Tumejiandaaje na majanga ya dharura?

Tumejiandaaje na majanga ya dharura?

Kwa eneo ilipo tugboat isingefanya kazi.
Tugboat hutumia kusukuma au kuvuta, isingeweza vuta kwenda nchi kazi sababu ya kina kifupi

Hii ndege ukifuatilia flight history haijaenda sehemu tofauti na Mwanza, BK, Dsm kwa hizi siku 3
Asante sana kwa elimu na ufafanuzi
 
Asante sana kwa elimu na ufafanuzi
Yote kwa yote serikali yetu yapaswa laumiwa, sababu wako reactive badala ya active.
Kiwanja cha Mwanza, Bukoba, Musoma viko karibu sana na Ziwa Victoria.

Hivyo viwanja vinahitaji speed boat kubwa ziwepo muda wote,
Bandari za karibu zatakiwa ziwe na tug boats

Hata kwenye hii ndege kilichowaumiza hawakuwa na cable ndefu za kuvuta., Cable zingeliwepo hata fire zingejiunga zingeweza sogeza ndege karibu
 
Fikiria serikali wanaweza kutumia Helicopter kuzindua matokeo ya Sensa lakini serikali hiyohiyo ikashindwa kutumia Helicopter kuokoa watu. Yani wanaweza kutumia Helicopter kwenye mambo yasiyo ya muhimu halafu kwenye mambo muhimu kama hili la ajali ya ndege Bukoba wakashindwa.
Ukweli Inasikitisha Sana, Ukitazama Eti Ndege Inavutwa Kwa Kamba
Tangu Asubuhi Mpaka Muda Taarifa Zinasema Hakuna Matumaini Ya Haraka
Hatari Sana Tanzania, Sensa Chopper Imeruka Haraka!!
 
Kuna Jamaa alibashiri hii ajali itatokea humu JF, watu wakamchukulia poa tu

Acheni kukuza ujinga hip ndege yake ya ndoto Wala haifanani na precision air
 
Huenda ikawa taifa limepata msiba mwingine mkubwa baada ya ndege ya Precion Air kupata ajali ziwa Victoria ikikaribia kutua Bukoba airport
Ndege hii ni ileile ya jana iloyopata hitilafu ya engine kuzimika na kutua kwa dharura Kilimanjaro airport

Kabla ya ajali hii kuna mwanajamii Forum kwa jina la maharage ya ukweni alitabiri kutokea kwa ajali ya ndege! Pengine kwa mataifa yanayozingatia mambo ya kiroho hili lingetosha kuwa kwenye alert! Lakini hili si mukatadha wa mada hii

Kuna mambo yanafikirisha sana kwenye hii ajali..! Kuna mambo sio kipaumbele kwetu hasa matukio ya dharura
Tutawapoteza watanzania wenzetu kwa kukosa vifaa sahihi na muhimu kwenye uokoaji
Hapakuwa na helikopta yoyote ya kutoa msaada kwenye uokoaji..
Hapakuwa na hata tag boat ya kuivuta ndege nchi kavu! Imevutwa kwa kamba na watu
Tuna bajeti nono kwa ajili ya Ma V8 ya viongozi lakini si kwenye dharura na uokozi.. Unapoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma haya ndio madhara yake

Sililaumu sana jeshi la zimamoto na uokoaji, kuna wakati likiwa limeona sasa kuwepo na umuhimu mkubwa wa kuwa na vifaa vya uokoaji zikiwepo drone za uokoaji watoa maamuzi waliishia kutumbuliwa na mwanakwenda! Kama tatizo lilikuwa mkataba wa kifisadi si ungetafutwa mwingine bora lakini si kuacha kabida kuagiza vifaa hivyo muhimu sana

Tuna majengo marefu sana kwasasa hapa nchini na madaraka makubwa lakini sina hakika kama kitengo chetu cha zimamoto na uokoaji kina uwezo wa kuyahudumia pindi litakapotokea janga

Maisha ya wananchi wengi yanaangaamia kwa kuipa siasa thamani kubwa kuliko weledi.. Kuna wale watoto wa Mtwara walipata ajali na gari ya shule! Huwezi kuamini walibwebwa na magari ya wagonjwa mpaka dar wakati ingetumika helicopter wangegikishwa kwa haraka Muhimbili na wangesaidika kwa haraka

View attachment 2408447View attachment 2408448
Siasa kila sehem
images.jpg
 
Mara zote wanaofika wa kwanza kwenye eneo la tukio sio viongozi, sio wanasiasa, sio watu maarufu na sio matajiri bali ni wananchi wa kawaida kabisa wanajitolea bila kuwa na agenda yoyote

Hawa na mitumbwi yao wako tayari kusaidia lakini hawana vitendea kazi
IMG-20221106-WA0098.jpg
IMG-20221106-WA0106.jpg
 
Back
Top Bottom