BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,083
Mwalimu Nyerere na Wamarekani tangu lini!?
Wamarekani wafunza askari wa JWTZ
Mwandishi Wetu
Daily News; Thursday,February 14, 2008 @00:05
MAREKANI imeanza kutoa mafunzo kwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao watatumika katika shughuli za kulinda amani, imefahamika.
Ubalozi wa Marekani umeeleza katika taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari kwamba mafunzo hayo yalianza Januari 21 katika sehemu ambayo haikutajwa, ikiwa ni mchango wa nchi hiyo katika kutekeleza kwa vitendo ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika kudumisha amani.
"Mwalimu Nyerere alikuwa na ndoto ya kuwa na Afrika ambayo ina amani, yenye utulivu na yenye haki. Alitaka Tanzania iwe mstari wa mbele katika kuhakikisha ndoto hiyo inatimizwa.
"Katika kufuata mfano wake, Rais Jakaya Kikwete anajiandaa kupeleka askari wa kulinda amani katika maeneo kama Darfur na Somalia. Marekani inajivunia katika kumsaidia Rais Kikwete na JWTZ katika kutekeleza nia hiyo," taarifa hiyo ya ubalozi imesema.
Msaada wa Marekani unatolewa kupitia programu inayofahamika kama Acota na unahusisha mafunzo na vifaa kwa batalioni tatu. Batalioni ya kwanza iliyoanza mafunzo Januari inatarajiwa kumaliza mafunzo hayo ya wiki 10 mwishoni mwa mwezi ujao na itakayofuata itaanza Aprili.
Vifaa vinavyotolewa na Marekani katika mafunzo hayo ni vya mawasiliano, jenereta, vifaa vya tiba, vya kuchujia maji na kufahamu eneo (GPS). Kabla ya mafunzo yanayosaidia na Marekani, Tanzania ilikuwa tayari imepeleka Polisi-Wanajeshi 77 huko Lebanon kama sehemu ya Jeshi la Kulinda amani la Umoja wa Mataifa. Nafasi zao zitachukuliwa na askari wengine 85 ambao walifunzwa na Marekani chini ya mpango wa Acota.
Tangu kuanzishwa kwa programu ya Acota zaidi ya wanajeshi 92,000 kutoka Afrika wamefunzwa kuhusu masuala ya ulinzi wa amani na lengo ni kufikisha askari 228,000 ifikapo 2010.
Nchi nyingine ambazo zimenufaika chini ya Acota ni Benin, Botswana, Burkina Faso, Cameroon, Ethiopia, Gabon, Ghana, Kenya, Malawi, Mali, Msumbiji, Niger, Nigeria, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Uganda na Zambia.