Tumesahau alichofanywa Dkt. Ulimboka, Mwangosi na Said Kubenea. Nchi hii ni ya kinafiki sana

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,982
Huwa nawatafakari sana Watanzania wa kizazi hiki wanaoimba kikwete alikuwa anapenda demokrasia. Najiuliza je Dr. Ulimboka au Mwangosi naye anasema hivyo hivyo Marehemu huyu?

Najiuliza waliouawa kwenye chaguzi ya Igunga nao wanasema hivyo hivyo au lile bomu lililolipuliwa kule Arusha kwenye Mkutano wa Chadema? Akina Alphonse Mawazo nao wanakubaliana na hoja hii?

Haya yalitokea katika Utawala wa kikwete. Kumwagiwa Tindi Kali na Kinusurika kuuawa Dr. Ulimboka baada ya kutupwa katika Msitu wa Mabwe pande.

Katika miaka kadhaa Tanzania haikuwahi kuwa salama. Isipokuwa Watanzania ni wanafiki kwa kiwango kikubwa. Kwani ni lini kauli za kuanza kusema Chadema itakufa zilianzishwa?

Kwani Dkt. Slaa na mkewe walipopigwa na kuvunjwa mkono Dr. Slaa ilikuwa lini? Mpaka Dr. Slaa kununuliwa kusaliti wapinzani ilikuwa Utawala upi?

Yaani tumesahau Richmond,Iptl,Tegeta Escrow na kashfa nyingi za kutisha? Madawa ya kulevya na ufisadi mkubwa na kisha Rais kuja sema wahusika wakikamatwa nchi itayumba akicheka mbele za umma wa watanzania?

Watanzania ni wanafiki kwa kiasi kikubwa sana. Ni watu wa kuogopwa sana. Kilichomfanya kikwete aonekane ni bora pia ni unafik wake wa kuweza kuuma na kupuliza.

Dkt. Magufuli hakuweza kupuliza. Aliuma na kuacha maumivu yaendelee kubak. Utawala wake ulikuwa ni ule ule wa Ubabe akilazimisha alichoamini kuwa ni maendeleo. Hakutaka kupingwa.

Jamani tumesahau Makonda alipewa zawadi ya Ukuu wa Wilaya baada ya kufanya kitendo gani cha kishujaa? Uhuni uliofanyika katika mchakato hewa wa Katiba na Mabilion ya pesa yaliyotumika?

Tunasahau kwa kuwa angalau wapinzania walikuwa wakipewa poshi kutulizwa n.k akina Zitto Kabwe na Mbowe mara kadhaa walipokuwa wakimbana sana kikwete alikuwa anaonana nao wanayamaliza.

Magufuli alikuwa hashirikiani nao katika misingi hiyo. Aligoma hata aliposhauriwa kuwa awe anaonana nao "kuwatoa kiaina" yeye aliwatenga kabisa. Hapa alikosea.

Leo hii ungewachukua akina Dr. Ulimboka, akina Mwangosi n.k ukawaambia Kikwete alikuwa mwanademokrasia wataangua kilio kikubwa. Aliyetuhumia kuhusika na hujuma ile ya Dr. Mwangosi alisemekana kuwa Ikulu. Hakushtakiwa akapewa zawadi ya Cheo.

Hili wanasiasa wengi hawazungumzi sababu Dr. Mwangosi hakuwa mwanasiasa. Kumbe angekuwa mwanasiasa angekuwa Tundu Lissu wa miaka ile. Tumesahau Madawa ya kulevya yalivyokuwa moja ya biashara kubwa nchini. Na vijana wetu wengi kuharibika mitaani wakiwemo wasanii.

Watanzania tutabadilisha nchi ikiwa tutaacha unafiki na kuamua kwa dhati kupambana na tawala zote dhalimu. Tupambane Katiba iweze tenga Nguvu kubwa wanayopewa marais juu ya kila sheria na kila mtu kufanya wapendavyo.

Tukiendelea na ubinafsi kuangalia watu kimaslahi, kidini na kikabila. Kila mwaka tutagawanyika kwa misingi hiyo na maadui watatutawala. Kama tutaendelea kusema moyoni huyu ni wa kwetu sisi. Nchi hii itasimama hapa huku wabunge wakitaka waongezewe mishahara bila woga kabisa.

