Tumepoteza almasi muhimu, Ndugu Lukuvi

Tumepoteza almasi muhimu, Ndugu Lukuvi

Huyu Mzee sikuwahi kumkubali kote alikopita, lakini kwenye ardhi, ameitendea haki ipasavyo ile nafasi.
Naamini hata kama ameenguliwa kwa majungu au kupishana na wakubwa, kazi kubwa aliyoifanya itampa faraja huko aendapo.

Ametatua matatizo mengi sana na kuiweka sawa wizara, upatikanaji wa hati, urasimishaji ardhi n.k pia hakua muongeaji sana kwenye media zaidi ya kazi zake kuonekana.

Nikatika kipindi chake tumeona watu wakipata hati bila gharama kuzidi 1M kwa viwanja vya kawaida kulingana na ukubwa kitu ambacho awali ulikua unaliwa pesa nyingi na bado hati hauipati.

Sijajua kama u spika utamfaa ila ingekua ni maoni yangu, asingetolewa ardhi akakamilisha kazi nzuri aliyoianzisha.

Namuombea kila la kheri popote atakapokua.
Katika nafasi ya uspika, mkuu nakubaliana na wewe Lukuvi ni mtu sahihi kabisa badala ya Ayubu.
 
No man is infallible, all men are falible Binadamu hatukosi kasoro. Lukuvi alikuwa mzuri kwenye ardhi. Kama naye Ni kundi la Sukuma, Basi Ni kumuita na kumuweka sawa . Alikuwa mtendaji mzuri.
Pole Bw Lukuvi.
2025 mpeni fomu ya urais!
 
Aanze mbele mdini huyo
Watu wa hivyo hata wafanye kazi nzuri kiasi gani ila kama ni mbaguzi unamsifia nini ?

Alisema eti wale ni wabaya sana na tukiwaacha hivyo waarabu watakuja kututawala seriously Will,

Halafu baada ya mda akaenda kule kule Oman kuomba akiwa kavaa Kanzu kinafiki yeye na Makinda akiwa kavaa baibui

Hafai hafai
 
Alisimamia mambo ya ardhi bila woga, mara nyingi alimuomba Mungu amsaidie kwani ni kazi ngumu na mafisadi kibao.
 
Mpe pole Samia, Lukuvi yeye alitimiza majukumu yake, labda amekusudia awe spika.
Naamini ni Spika ajae kutokana na weledi na uandamizi wake bungeni anatosha kwa nafasi ya Uspika CCM inabidi wamwangalie yeye anauzoefu na Bunge toka la upinzani kapambana sana kwa hoja na Mnadhimu wa kipindi hicho Tundu Lissu
 
Kwa kweli huyu mzee alijitahidi japo porojo mwanzo alikuwa nazo vitendo hafifu.

Leo nilibahatika kupita Kurasini nikitokea kigamboni. Roho yangu iliumia sana jinsi Kurasini Club kule Nyumba za TPA kulivyokuwa na hali niliyoina leo. Kwa kweli serikali kama hili la wamachinga inatakiwa wizara ya ardhi na makazi ipitishe greda kwa watu wote waliojenga kuzidi mipaka yao na mawe ya awali.

Kurasini imekuwa haina barabara vibanda vya biashara vimejaa kila kona kila mtu kajenga fremu chips,duka,baa, stationary. Huu si uchumi ni ujinga kuharibu makazi kisa vijibanda vinavyozidi biwanja na nyumba.

Hili ndugu Lukuvi amelishindwa kabisa. Maeneo yote serikali ivunje wale walioziba njia, wameziba mitaa na hili lifanyike Nationwide mbona Zimbabwe wanaweza hata Sinza kama kila mtu akifuata mawe ya kiwanja hakuna vibanda umiza vitabaki na ndio inavyotakiwa hasa tunakoenda kwenye hali ya joto zaidi.

Zamani Magomeni au Kinondoni kulikuwa na njia kati ya nyumba na nyumba lakini siku hizi ni sweatshops zimejaa. Hili lazima tukabiliane nalo hata kama lina uchungu.
 
No man is infallible, all men are falible Binadamu hatukosi kasoro. Lukuvi alikuwa mzuri kwenye ardhi. Kama naye Ni kundi la Sukuma, Basi Ni kumuita na kumuweka sawa . Alikuwa mtendaji mzuri.
Pole Bw Lukuvi.
Mbaguzi wa dini rejea clip yake akiwa kanisani huko kwao Isimani ili trend sana.
 
No man is infallible, all men are falible Binadamu hatukosi kasoro. Lukuvi alikuwa mzuri kwenye ardhi. Kama naye Ni kundi la Sukuma, Basi Ni kumuita na kumuweka sawa . Alikuwa mtendaji mzuri.
Pole Bw Lukuvi.
Mwache ajipange na 2025, au hutaki awe rais....
 
No man is infallible, all men are falible Binadamu hatukosi kasoro. Lukuvi alikuwa mzuri kwenye ardhi. Kama naye Ni kundi la Sukuma, Basi Ni kumuita na kumuweka sawa . Alikuwa mtendaji mzuri.
Pole Bw Lukuvi.
Hebu waacheni wale keki ya Taifa na watoto na wajukuu zao huyo unayemtaja alikuwa upande wa wananchi sio wao
 
Kwa kweli huyu mzee alijitahidi japo porojo mwanzo alikuwa nazo vitendo hafifu.

Leo nilibahatika kupita Kurasini nikitokea kigamboni. Roho yangu iliumia sana jinsi Kurasini Club kule Nyumba za TPA kulivyokuwa na hali niliyoina leo. Kwa kweli serikali kama hili la wamachinga inatakiwa wizara ya ardhi na makazi ipitishe greda kwa watu wote waliojenga kuzidi mipaka yao na mawe ya awali.

Kurasini imekuwa haina barabara vibanda vya biashara vimejaa kila kona kila mtu kajenga fremu chips,duka,baa, stationary. Huu si uchumi ni ujinga kuharibu makazi kisa vijibanda vinavyozidi biwanja na nyumba.

Hili ndugu Lukuvi amelishindwa kabisa. Maeneo yote serikali ivunje wale walioziba njia, wameziba mitaa na hili lifanyike Nationwide mbona Zimbabwe wanaweza hata Sinza kama kila mtu akifuata mawe ya kiwanja hakuna vibanda umiza vitabaki na ndio inavyotakiwa hasa tunakoenda kwenye hali ya joto zaidi.

Zamani Magomeni au Kinondoni kulikuwa na njia kati ya nyumba na nyumba lakini siku hizi ni sweatshops zimejaa. Hili lazima tukabiliane nalo hata kama lina uchungu.
Huyu wa sasa atayaweza hayo?
 
No man is infallible, all men are falible Binadamu hatukosi kasoro. Lukuvi alikuwa mzuri kwenye ardhi. Kama naye Ni kundi la Sukuma, Basi Ni kumuita na kumuweka sawa . Alikuwa mtendaji mzuri.
Pole Bw Lukuvi.
Hebu pia tutafakari kauli hizi:

1: Magufuli," wewe Lukuvi siwezi kukupendekeza uwe Rais una zaidi ya miaka 60"

2: Samia,"wale waotaka kujiandaa na 2025, nitawapa nafasi hiyo ili wakajiandae vizuri"
 
Hapo kwenye ardhi amechemka , mabula hawezi kuvaa viatu vya Lukuvi
 
Hakuna atakayeweza Si mabula wa Riz1. Na naona Mama Mabula atakaa kwa kutulia zaidi ukizingatia yeye ni mtu toka lakezone.
 
Back
Top Bottom