Tumeridhika (Picha)! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeridhika (Picha)!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 4, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mkazi wa Msasani Bonde la Mpunga akipita katika matofali kukwepa maji machafu yatiririka kutoka katika makazi ya watu.(Picha kwa hisani ya Mroki)

  My Take:
  Picha hii ukiangalia kwa haraka ni kama picha ya kawaida tu ya hali halisi ya maisha ya watu wetu. Lakini ukianza kuiangalia kwa vipande na kuweka focus ya kitu au theme moja moja utaona kuwa inabeba ujumbe mzito kweli.

  a. Nyumba
  b. Maji machafu
  c. Mtu
  d. Makazi
  e. Umeme
  f. Takataka

  Kitu kimoja hata hivyo nilicho na mang'amuzi nayo ni kuwa usione mazingira hayo kwa nje, hizo nyumba kwa ndani zina umeme, TV n.k na wakazi wake wanatembea na viselula huku wakitinga pamba za nguvu kila siku wakienda kujobu au kuchakarika. Wakazi wake usishangae kuwaona kwenye matamasha mbalimbali wakiwa wanaburudika na moja moto moja baridi.

  Hii picha ina ujumbe mzito sana.
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Na watoto wao wanaenda shule vilevile....zile za HakiElimu
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na humo wanazaliwa "MAFISADI" watarajiwa wengi tu. Vinginevyo hakuna namna kuondokana na hali hii.
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na wewe unapenda MAFISADI. Na wengi wametokea huku. Wengine walitokea kwenye nyumba walizochangia na ng'ombe lakini sasa hawawezi tena kuishi humu.
  Nani anatakiwa aishi humu zaidi ya mtoto wa mlala hoi
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania?
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na haya ni "afadhali" kidogo. Vijijini hali ni mbaya zaidi kuanzia chakula, hakuna vitanda wala magodoro, hakuna maji, hakuna vyoo,....
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Najaribu kufikiria kama kweli wakazi au wamiliki wa nyumba hizi kweli wameridhika au wamekata tamaa. Yawezekana kabisa mtu anayeamka asubuhi kutokea katika moja ya nyumba hizo akawa ni mtu mwenye mawazo mabaya interms of kwanini wao na sio sisi???

  Kwa hiyo hata mafisadi wanaozaliwa katika nyumba hizo wanapopata nafasi ya kukamata kamfereji ka ufisadi huwa wananyonya mpaka wanakausha kwani wanaamini ndio njia ya kulipiza na kujifariji.....Nadhani mvua za masika zinapofika hiyo sehemu sijui inakuwa katika hali gani jamani.....Lazima tujiangalie tena kuna tatizo mahali fulani katika utendaji kama sio akili za viranja wetu!!!
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hulka ya uchafu imetawala fikra za wengi ikiwa ni pamoja na wale wenye dhamana ya kusimamia taratibu na kanuni za usafi wa mazingira. Labda iundwe Tume kuchunguza HALAFU ITOE MAPENDEKEZO NINI KIFANYIKE!..Lol!
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Eneo hili limo ndani ya Manispaa TAJIRI kabisa hapa Nchini, KINONDONI. Meya wake, Mstahiki Londa, ni mmoja wa matajiri wazawa wa Dar kwa sasa?
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Na vipaumbele umeviangalia? Meya wa Ilala amezindua kampeni maalumu ya usafi wiki iliyopita...je Meya wa Kinondoni ana ajenda hii? Je nani anapaswa kuwajibika kwa hicho tunachokiona kwenye picha? ni manispaa, wakazi wa eneo husika? wapita njia au nani?
   
 11. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maeneo mengine yalitakiwa yasiwe makazi ya wananchi. Bonge la Mpunga ni mfano halisi kabisa.

  Je, lawama zingine zitupiwe kwa wale vijana wetu tuliowasomesha chuo cha ardhi? Mipango miji ni aje nyinyi?
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wapeni CHADEMA Manispaa kama hizi. Mabadiliko yataonekana tu. Nimeona wamefanya kazi nzuri sana TARIME.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na ninaamini kuwa ukienda kuangalia kwenye master plan ya jiji la dar, Bonde la Mpunga halijawa indicated kama eneo la makazi
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Hapo umegusia tatizo lingine....
  vijislams vinajitokeza polepole kila mahali na viongozi wanaangalia na hawasemi kitu.Hivi wahusika wa mipango miji kama mpo humu JF hebu tupeni ufafanuzi ni kwanini hamfanyi kazi yenu kwa makini?As professionals, mnajiskiaje mnapoona jiji/miji mnayopaswa kusimamia inazidi kuharibika siku hadi siku? Na je, hamuoni historia itakuja kuwahukumu maana " landmarks" mnazoacha zitabaki kwenye kumbukumbu? Jirekebisheni jamani!Tusikalie kuwasema viongozi wa kisiasa tu humu JF tujiseme hata sisi wenye taaluma na dhamana.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuna matatizo katika ngazi zote.

