Nchi hii inaupendeleo sana

NANCA

Member
Jun 23, 2023
92
100
Leo nlikua maeneo ya kawe beach nkafika maeneo ya kikwete ambapo zamani kabla yake palikua na mfereji/mto mkuuubwa unaotiririsha maji yake bahari ya hindi. Mfereji huo ulikua ukikua,kutanuka na komong'onyoa sehemu ya ardhi ya makazi hayo lkn leo hii baada ya mheshimiwa kujengewa hapo basi mfereji huo umejengewa vizuri kupitisha maji ili mheshimiwa awe salama.

Wakati kwa mheshimiwa pakijengewa vyema bado mifereji/mito mingine ya watu wengine inazidi kula viwanja vyao na nyumba zao ata kulazimika kurundika mawe ili kupambana na hyo hali.

Wakati mheshimiwa akijengewa vizuuri ili mtu huo usimle, masikini wa kule msimbazi na jangwani wanaambiwa waondoke sbb mazingira hayo ni hatarishi. Nadhani ktk mabonde hayo Kama kungekua na mheshimiwa fulani basi masikini wale wangepona, mabonde yangejengewa.

Wakati mheshimiwa anarindwa na mmong'onyoko wa mtu huo Kuna masikini Kama mimi naibiwa uwanja wangu na halmashauri au na mbunge kwa kuitumia halmashauri afu kila napokwenda si skizwi, nina hasira sana.

Wakati mheshimiwa anaekewa mazingira safi Kuna watanzania wanatakiwa kutoka ngorongoro ili waheshimiwa na watalii wakapate mazingira safi ya uwindaji na utalii.

Kiufupi ukifungua kifua changu na ukapasua moyo wngu utakutana na risasi ya dhahabu ya ukombozi dhidi ya dhuruma na kutoskizwa tuvyofanyiwa ss watu wadogo. Siku Mungu ikisaidia basi tujipange kuishi sawa. Huwenda haya nayopitia sasa ni jiko, niko jikoni Mungu ananipika ili kupambana na udharimu, uonevu, ukandamizaji na kujipendelea kwa waheshimiwa akiwemo huyu mbunge mwizi na mlaghai wa viwanja vya watu.

Mwisho niseme kua shida yangu sio kikwete na familia yake kujengewa mfereji au kupata chochote kile, shida yangu ni kwann kila kitu na usalama wote wa mali zao na wavitakavyo viende kwao? Mbona ssi wanatufanya Kama mapunda kuwapambania wao? Je mheshimiwa fulani angekua anamiliki jangwani,msimbazi,ngorongoro mngemtoa au mngeeka tu mazingira vizuri? Je pale kwangu ndo pangekua kwa mheshimiwa fulani mngemsumbua au mngetumiwa na mbunge ili kupapata? Kimsingi nina hasira, ktk nchi hii the law of impartiality haizingatiw Kuna upendeleo mkubwa sana. Ujumbe huu umfikie ndugu mama prof mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambani anapambana kuifanya haki kua anapatikana automatically bila kujua anaofanya nao kazi ni ma ndumi la kuwili. Pia ujumbe huu umfikie mkuu wa mkoa mwenye yule mbunge std IV mwizi wa viwanja vya watu.
HUU NDO UJUMBE WANGU WA KUFUNGIA MWAKA.
 
Back
Top Bottom