Tumefikaje hapa tulipo?

Hakuwa strong! Mbona mwaka 2015 Kikwete alimfuta Lowasa, ni vivyo hivyo Mkapa angeweza kumfuta Kikwete na timu yake yote!
Kikwete alikuwa ana mgombea wake amemuandaa mwenye ushawishi pia, hilo lilichangia kumfuta Lowassa.

Kulikuwa na kundi kubwa lenye nguvu ikiwemo wakongwe wa Ccm waliokuwa hawamtaki Lowassa hilo pia lilichangia..

Mkapa pia alionekana kuwa na nguvu ya ushawishi kuamua nani awe mgombea Urais wa Ccm mwaka 2015, hilo lilichangia Lowassa kufutwa.

Mwaka 2005 mazingira kama ya 2015 hayakuwepo na kama yalikuwepo yalikuwa dhaifu mno kumfanya Mkapa kumfuta JK.

Mtandao wa Mwaka 2005 ulikuwa hatari mno na athari zake mpaka leo tunaziishi.
 
Nimalizie kwa kusema hivi. Katika ule mchoro alouweka Profesa Shivji ni muhimu sana Wananchi tuelewe jambo moja muhimu sana. Ya kwamba sisi tuna WAJIBU kama Wananchi na ndio maana zipo sehemu mbili. Sehemu ya Wananchi akaeleza mambo matatu ambayo ni UHURU, UTU na USALAMA.

Haya mambo matatu, ni YETU sisi wananchi kuyalinda, tusiyatazame hayo kama ni WAJIBU wa UTAWALA bali wetu sisi Wananchi na nimeona kuna baadhi yetu tunadhani ni wajibu wa Utawala kutuhakikishia sisi Uhuru, Utu na Usalama.

Sasa ikiwa wewe mwananchi unashindwa kuulindwa Uhuru wa watu wengine, huthamini UTU wa wenzako wala Usalama wa jamii haukuhusu hii bila shaka hata Utawala utaongozwa na watu wenye akili hizo, wasiothamini misingi hiyo kwa sababu wametokana baina yetu (Wananchi). Matokeo yake hata misingi yao ya Utawala waiwezi kuwaongoza watu wasiojali misingi ya UTU wao.

Hivyo basi Watawala wanatumia mamlaka yao tulowakabidhi kuendelea na mazoea walokuzwa nayo Uraiani kutothamini wala kuheshimu misingi ya UTU wetu sote. Mamlaka alokabidhiwa ni rungu kupambana na watu wa aina yake mwenyewe.

Natamani sana somo hili lingefundishwa shuleni, vyuoni na hata vyama vyote vya Siasa ili kujenga foundation ya vijana wa kesho ili misingi hii iwe ndio mila na utamaduni wetu.

- Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo.
 

Kama wataendelea kuwasikiliza akina Wassira, Butiku na Kabudi. Hii nchi tutaizika rasmi 2030. Hawa wazee wanajari matumbo yao kuliko nchi.
 
Swali kwako, ufisadi wa Lowasa ulithibitika au ilibakia kuwa maneno tu??

Pia kwanini unazunguuka sana mbuyu na kushindwa kusema viongozi wa ccm ndio wametufikisha hapa tulipo??

Nakubaliana kabisa na wewe khs mmomonyoko wa maadili kwa viongozi hasa kwy kujilimbikizia mali na ccm kuachana na suala la maadili ya uongozi.
Hicho ndio chanzo cha minyukano na dharau ndani ya ccm, kisha wakatoka nje na kufanya watakavyo bila kujali wananchi ndio wenye nchi.
 
Ushahidi wa Lowassa waulize Chadema maana Dr.Slaa alimtaja 2007! Halafu ndugu yangu kuna kesi gani ya Ufisadi wa viongozi ambayo wewe unaijua ilithibitishwa?

Maswali mengine bana khaaa!
 

And what we see is the beginning of the end of 2005 legacy . Mtoto wa mjini style na ujanja ujanja wake, umefeli. Imebakia kutumia nguvu na kutapatapa. Kuzima watu wasikiri.

The power behind 2005 culmination, combined very ambitious people,, with the appetite and desire to get rich quickly. In the process, they have not been able to produce the rightful successors of the throne.

Hapa tulipo tuna changamoto sio za kitoto. Udini umeshamiri kweli kweli. Maadili ya utumishi wa umma yamepungua. Kutokujari na kutiowajibika ndio imekuwa fashion.

Mwenye macho haambiwi ona....tumeanza kukwama kidogo kidogo. Hatutaweza kuendelea mbele tukiwa isolated au kama tumekuwa kisiwa
 

Sio siku nyingi wataparurana mpaka waite maji mmma 😂 😂 😂 😂 . Wanabadilisha spe taili tu..zile kuuukuu
 
Ushahidi wa Lowassa waulize Chadema maana Dr.Slaa alimtaja 2007! Halafu ndugu yangu kuna kesi gani ya Ufisadi wa viongozi ambayo wewe unaijua ilithibitishwa?

Maswali mengine bana khaaa!

Nilifikiri lengo la uzi huu ni kujadili tumefikaje hapa na tutokaje.
Kumbe ni fursa za Wamajalalani kama kawaida yao. Haya vumisha ngoma usikike wakukumbuke.
 
Wacha maelezo mengi alie tufikisha huku ni magufuli mzee wa chato yule fala

Maana ata kipind cha mkapa au JK katiba ilikua ni hii hii na maisha yalienda ila baada ya magufuri kuingia ndo chanzo cha mattzo meng kuanza

Katiba ilikua mbaya ila viongozi walikua na uwoga na aibu na hawakutaka kujaribu vitu visivyo takiwa kujaribu ila baada ya jiwe kuingia ndo mattzo yote yalipoanzia

Yule muhuni Mungu mnrahani na uko kaburini Mungu amuongezee matesa na ata sku ya kufufuka zege ya kaburi lake isipasuke fala sana yule
 
Unazunguka sana; mwanzo wa tatizo ni Samia na Kikwete na mwisho wake ni Samia na Kikwete, majizi makubwa haya
 
Profesa Mkandara taifa hili limejaliwa kuwa na viongozi wengi wenye busara lakini inashangaza busara zao hazithaminiwa na maCCM. Laiti maCCM wangekuwa wanachota nondo kutoka kwa viongozi wastaafu, nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo.
 
Mpaka leo sielewi hivi tunachong'ang'ania kwa zanzibar ni kipi? Kwamba kuna rasilimali gani ambayo bara hamna mpaka tulazimishe muungano.

Zamani nilitaka serikali tatu ila kwa sasa ni bora serikali moja tu zanzbar iwe mkoa au waondoke kwenye muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…