Tumejiandaaje na majanga ya dharura?

Tumejiandaaje na majanga ya dharura?

Mi naomba kuuliza huwa na sikia kuna jeshi la angani, nchi kavu na jeshi la majini, swali hili jeshi la majini ndo hili linalookoa kwa kuvuta kamba!
 
Huenda ikawa taifa limepata msiba mwingine mkubwa baada ya ndege ya Precion Air kupata ajali Ziwa Victoria ikikaribia kutua Bukoba Airport.

Ndege hii ni ileile ya jana iliyopata hitilafu ya engine kuzimika na kutua kwa dharura Kilimanjaro Airport.

Kabla ya ajali hii kuna mwanajamii Forums kwa jina la maharage ya ukweni alitabiri kutokea kwa ajali ya ndege! Pengine kwa mataifa yanayozingatia mambo ya kiroho hili lingetosha kuwa kwenye alert! Lakini hili si mukatadha wa mada hii.

Kuna mambo yanafikirisha sana kwenye hii ajali..! Kuna mambo sio kipaumbele kwetu hasa matukio ya dharura.

Tutawapoteza watanzania wenzetu kwa kukosa vifaa sahihi na muhimu kwenye uokoaji. Hapakuwa na helikopta yoyote ya kutoa msaada kwenye uokoaji.

Hapakuwa na hata tag boat ya kuivuta ndege nchi kavu! Imevutwa kwa kamba na watu.

Tuna bajeti nono kwa ajili ya Ma V8 ya viongozi lakini si kwenye dharura na uokozi.. Unapoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma haya ndio madhara yake.

Sililaumu sana jeshi la zimamoto na uokoaji, kuna wakati likiwa limeona sasa kuwepo na umuhimu mkubwa wa kuwa na vifaa vya uokoaji zikiwepo drone za uokoaji watoa maamuzi waliishia kutumbuliwa na mwanakwenda! Kama tatizo lilikuwa mkataba wa kifisadi si ungetafutwa mwingine bora lakini si kuacha kabisa kuagiza vifaa hivyo muhimu sana.

Tuna majengo marefu sana kwa sasa hapa nchini na madaraka makubwa lakini sina hakika kama kitengo chetu cha Zimamoto na uokoaji kina uwezo wa kuyahudumia pindi litakapotokea majanga.

Maisha ya wananchi wengi yanaangaamia kwa kuipa siasa thamani kubwa kuliko weledi.

Kuna wale watoto wa Mtwara walipata ajali na gari ya shule! Huwezi kuamini walibwebwa na magari ya wagonjwa mpaka dar wakati ingetumika helicopter wangefikishwa kwa haraka Muhimbili na wangesaidiwa kwa haraka.

View attachment 2408447View attachment 2408448

Ile bendera ya Tanzania ule mstari mweusi wa katikati ndio unaotesa watu katika ulimwengu wa roho jaribu kufatilia .. hiyo nchi ya Tanzania haitakuja kutoboa ng'o mpaka bendera yake itakabadilishwa rangi zake..
 
Ile bendera ya Tanzania ule mstari mweusi wa katikati ndio unaotesa watu katika ulimwengu wa roho jaribu kufatilia .. hiyo nchi ya Tanzania haitakuja kutoboa ng'o mpaka bendera yake itakabadilishwa rangi zake..
Kuna ukweli kwenye hilo [emoji2827]
 
Baada ya kuona kimya rubani akapiga tena simu Tower na kuwaambia nipeni muongozo maana mafuta yataisha nimezunguuka sana, Tower wakamjibu ipeleke ziwani timu ya uokozi haitachelewa kuja kuwaokoa.
JamiiForums1161114180.jpg
 
Back
Top Bottom