  Watawala ni vipofu na kama wanaona hawana shida ya kushughulikia hayo matatizo kwa sababu hayawagusi.

  Ila wakazi wa pale nao wana matatizo tena makubwa kuliko watawala. Walitakiwa kuwambia watawala wao kile wanachokitaka. Kama hawawasikilizi wanawatimua kazi. Najua mawazo hayo hawana na ndio maana hutashangaa kukuta nyumba hizo zimejaa mabango ya wagombea wakati wa uchaguzi hata kama wagombea hao wanawalaghai. Pia kutakuwa na bendera nyingi tu za chama kilichoshindwa kuwathamini na pia wao nadhani bado wanazo t-shirts ana khanga. Utawasaidiaje watu hao??
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kazi gani unataka wafanye? Kazi kubwa sana wameshafanya. Kwani hujasikia maboss wao wanawasifia?

  Profession gani unaongelea? Kuna pesa pale? Kama hakuna pesa mtu aende kufanya nini??

  Umewauliza wanataka kuacha legacy gani?? Mimi najua legacy zetu kama WaTz wa kizazi hiki ni kuacha "pesa nyingi sana" (bila kujali umezipataje), nyumba ndogo za kutosha, watoto kibao wasiojuana (walau mmoja kila mtaa) na misifa kibao (angalau uwe umerushwa walau mara moja kwenye bongo flava). Sasa hiyo historia unayoongelea siyo yetu!

  Lakini mwisho wa yote, sisi waathirika tunajua kuwa tunaathiriwa na mazingira yetu ambayo ni matokeo ya matendo ya watawala? Mpaka hapo tutakapojua ndio tunaweza kuanza kuongea! Vinginevyo tuache tuendelee kuuchapa usingizi!!
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii ndio 'ari mpya kasi mpya'watu tunazidi kutaabika sana tu.
  Angalia kwa sasa mtu ukitoka nyumbani unakuja kazini kuanzia kodi ya meza nyumbani+usafiri+chai+msosi mchana+nauli kurudi nyumbani=si chini ya 10,000 mshahara kwa mwezi kwa mhindi haizidi 100,000/= sijui wa serikalini mnapeta vipi.
  Ukiwa fisadi hapo unamfisadi mhindi akikaa vibaya unamkwapilia utakuwa unamwonea????
  Hii ndio hali halisi ya maisha ya MTZ hali mbaya sana asikwambia mtu.
  Hapo sijapiga kodi kwa mwezi pamoja na umeme wa kuchangia kila baada ya wiki 2 5000 yaani inauma sana.Ukirudi kijijini ndo balaa zaidi ya huku mjini.
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  I like this!
  mambo ya mshiko siyo? Mshiko jamani unatufikisha pabaya!Hakuna tena kujali maslahi ya taifa wala kujali historia itakuja kuhukumu vipi! Ina maana ndiyo tumeridhika au tumekata tamaa?
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Napata taabu kusema kama tumeridhika au tumekata tamaa kwa sababu sina hakika kama tunajitambua na tunajua tunalolitaka. Mpaka hapo tutakapoweza kujua sisi tu akina nani, tunataka nini, tunataka kwenda wapi na kwa nini ndiyo tunaweza kufikia hizo hitimisho ulozitaja hapo juu. Nadhani bado tunauchapa usingizi.

  Shida yangu ni kuwa wale ambao angalau tuko tunapiga mswaki hatujaribu kamwe kuwastua wenzetu. Tunawaongezea blanketi na shuka waendelee kuuchapa usingizi. Kama tungewanyang'anya wakaguswa na baridi kidogo hiyo picha wa wakazi wa Bonde la Mpunga ingekuwa tofauti!
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kamanda naona unawatukana watu hapa...
   
Loading...