Huu ni uongo wa mchana. Hata shetani "baba wa uongo" atakubaliana na mimi. Tundu Lissu katika mikutano yake hakutamka hata neno moja la kuitukana nchi.
Nilimsikiliza Lissu kwa makini sana. Ukimsikiliza vizuri ni lazima utaingiwa na chembechembe za ufahamu kuhusu uzalendo wa kweli. Ninamwombea apone haraka na akipona tumhamasishe afanye ziara ya pili kabla ya kurudi kugombea Urais.
Kama mchango wangu katika kukuza uzalendo nime-download hizo hotuba alizotoa zote. Nina mpango wa kuzisambaza huko mtaani vijana wamsikilize wajifunze uzalendo.
Ninaamini miaka michache ijayo vijana wazalendo watakuwa wanazitafuta huko YouTube wamsikie huyu nguli wa sheria na mwanaharakati wa kipekee katika ukanda huu.
Nadhani kwa Afrika Nzima karne hii ya 21 Tundu Lisu amekua Sauti ya kupinga Ukoloni wa Mtu Mweusi kumtawala Mwafrika Mwenzake Kikatili bila kujali maumivu yake. Watawala wa Kiafrika wanatia aibu sana kwa wanavyoshindwa kujenga mifumo bora ya kisiasa na kijamii na kiuchumi.
Yanayofanyika Tanzania kisiasa hayakua na ulazima wowote kama Katiba ingefuatwa na kiheshimu maamuzi ya wapiga kura.
Utawala huu ulikua na nafasi nzuri sana ya kufanya mambo mazuri na kupata heshima kubwa sana kama ungesimamia katiba na sheria nyingine kama zile za Uchaguzi. Kung'ang'ania kuilinda CCM na makada wake wenye tuhuma nyingi matokeo yake yanaligharimu Taifa.
Awamu yetu hii ilikua na uwezo wa kuunda katiba bora na kuleta maendeleo makubwa sana na baada ya muda wao kuisha wanheheshimika sana na kuenziwa kwa pale watakapoishia kuliko kuwaza kuifanya dunia kuwa pepo kwa kuwagawanya watu kwa makundi huku watawala wakiwa daraja la juu sana na wenye mamlaka na maamuzi kama miungu na mwisho wa yote wakaishia kushitakiwa na kumalizia maisha yao duniani kwa vifungo gerezani.
Hata kwenye kutafuta maisha kuna watu wanaotafuta fedha kwa udi na uvumba huku wakiumiza wengine kwa dhulma,rushwa na utapeli alimradi wapate fedha nyingi. Hii sio sawa katika maisha bora ya binadam wenye utu . Wachamungu watakataa na kusema bora kupata fedha kidogo kwa halali bila kuumiza wengine kuliko kupata nyingi kwa kuumiza wengine.
Asili ya binadamu ni binadam na ameumbwa na Mungu.Na haijawahi kutokea mtawala akatenda anavyotaka yeye bila kupingwa na binadamu wenzake na mwishowe akapoteza umaarufu na hata kuporomoka kisiasa.
Serikali ingemtibu Lisu na kuonyesha ushirikiano wa kukerwa na majangili yasiyojulikana yaliyotaka kumuua Lisu kama wanavyokerwa na majangili yanayoua Tembo nadhani Lisu asingelalamika kama anavyolalalamika kwa majirani baada ya kuona wazazi hawamjali na wanahamasisha asipewe hata chakula ( mshahara wake).
Serikali ikitaka kujisafisha ianze kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Na ikiwezekana viongozi wa dini wajitolee kuiunga mkono kwa kuwa waangalizi wa mwenendo mzima wa uchaguzi serikali za mitaa ili wakiwaombea watawala basi wamwambie Mungu ukweli. Mana huwezi kutubu dhambi usiyoijua au kudhani kuwa umekosea.
Lisu ni mwanga mpya wa Tanzania na Afrika. Tunajivunia kuwa Taifa letu kuwa na MTU huyo Tundu Antipasi Lisu. Ameitangaza nchi kwa Muda mfupi.
Mungu ampe Lisu nguvu na uponyaji na ulinzi dhidi ya wenye uchu wa madaraka na Vyeo na husuda.
Sent using
Jamii Forums mobile app