Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,601
- 9,787
Chanzo: www.ippmedia.comMkuu wa kituo cha polisi mbaroni kwa ujambazi
2007-10-26 09:29:16
Na Renatus Masuguliko, PST Chato
Polisi Mkoani Kagera inamshikilia Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Bwanga, Wilayani Chato kwa tuhuma za kushiriki katika tukio la ujambazi wa kutumia silaha lililotokea wilayani humo hivi karibuni.
Wakati hilo likiendelea, watu wanaoaminika kuwa majambazi yameteka nyara mabasi matatu na kufanikiwa kuondoka na mali chache huku basi moja likipinduka katika harakati za kuyakimbia majambazi hayo.
Katika tukio la mkuu wa kituo kukamatwa, imeelezwa kuwa kunafutia wanananchi wilayani hapa wakiwemo?baadhi ya abiria?kumtambua kwamba alikuwa miongoni mwa watu wanaodaiwa kuwa majambazi katika eneo la tukio.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera, Bw. Abdallah Msika alithibitisha kwa njia ya simu jana kushikiliwa kwa mkuu huyo wa kituo na kumtaja kwa jina la Koplo Rajabu.
Hata hivyo, hakutaja ni lini alikamatwa kwa mahojiano lakini alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi.
`Kwa kuzingatia utaratibu wa jeshi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakiwemo waliokumbwa na tukio la uvamizi wa kutumia silaha lililotokea katika kijiji cha Mkungo Kata ya Busaka, wakidai kumtambua kuwepo kwenye tukio tulimkamata na tunaendelea kumhoji toka wiki iliyopita,` alisema Kamanda Msika.
`Tunataka kujua ukweli, kwani katika moja ya matukio yanayodaiwa kuwa alishiriki, sisi tunajua kuwa hakuwepo katika eneo hilo bali alikuwa wilayani Ngara kwenye operesheni maalum, lakini bado tunajiuliza kwa vipi wananchi wamtaje?` aliongeza.
Alisema kinachofanyika sasa ni kuwashirikisha wananchhi waliotoa taarifa hizo na uongozi wa polisi wilayani Ngara alikokuwa kwenye shughuli maalum kufahamu kwa kina ilikuwaje akahusishwa na kuonekana eneo la tukio.
`Kwa sasa ni mapema mno kusema kwa kina kuhusiana na tukio la kukamatwa kwake lakini nitatoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya uchunguzi kukamilka... Nisingependa kumhusisha moja kwa moja kuwa amekamatwa kwa kushiriki ujambazi,` alisisitiza Kamanda Msika.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka wilayani humo, mkuu huyo wa kituo anatuhumiwa kuhusika kushirikiana na majambazi walioteka magari kadhaa katika kijiji cha Mkungo likiwemo gari la hospitali.
Habari hizo zilidai kuwa kiongozi? huyo na baadhi ya watu waliokuwa wakisafiri na moja ya gari lililotekwa na majambazi hao, yaliyokuwa na silaha, walimfahamu bayana mkuu huyo na walilazimika kuwajulisa baadhi ya viongozi katika maeneo jirani.
Ilidaiwa kuwa wananchi hao walikusanyika huku wakiwa wameshatoa taarifa katika kituo cha polisi cha Buselesele na Chato ambapo walifanikiwa kuweka mawe barabarani ili kuyazuia magari yasipite.
Wakati wakiwa katika harakati hizo, gari lililokuwa likitumiwa na majambazi hao akiwemo mkuu huyo wa polisi, lilifika na mkuu huyo kuteremka haraka na kuwaambia wananchi hao kuwa lile gari lilikuwa la walinda amani hivyo waliruhusu lipite.
Wananchi hao waliliruhusu baada ya amri hiyo, lakini baada ya muda mfupi kupita? gari la polisi lilifika katika eneo hilo likilifukuza gari hilo la majambazi na walipoambiwa kuwa limekwishapita, polisi walilazimika kuwafuatilia bila mafanikio.
Wananchi hao walidai kuwa? walilaghaiwa na ofisa huyo wa polisi baada ya kudanganya kuwa gari hilo llilikuwa na watu wema na kuliruhusu kupita hatua iliyosababisha watoe taarifa kwa mara ya pili kwa mamlaka husika na hatua kuanza kuchukuliwa.
Sasa kama mpaka Mkuu wa kituo anashiriki ujambazi, sie wananchi tusiojua hata moja kuhusu matumizi ya silaha tutajilindaje?