Huenda ikawa taifa limepata msiba mwingine mkubwa baada ya ndege ya Precion Air kupata ajali ziwa Victoria ikikaribia kutua Bukoba airport
Ndege hii ni ileile ya jana iloyopata hitilafu ya engine kuzimika na kutua kwa dharura Kilimanjaro airport
Kabla ya ajali hii kuna mwanajamii Forum kwa jina la
maharage ya ukweni alitabiri kutokea kwa ajali ya ndege! Pengine kwa mataifa yanayozingatia mambo ya kiroho hili lingetosha kuwa kwenye alert! Lakini hili si mukatadha wa mada hii
Kuna mambo yanafikirisha sana kwenye hii ajali..! Kuna mambo sio kipaumbele kwetu hasa matukio ya dharura
Tutawapoteza watanzania wenzetu kwa kukosa vifaa sahihi na muhimu kwenye uokoaji
Hapakuwa na helikopta yoyote ya kutoa msaada kwenye uokoaji..
Hapakuwa na hata tag boat ya kuivuta ndege nchi kavu! Imevutwa kwa kamba na watu
Tuna bajeti nono kwa ajili ya Ma V8 ya viongozi lakini si kwenye dharura na uokozi.. Unapoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma haya ndio madhara yake
Sililaumu sana jeshi la zimamoto na uokoaji, kuna wakati likiwa limeona sasa kuwepo na umuhimu mkubwa wa kuwa na vifaa vya uokoaji zikiwepo drone za uokoaji watoa maamuzi waliishia kutumbuliwa na mwanakwenda! Kama tatizo lilikuwa mkataba wa kifisadi si ungetafutwa mwingine bora lakini si kuacha kabida kuagiza vifaa hivyo muhimu sana
Tuna majengo marefu sana kwasasa hapa nchini na madaraka makubwa lakini sina hakika kama kitengo chetu cha zimamoto na uokoaji kina uwezo wa kuyahudumia pindi litakapotokea janga
Maisha ya wananchi wengi yanaangaamia kwa kuipa siasa thamani kubwa kuliko weledi.. Kuna wale watoto wa Mtwara walipata ajali na gari ya shule! Huwezi kuamini walibwebwa na magari ya wagonjwa mpaka dar wakati ingetumika helicopter wangegikishwa kwa haraka Muhimbili na wangesaidika kwa haraka
View attachment 2408447View attachment 2408448