondoa maisha yake enzi za nyuma. Hata Rais wa Zanzibar Karume aliuwawa kwa pigwa risasi. Watu wametekwa na hata kupotea miaka na miaka. Leo tunataka sema mabaya Tanzania yalitokea tu wakati wa awami ya tano.
Huu ni unafiki roho ya wivu na kutojielewa kwa baadhi ya watanzania.
Katibu Mkuu wa CCM kifo chake kilikuwaje? Kolimba. Waziri Mkuu Sokoinne kifo chake kilikuwaje? Unakumbuka Nyerere aliongea nini?
So hakuna kifo halali na kisicho halali? Dhuruma ni dhuruma tu.
 
Dah! Baada ya kung'olewa meno, Dr. Ulimboka alikimbiwa na wenzake wote maskini akabaki mwenyewe huku dola ikifanya yake!

Huku akina JK wanachekelea...

Hii sawa na siku alipouawa Gaddafi akina Obama na H. Clinton walikunywa mvinyo wa hatari kutoka Israel.
 
Umeongea mambo ya msingi sana lakini chuki kubwa kwa watu wengi ni swala la magufuli kugusa watu wenye vyeti vyeki ukisikia kelele nyingi za watu huwa zinabebwa na wahanga wa hili kundi .ukisikia magufuli alikuwa katili ukichunguza ni mhanga wa kutumbuliwa kutoka cheti feki au mriji umekatwa kutoka sehem flani hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
Na vipi waliotekwa,kupigwa,kufilisiwa,na hata kuuawa?Unawaweka kundi gani.?
Pia Kuna viongozi wa upinzani na wafuasi wao wamepewa kesi za ajabu ajabu.
Usisahau maiti za kwenye viroba zilizokuwa zinaokotwa baharini na mitoni.
Vile bado zinaokotwa?
 
Back
Top Bottom