Mkuu wa Majeshi anakujwa tembelea kituo na kukifungua rasmi "AFRICOM"!
Mkuu wa Majeshi anakujwa tembelea kituo na kukifungua rasmi "AFRICOM"!
Una maanisha Joji Bushi!?
Hapa naona mna wasiwasi usio na msingi. Kuna ubaya gani kupewa mafunzo ya kijeshi na Marekani? Jeshi letu lazima lifundishwe namna ya kutumia technolojia mpya za kivita. Kama sio Marekani basi nani afanye hiyo kazi?
Mnanikumbusha wakomunisti wa zamani ambao walidhani kila kinachohusu Marekani ni kibaya. They have been consigned to the dustbin of History, and the US thrives.
Ingekuwa vema sana kama Marekani ingeweka makao makuu ya Africa Command yao Tanzania. Ingetusaidia kwa namna nyingi mno. Ingekuza utalii na mawasiliano ya aina mbali mbali, na hata kungeweza kuweko direct flights kati ya New York na Dar.
Hamjasema kwa nini mnaogopa Marekani. Si maadui wetu. Wanaweza kuwa mapatna wazuri sana.
Labda unaweza usimpende Bush, lakini kwa nini usiwapende Wamarekani? Ni watu tu kama Waingereza, Wajerumani n.k., ambao tuna uhusiano mzuri nao. Au umekuwa kama Wairani ambao wanasema Waamerika ni mashetani?
Watanzania wanaipenda Marekani, ndio maana wengi wangetaka kwenda kuishi huko, na baadhi wamefanya hivyo. Hata hivyo, lazima tuangalie maslahi ya taifa letu, kama vile Wamarekani wanavyoangalia maslahi ya taifa lao daima. Iwapo tutawekeana mkataba wa ushirikiano, lazima tuwe macho tusiuze taifa kwa mkataba mbaya.
Tuna swala hapa la cost / benefit analysis. Kwa kipengele hicho, mimi naona faida ya kuwa na kituo cha jeshi la marekani Tanzania inazidi sana hasara zake. Kenya ina kituo cha jeshi la Marekani. Sidhani hilo limeingilia uhuru wa Kenya.
Sidhani kama Marekani ingetaka kuwa na kituo cha jeshi Tanzania. Kama ingetaka, basi kwa maoni yangu faida yake ingezidi sana hasara zake.
Wako mafundamentalist wengi wasiotaka kusikia chochote kinachohusu Marekani. Tusiwaige bila kufikiria wenyewe maslahi ya taifa letu. Kila shetani na mguu wake.

Haya, siri za ujio wa bushi zinaanza kufichuka. Tunawapeleka vijana wetu wakauliwe huko. Bush anamajeshi kede kede na yanavifaa kede kede vya kisasa kabisa, kwa nini asipeleke jeshi lake?
Kikwete, kama unataka ku-play role ya kulinda amani Darfur, naomba ufanye kama ulivyofanya kwa Somalia, hao wanaotaka kulinda amani waje hapa wafunzwe na usipeleke kabisa vijana wetu huko. Mama yangu weee, tunatumbukizwa pabaya sana na hawa wa Merekani. Eeeh Mwenyeezi Mungu wetu, inusuru Tanzania, wanusuru wa Tanzania na baa hili linalo tunyemelea.
Tumekwisha ingiliwa kwa kupitia mlango wa KIA( Chai Maharage)
Kilicho baki ni kukaza uzi tuimarishe elimu ili Technolojia ikue.
Wazee hao wa kazi wakiingiaga huwa hawatokkagi hata siku moja.
Nyerere alikuwa na uhusiano wa Karibu kabisa na JFK, kwa hiyo si jambo geni wamarekani kuingia na kuweka kambi Tanzania, it was abaout time.
Baada ya kennedy kuuawa Nyerere aligeukia kwa akina Mao.
Kwa muda mrefu tumejifanya eti hatufungamani na upande wowote wakati kuna watu tunawaunga mkono na wengine tunawakandia. Huko ndo kuto fungamana na upande wowote?
NDio maana yake...JK hatimaye amekubali; zile safari nyingi za Marekani tuliambiwa ni kuleta wawekezaji sasa ndio hawa wanakuja na bunduki zao.
Mimi naona hii pengine ni nafasi nzuri kwa dada na kaka zetu kupata watoto wengi tu wenye damu za kizungu...!!
Duh! tulipokuwa JKT hiyo ilikuwa inaitwa "usawa wa gudulia"