WomanOfSubstance
Platinum Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 972
Napata taabu kusema kama tumeridhika au tumekata tamaa kwa sababu sina hakika kama tunajitambua na tunajua tunalolitaka.
Shida yangu ni kuwa wale ambao angalau tuko tunapiga mswaki hatujaribu kamwe kuwastua wenzetu. Tunawaongezea blanketi na shuka waendelee kuuchapa usingizi. Kama tungewanyang'anya wakaguswa na baridi kidogo hiyo picha wa wakazi wa Bonde la Mpunga ingekuwa tofauti!
Mungu atuipushie mbali na balaa llnaloweza kutokea.
Hivi tumerogwa?
Mchawi wetu ni Ujinga wetu ambao tumerisishwa tuko dhamani,watanzania ni watu wapole wataratibu na majasiriMchawi wetu atakuwa nani?
Na vipaumbele umeviangalia? Meya wa Ilala amezindua kampeni maalumu ya usafi wiki iliyopita...je Meya wa Kinondoni ana ajenda hii? Je nani anapaswa kuwajibika kwa hicho tunachokiona kwenye picha? ni manispaa, wakazi wa eneo husika? wapita njia au nani?
\Wapeni CHADEMA Manispaa kama hizi. Mabadiliko yataonekana tu. Nimeona wamefanya kazi nzuri sana TARIME.
Na ninaamini kuwa ukienda kuangalia kwenye master plan ya jiji la dar, Bonde la Mpunga halijawa indicated kama eneo la makazi
Mkazi wa Msasani Bonde la Mpunga akipita katika matofali kukwepa maji machafu yatiririka kutoka katika makazi ya watu.(Picha kwa hisani ya Mroki)
My Take:
Picha hii ukiangalia kwa haraka ni kama picha ya kawaida tu ya hali halisi ya maisha ya watu wetu. Lakini ukianza kuiangalia kwa vipande na kuweka focus ya kitu au theme moja moja utaona kuwa inabeba ujumbe mzito kweli.
a. Nyumba
b. Maji machafu
c. Mtu
d. Makazi
e. Umeme
f. Takataka
Kitu kimoja hata hivyo nilicho na mang'amuzi nayo ni kuwa usione mazingira hayo kwa nje, hizo nyumba kwa ndani zina umeme, TV n.k na wakazi wake wanatembea na viselula huku wakitinga pamba za nguvu kila siku wakienda kujobu au kuchakarika. Wakazi wake usishangae kuwaona kwenye matamasha mbalimbali wakiwa wanaburudika na moja moto moja baridi.
Hii picha ina ujumbe mzito sana.
Hapana bana! hiyo picha siyo Tanzania na wala sio Afrika! Hatuko wala hatuishi hivyo sisi....
\
Hakuna lolote uko wewe...nani kasema...washaanza kulalamika mtu waliye changua...sasa hawezi hata kupanga hoja bungeni,ana kigugumizi....
Bora diwani angekuwa ndio mbunge....ni nini kuwa na hoja harafu ukashidwa kuziwakilisha katika mpangilio...?wangine watasema...ni ugeni..mbona wengine kama zito walipo ingia walianza upiganaji day one....kweli hamna pale...pengo halijazibika.
DC, Hebu fafanua zaidi.
Kwa hili suala la usafi/uchafu - kujali/kutokujali nadhani tuna matatizo .Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu kuanzisha kampeni ( kama mtu binafsi) ya kusafisha mazingira ya eneo ninaloishi mimi -hivyo vikwazo unavyokumbana navyo usiombe!Lakini tulipelekeshana tu vizuri.
Katika maeneo mengi ya makazi kuna mchanganyiko wa watu wenye fikra tofauti - wapo wenye kujali na kufanya mazingira yao yawe safi - halafu wapo wale wasiojali kabisa na hawa ni wagumu sana kushughulika nao maana wanachojali wao ni mradi kumekucha.Na usipoangalia utaishia kutukanwa mpaka ushangae.Je usafi ni class issue?
Narudi tena kwa wenzetu wapanga miji. Miji/jiji letu lilivyopangwa inashangaza kidogo- kuna mchanganyiko maalum. Utakuta mixture of high,low.medium density plots.jE, NINI mantiki ya huu mchanganyiko? haieleweki kama eneo ni slam au ni affluent surbarb na ujengaji wa nyumba nao unashangaza pia.Tazama maeneo kama Mikocheni,Msasani na hata Mbezi Beach utaona hiyo hali.Inakuwa vigumu sana kuweka madhari nzuri kwa maana huo mchanganyiko wenyewe ni kero.Sijui tufanye nini.