Mimi nmeasi chama. Nmebaki na Utanzania wangu. Tumeona madhara ya kuwa na Katiba Mbovu sasa tuililie katiba mpya. Tunaweza jisahau kwa kulambishwa asali wakati tunaumwa Kansa na mguu unaoza. Tutapewa dawa ya usingizi tukija shtuka mwili wote umeoza kwa kansa.
 
Hata mimi nashangaa jinsi watu wanavyomzungumzia huyo Magufuli unaweza kudhani Tanzania ilikuwa sehemu salama kabisa hakukuwa na matukio ya ajabu ajabu huko nyuma kabla ya Magufuli, tatizo la Magufuli hakujua kupuliza alikuwa kiburi na aliwafanya wale waliyokuwa wanajiona wako salama kutojihisi salama tena.
 
Tatizo la Dr. Ulimboka baada ya shambilio la kutaka kumuua alikaa kimyaa hadi leo watanzania hawajui yupo wapi na anafanya nini. - Wengine wanasema ati alishikishwa kitu kidogo kama pole ili afumbe mdomo na kutafutiwa kazi nje ya nchi.
 
Tatizo la Dr. Ulimboka baada ya shambilio la kutaka kumuua alikaa kimyaa hadi leo watanzania hawajui yupo wapi na anafanya nini. - Wengine wanasema ati alishikishwa kitu kidogo kama pole ili afumbe mdogo na kutafutiwa kazi nje ya nchi.
Kwahiyo hiyo inahararisha kitendo alichotendewa?
 
Watanzania tutabadilisha nchi ikiwa tutaacha unafiki na kuamua kwa dhati kupambana na tawala zote dhalimu. Tupambane Katiba iweze tenga Nguvu kubwa wanayopewa marais juu ya kila sheria na kila mtu kufanya wapen
Umeongea jambo la msingi sana hapa chief
 
Hata mimi nashangaa jinsi watu wanavyomzungumzia huyo Magufuli unaweza kudhani Tanzania ilikuwa sehemu salama kabisa hakukuwa na matukio ya ajabu ajabu huko nyuma kabla ya Magufuli, tatizo la Magufuli hakujua kupuliza alikuwa kiburi na aliwafanya wale waliyokuwa wanajiona wako salama kutojihisi salama tena.
Huu ndo ukweli ambao wengi hawataki kukubaliana nao.
 
Watanzania si
Tatizo la Dr. Ulimboka baada ya shambilio la kutaka kumuua alikaa kimyaa hadi leo watanzania hawajui yupo wapi na anafanya nini. - Wengine wanasema ati alishikishwa kitu kidogo kama pole ili afumbe mdogo na kutafutiwa kazi nje ya nchi.

Watanzania sio wa kuwaamini..mwishoni aliachwa peke yake na ndugu zake.maisha yake yakawa yameharibika. Akaambiwa achague kupewa pesa anyamaze au aendelee na harakati safari hii hatopona. Ungechagua nini na watanzania wenyewe sisi wanafik.
 
Mwangosi aliuawa na askari kwa sababu ya mob psychology tu ya maaskari, huwezi kumtuma askari akaue mtu kwa bomu la machozi.

Ulimboka huyo alipewa kibano kidogo tu cha kumshikisha adabu maana alikuwa anaendesha migomo isiyokoma ya madaktari ya kuparalyse huduma za Afya kwa wananchi, kwanza alipaswa ashitakiwe kwa kusababisha vifo vya watu wengi sana sababu ya kuendesha migomo kinyume cha taaluma ya utabibu

Sasa tuambie hawa wafuatao
Maiti za kwenye viroba
Ben Saananei yuko wapi
Simon Kanguye yuko wapi
Kamanda mawazo vipi?
Aliyempiga risasi tundu Lisu
Aliyemteka Roma mkatoliki
Aliyemteka Mo
Achilia mbali waliokufa kwa presha sababu ya uporaji wa pesa zao
Au waliokufa kwa mshtuko wa moyo kwa kuvunjiwa nyumba zao
Au waliokufa kwa msongo wa mawazo kwa kuporwa korosho zao
 
Mwangosi yuko wapi

Hatari,yajayo yanafurahisha.
 
Back
Top Bottom