Tumepigiwa simu, mwisho wa fedha za wahisani waja

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
428
Mwaka 2003 wakati Rais wa Rwanda Paul Kagame akihojiwa na Jarida la News of the World kuhusu Misaada ya kifedha inayotolewa kwa bara la Afrika na kama imeweza kumaliza ufukara na hata kuyahamisha mataifa ya Afrika kutoka kuwa na wananchi wanaoishi chini ya dora moja kwa siku hadi kuwa wa kipato cha kati alijibu bila kutafuna maneno kwamba MISAADA haina tija kwa Afrika.

Kwa kauli yake Kagame alisema kuwa "Kwa miaka zaidi ya 60 Afrika imepokea zaidi ya Dola za Marekani Trilioni 1 lakini hakuna kitu cha maana cha kuonesha katika kupiga hatua kimaendeleo.Ufukara umekuwa ndiyo kielelezo cha nchi karibu zote za Afrika"

Kauli hiyo ya Kagame ambayo kwa mara kadhaa imekuwa ikirudiwa na wanazuoni wengi ambao wamekuwa wakipinga kwa nguvu zote misaada ya kifedha (Nieleweke Development aids) inayomiminika barani Afrika inapata nguvu zaidi kutokana na ukweli mwingine wa kitafiti kwamba zaidi ya Asilimia 45 ya fedha za wahisani ambazo zimekuwa zikimiminika barani Afrika na kwa maana hiyo Tanzania zimekuwa zikiishia mikononi mwa mafisadi na vigogo serikalini. Na kiasi cha zaidi ya asilimia 20 kimekuwa kikitumika katika malengo yasiyokusudiwa (yaani misused aids).Ni asilimia 30-35 ya kiasi cha fedha ndicho kimekuwa kikitumika kwa maendeleo ya Afrika.

Kwa mfano; mwaka 2005, Mwanadiplomasia wa Uingereza Sir Edward Clay aliwatuhumu wazi mawaziri wa Kenya na baadhi ya watendaji kwamba wamekuwa wakitafuna bila huruma fedha za misaada. Aliwafananisha kama mbwa anayekula na kuvimbewa na kutapika miguuni mwa bwana wake. Yaani utafunaji wa fedha za wahisani umepitiliza kiwango kiasi kwamba viongozi wa Afrika wamevimbiwa na sasa wanatapika miguuni mwa wahisani. This is Crazy.

Hivi karibuni Ofisi ya Waziri Mkuu Uganda imetuhumiwa kutafuna zaidi ya Paundi Milioni 61 kutoka Uingereza.Habari hizi za fedha za wahisani kutafunwa kama nilivyoeleza hapo juu ni nyingi na kwa sasa imefikia hatua zaidi ya asilimia 40 ya fedha hizo zinakwenda kwenye makoti ya mafisadi katika Serikali za Afrika.

Swali ninalojiuliza kama fedha za wahisani zinatafunwa kiasi hicho (Cha asilimia 40) na kwa kweli hakuna maendeleo ya wazi ya kujivunia ikilinganishwa na kiasi cha fedha kilichomwagwa Afrika, kwa nini Wahisani wanaendelea kumwaga mabilioni yao Afrika? Wanalenga kutajirisha na kujaza matumbo ya mafisadi na viongozi wezi? Kwa faida gani hasa?

Wanabodi kwa maneno mengine nimejaribu kupima fedha za wahisani, ufisadi unaozighubika na impacts yake katika mataifa ya Afrika ikiwemo Tanzania yetu nimeona hakuna haja ya kuendelea kutembeza bakuli. Hatuhitaji fedha za wahisani kwa sababu zinashibisha na kulevya watawala.

Sasa hawabuni tena vyanzo vya mapato, hawakusanyi kodi, wanaruhusu rasilimali kutoroshwa kama wehu vile, hawafikirii kuja na sera za kuwakomboa Waafrika. Kwa ujumla wamevimbewa fedha za wahisani na wako tayari kwenda kutapika fedha hizo kwenye mahoteli, makasino na mabenki ya Ulaya na America.

Najiuliza tu, kama niko ndotoni hivi siku ikitokea Wahisani (Gen.Ulimwengu anawaita Wajomba) wakatupigia simu na kutueleza 'Kuanzia leo Fedha hazitoki tena' tutafanyaje? Ni kweli Waafrika na kwa maana hiyo Watanzania tutakufa? Tutakufa kwa sababu ipi? Ni nani anaguswa moja kwa moja na fedha hizi zinazomwagwa kila mwaka kutoka kwa Wahisani? Tumeshawahi kweli kuwanza maisha nje ya wahisani? Nauliza tena; ni kweli Maisha nje ya Wahisani tutakufa? Kwa nini tufe? Tujadili jamani.

NB: Naunga mkono sera ya Majimbo na decentralization process (bila kujali nani anaihubiri) ili kuhakikisha rasilimali zinasimamiwa na kutajirisha kikamilifu maeneo zinakopatikana. Na kwa kuwa kila jimbo lina baraka za kipekee sioni sababu ya kutounga mkono hata kwa utaratibu wa Subsidizations kwa majimbo yatakayo kuwa nyuma.
 

Eng Kimox Kimokole

JF-Expert Member
Jun 9, 2010
1,031
754
......NB: Naunga mkono sera ya Majimbo na decentralization process (bila kujali nani anaihubiri) ili kuhakikisha rasilimali zinasimamiwa na kutajirisha kikamilifu maeneo zinakopatikana. Na kwa kuwa kila jimbo lina baraka za kipekee sioni sababu ya kutounga mkono hata kwa utaratibu wa Subsidizations kwa majimbo yatakayo kuwa nyuma.

Koooote huko mbwembwe tu hapo niipoquote ndipo paliponifurahisha
 

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
549
182
Wajomba wapige simu eti "kuanzia leo fedha hazitoki tena"? hah! hiyo sahau kabisa... hapo ndo kwenye ulaji wao hawawezi kusitisha, wala usizugike na maneno ya yeyote ya wazungu eti fedha zinaliwa na viongozi walafi... wao watoaji ndio walaji wakubwa! viongozi wetu ni ujinga na ubinafsi kukubali misaada/mikopo ya masharti ambayo inafavour watoaji kwa njia kadhaa huku wao wakiambulia kiduchu wananchi wakibeba zigo kubwa la madeni na kuibiwa rasilimali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom