Tumeanza kula matunda ya mikutano ya Tundu Lissu Ulaya na Marekani

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,794
2,000
Tundu Lissu akiwa huko Ulaya na Marekani ameichafua sana na kuitukana sana nchi yetu na uongozi wake na baadhi ya wafuasi wake wakishangilia na ku support mikutano hiyo.

Maongezi aliyoyafanya Mhe Tundu Lissu lazima tu yazae matunda na wapo wataofaidi na pia ambao hawatafaidi mikutano hiyo.

Hongereni wale mnao anza kula matunda ya mikutano hiyo maana ilikuwa mikutano muhimu sana kwenu.
 
KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
763
1,000

Huu ni uongo wa mchana. Hata shetani "baba wa uongo" atakubaliana na mimi. Tundu Lissu katika mikutano yake hakutamka hata neno moja la kuitukana nchi.

Nilimsikiliza Lissu kwa makini sana. Ukimsikiliza vizuri ni lazima utaingiwa na chembechembe za ufahamu kuhusu uzalendo wa kweli. Ninamwombea apone haraka na akipona tumhamasishe afanye ziara ya pili kabla ya kurudi kugombea Urais.

Kama mchango wangu katika kukuza uzalendo nime-download hizo hotuba alizotoa zote. Nina mpango wa kuzisambaza huko mtaani vijana wamsikilize wajifunze uzalendo.

Ninaamini miaka michache ijayo vijana wazalendo watakuwa wanazitafuta huko YouTube wamsikie huyu nguli wa sheria na mwanaharakati wa kipekee katika ukanda huu.
 
Mshangai

JF-Expert Member
Feb 16, 2008
455

Sikia we Dada , kushindwa kutofautisha Serikali na Taifa ni sawa na wewe ushindwe kutofautisha mbele na nyuma hivyo uhisi kuna matumizi sawa kisha waelewa wakuambie unatumika kinyume na maumbile.
Nadhani wewe na wenzako hapo umeona tofauti ya Serikali ya ccm na Taifa Tanzania!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Download na kuanza kuzisambaza mchana kweupe....karibu sana
 
tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,794
2,000
Sikia we Dada , kushindwa kutofautisha Serikali na Taifa ni sawa na wewe ushindwe kutofautisha mbele na nyuma hivyo uhisi kuna matumizi sawa kisha waelewa wakuambie unatumika kinyume na maumbile.
Nadhani wewe na wenzako hapo umeona tofauti ya Serikali ya ccm na Taifa Tanzania!

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi na wewe unajiona mjanja kisa Lissu kasema tofauti ya Serikali na Taifa.....hujui kama Taifa ni Serikali pia.Wewe unafikiri Rais anawakilisha nini anapoenda nje ya nchi kwenye mikutano ya Kimataifa mfano anapokuwa pale UN huwa anatoa msimamo wa nini Taifa au Serikali au pale anawawakilisha wakina nani? jitambue Lissu anakulisha matango mwitu na wewe unachekelea ili akiwa huko nje aonekane hawasemi watanzania au halisemi taifa......Serikali ni Taifa na Taifa ni Serikali.
 
KWADWO ABIMBOLA

JF-Expert Member
Jan 8, 2019
763
1,000
Do that hakuna shida ...tunasuburi tusikie hizo hotuba kwenye CD na hizo ring tone zenu
Tayari zipo zimejaa YouTube. Kwa sasa ni kuwatumia wale wasiokuwa na internet. Hata tukitembea vijijini tunawapa wa huko nao wasikilize.

Sijui unawaza nini unaposema unasubiri wakati na wewe pia tayari ulishamsikiliza. Tatizo lako ni kukaza shingo na kuikataa dozi ya uzalendo kutoka kwa jembe letu Tundu Lissu.
 
tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,794
2,000
Tayari zipo zimejaa YouTube. Kwa sasa ni kuwatumia wale wasiokuwa na internet. Hata tukitembea vijijini tunawapa wa huko nao wasikilize.

Sijui unawaza nini unaposema unasubiri wakati na wewe pia tayari ulishamsikiliza. Tatizo lako ni kukaza shingo na kuikataa dozi ya uzalendo kutoka kwa jembe letu Tundu Lissu.
hata zipo kwenye youtube hakuna shida....wewe anzisha mradi wako wa kuweka kwenye CD na kuzisambaza
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom