Tumealikwa kwenye maandalizi uchaguzi mkuu Kenya 2012.....Je,wanasiasa Tunaweza kujifunza kitu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumealikwa kwenye maandalizi uchaguzi mkuu Kenya 2012.....Je,wanasiasa Tunaweza kujifunza kitu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Jul 30, 2011.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Siasa za Kenya zimepamba Moto uchaguzi mkuu utafanyika Mwakani.inaonekana uchaguzi huu umepaniwa sana na vyama vya siasa na wagombea Urais wako serious kweli kweli.
  Nimepata Mwaliko kutoka kwa kambi moja ambayo hadi sasa ina Nguvu sana.Miongoni mwa vijana Saba kutoka baadhi ya nchi za kiafrika akiwemo Mwenyekiti wa Vijana wa ANC ya Afrika kusini julius Malema,Msemaji wa umoja wa vijana wa ANC Floyd Shivambu, Adams atoh okafo wa Ghana na aliyekuwa Rais wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Nigeria Kenneth Orkuma Hembe wamealikwa kwa ajili ya kusaidia katika maandalizi ya awali katika kuweka mkakati wa jinsi ya kuvuna kura za vijana ambao wameonekana ndiyo mtaji mkubwa kwa wagombea urais 2012

  Je,kama ingekuwa Tanzania CCM ingeweza kuruhusu jambo kama hili kama ingetokea upinzani wakaalika watu kutoka nje kwa ajili ya issue kama hizi? Je,wanasiasa na wadau wa vyama vya upinzani tunaweza kukusanya mawazo au tactics beyond borders pengine hata kwenda mbali zaiki na ku-hire political tacticians kama akina Dick Morris ili kuimarisha mbinu na mikakati ya kisiasa kipindi cha uchaguzi mkuu?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  You never know until you try kaka. Vyama vya upinzani Tanzania vimesha jaribu kufanya kitu kama hicho?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,476
  Likes Received: 19,872
  Trophy Points: 280
  katiba inaruhusu?
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Labda nahitaji kuelimishwa mkuu. Kuna sehemu maksusi kwenye katiba ina kataza? Kumbuka kisheria kama kitu hakija katazwa na katiba basi ni halali. Kwa hiyo unless kama katiba ime kataza directly or indirectly kitu kama hicho sioni neno. Ila I could be wrong.
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Pengine wanaweza kuwabana kwa kutumia aina ya visa waliyokuja nayo....Mwaka 2007 serikali ya Kenya ilimtaka Dick Morris campaign advisor and strategist wa Raila Odinga kuondoka Kenya kwa sababu ali-misuse tourist visa yake kwa ajili ya Siasa.Hiii ilikuwa ni baada ya serikali kugundua kwamba Financial statement ya ODM ya Mwaka 2006 ilionyesha kiasi cha Us Dollars 250,000 kwa ajili ya kumlipa Dick Morris.Pia waliona nongwa zaidi ilipoonekana Senator Mmoja wa US alimchangia Raila Odinga kiasi cha US Dollars 1,000,000

  Sasa mambo kama hayo hapa kwetu yapo ndiyo maana ukiangalia ile Electorate expenses act 2010 ilitungwa sio kudhibiti matumizi ya funds bali ilikuwa kudhibiti sources of funds na ililenga kubinya Upinzani zaidi.Suala la Membe kuwatisha tisha mabalozi na kupotosha Azimio la vienna la mwaka 1961(vienna convention) ni kiashiria tu
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,519
  Likes Received: 5,660
  Trophy Points: 280
  kenya raia wao wanauelewa mkubwa sana sababu ya elimu.hapa tz tukitumia hao wataalamu wa nje chama tawala watawahadaa raia,fikiri tutumia mapesa kuwalipa kama kenya tutaeleweka kweli ben?
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,519
  Likes Received: 5,660
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kufanya watz wawaelewe na si sheria.majibu ya maswali mengi yawe tayari.hasa gharama kubwa kutafuta madaraka n.k
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,519
  Likes Received: 5,660
  Trophy Points: 280
  pia nafikiri kama vijana inabidi tubuni mbinu zetu kama watz ambazo zitatuweka huru na sio kuja kuwatumikia wengine ukiwa madarakani.kwanini kampeni za enzi za mwalimu tusizitumie na kuziboresha tu wakuu?
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ya kujifunza yako mengi ingawaje context ya Kenya ni tofauti na hapa kwetu; mojawapo ni jinsi wenzetu wanavyojenga alliances wakati wa uchaguzi, hili ndio tatizo letu kubwa vinginevyo ccm ingekuwa historia.
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nadhani mfumo wa ubepari unawasaidia sana.....leo hii kuna Aspirant mmoja wa Urais ameshaweka budget Estmate ya Kshs 8 Billion.Sasa ( Bilioni 8 X 20 = 160 ) kwa hela za Tanzania 160,000,000,000 ni zaidi ya budget yetu ya mambo ya nje karibia mara moja na nusu.

  Kweli wananchi wana uelewa mkubwa Kenya,na pia siasa zao bado zina influence ya ethnicity ndiyo maana inabidi kutumia gaharama kubwa kweli kweli ili kupata supporters wa kutosha


  Sisi Tanzania inabidi tutumie mkakati wa hali ya juu uchaguzi ujao,tuwe na secretariet makini uchaguzi ujao.Alliance inayohitajika ni ku-pull in the civil society groups,watu wenye influence kwa wafanyakazi,wakulima,na most importantly big fraction of voters block vijana.ni lazima tuanze maandalizi mazito.Ni lazima tuingie kwenye nyoyo za matabaka ya chini na ya kati.Hii sensa ya mwakani inabidi tucheze nayo sana kimkatai kabla ya kupata data mpya za daftari la wapiga kura 2014.Hapa kwetu kazi tukiifanya agressively,bila shaka tuna uwezo wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 70%

  Wenzetu wanajua sana kujenga alliances, naona Willium Kipchirchir Ruto anaiga sasa style ya kujenga alliance ya Raila Amolo Odinga.Kambi yake ya coastal Region iliyokuwa inaongozwa na Najib balala imepata pigo,Amegeukia kambi ya Raila odinga.Kwa vyovyote turufu aliyonayo ni kupata support kutoka kwa akina John Michuki,Sally kosgei,Prof.sam Ongeri kwa sabau wakisii hawana imani8 sana Raila,Nicholous Biwot incase Uhuru Kenyatta akiamua kuunga alliance nyingine,Eugene wamalwa na akina Martini shikuku ili kupata support kubwa ya the populous ethnic group ya Waluhya,Kalonzo Musyoka yeye hakuna mwanasiasa atakayemuamini tena coz hana tofauti na Jk kwa kucheza siasa za Usaliti na hatabiriki
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ben; Najib na Amolo hawezi kutupata hata siku moja ingawa mara zote mwanzoni ujifanya hawapo pamoja ili kuweka mambo yao sawa, hawa ni watu wamekuwa pamoja kwa siku nyingine na pia wameonja wote kwa pamoja mateso ya Serikali iliyokuwa ya Kidhalimu ya KANU

  Ebu nipe tathimini ipo vipi huko maana nipo mbali kidogo na kujuwa siasa za huko
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wangeitwa magaidi!!
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Arafat thanks,

  Ni kweli mkuu,nadhani Ruto alikuwa amedanganyika baada ya kuona Mbunge wa Mvita Najib Balala amekaa pembeni .....Kwanza hata kama Najib Balala alikuwa na mpango wa ku-switch off kwenye camp na kuhamia nyingine angepoteza zaidi kwa sababu Raila Odinga ana influence sana Coast.Pia tayari Raila alikuwa na wabunge wengine ambao angeweza kujenga nao alliance kule coast na kuwajengea capacity na kuifanya secretariat ya kule bila kuonyesha ana strategy gani huko mbele

  Juzi matokeo ya kura ya maoni ya Synovate yalikuwa hivi

  Raila Amolo odinga----------------------------32%

  Uhuru Kenyataa--------------------------------21%

  Stephen Kalonzo musyoka--------------------11%

  Willium Kipchirchir Ruto..............................11%

  Martha karua-------------------------------------5%

  Eugene Wamalwa--------------------------------3%

  Kalonzo Musyoka ana influence ya kura za Wakamba,Uhuru kenyatta wakikuyu ambao pia kuna Martha karua,Wakalenjini kuna Ruto,Waluhya kuna Eugene wamalwa ambaye hana nguvu kivile isipokuwa anabebwa sana na jina la ukoo wa aliyekuwa Makamu wa Rais the Orator guy Michael kijana Wamalwa

  kuna wanasiasa machachari ambao ni vijana kama akina peter Kenneth,huyu anaweza kuwa mshirika mwenye manufaa kwa kambi yoyote kati ya kambi ya Raila odinga,Ruto,kenyatta kama atakuwa camp tofauti na Kenyatta
   
 14. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Tycoon Moi yamkini anamuunga mkono Uhuru kwa nguvu zote, sasa hapo kuna hatari kubwa kwa Kamanda wangu Raila, maana najuwa Moi anaweza kumnunua Kalonzo kuungana na Uhuru then watashuti sana kwenda juu, Bado kuna haja kubwa sana ya kuwasuluhisha Ruto na Amolo ili wawe kambi moja kama wanahitaji ushindi wa nguvu kama ule ulioporwa last time. Martha najuwa wazi atakuja kuumga Raila Mkono mwishoni maana mambo ambayo Kibaki alimfanyia hakutegemea wakati alifanya kazi kubwa sana katika uporaji wa ushindi wa ODM, wazee wafute jinsi ya kuwasuluhisha Raila na Ruto.
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,927
  Likes Received: 12,133
  Trophy Points: 280
  Unaonekana uko in touch sana na siasa za Kenya kuliko za nyumbani na chama chako vipi Igunga utaenda lini kusaidia.
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Arafat,

  Kundi la G-7 litasambaratika kwa sababu habari za ndani ni kuwa tayari Ruto anataka Uhuru amuunge mkono kwani mwaka 2002 yeye ndiye aliyemuunga mkono Uhuru.Raila Odinga mkakati wake wa alliance naupenda sana and we have alot to learn from him.

  Siasa za Godfatherism zina influence bado na Moi bado ana influence kwa aspirants wa Urais inagawa si kwa nguvu sana kama olusegun obasanjo wa Nigeria na PDP yake. Si unajua sasa hivi nick name yake ni master-rigger.

  Kambi ya G-7 ya akina Uhuru,ruto,wamalwa,kalonzo,Dualle,Balala ambaye tayari amewa-turn off inategemea kumuweka front Eugene wamalwa kama mambo ya akina Ruto na kenyatta yatakuwa tight kule ICC.Uhuru ana nguvu sana Cental na mkoa wa bonde la ufa (rift valley province) ukilinganisha na kalonzo Musyoka.Wataweza kumtumia Eugene wamalwa kama mgombea urais ili kupata kura nyingi kutoka kwa waluhya wenye idadi kubwa bado ya wapiga kura huko western province.Huko inabidi wamtumie Cyrus jirongo kama kiongozi wa kuratibu secretariat yao

  Hata hivyo kambi ya Raila Odinga inabidi imtumie musalia Mudavadi huko kuwagawa kupata support ya waluhya.Kama akina Ruto wataona hali imekuwa tight na wakishindwa kuelewana wakagawanyika kila mmoja akagombea independently basi mostlikely uchaguzi huo wa urais utaingia kwenye run-off.Sasa itakuwa Rahisi kwa Ruto na akina Uhuru kenyatta kufanya tactic alliance kwenye pigo la mwisho

  Hata hivyo,Kambi ya Raila inabidi ifanye alliance safari hii strategilly kuahkikisha wanapata ushindi mzito wa first round tu ama sivyo inabidi waweke reservation ya political concession kwa wale supporters wa mwisho strategically incase of run-off.Race ya two horses affairs itakuwa na manufaa zaidi kwa Moi na akina John Michuki kwa sababu wao watakuwa kwenye position nzuri zaidi kushawishi na kuingia kwenye makubaliano kwa manufaa yao.Hapo ndipo utakapowaona hata akina Simeone nyachae wamefufuka na kumwaga resources
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Quinine,

  Unaweza kuwa sahihi kutegemeana na kipimo ulichotumia kufikia conclusion....hata hivyo Tanzania sio kisiwa.Kila kitu na muda wake.........! ! !
   
 18. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kimsingi Raila Odonga is more popular kuliko wagombea wengine wote na anatarajiwa kushinda kwenye round ya kwanza ya uchaguzi, lakini kikwazo kikubwa kwake ni hali halisi kuwa hawezi kufikisha 50% ya kura zote katika round hiyo na hivyo marudio ya uchaguzi kwa washindi wawili wa juu ni kitu kinachotarajiwa....

  Raila Odinga katika uchaguzi wa 2007, aliungwa mkono sana kwenye maeneo yenye population ya kutosha kumpa uraisi ya Nyanza-Kwao, Nairobi, Rift Valley kwa Rutto na Western-Luhya kwa Mudavadi na kushindwa?? na Kibaki,..lakini kueleka 2012 Raila Odinga hana ushawishi tena kwenye eneo muhimu la Rift Valley na ana changamoto kubwa kwa Waluhya hasa kutokana na kupungua kwa ushawishi wa Mudavadi kwa kuonekana mtu dhaifu asiye na ambitions za kuwa raisi na wakati huohuo kuibuka kwa kijana Eugen Wamalwa anayeonekana kuelekea kumfunika Mudavadi kwenye siasa za Luhya, time will telll...

  Kutokana na siasa hizi za kikabila, mkakati wa G7 ni kuunganisha nguvu kwa yeyote miongoni mwao atakayeshika nafasi ya pili na kushirikiana as a team kwenye uchaguzi wa marudio dhidi ya Raila, na hapa ndipo uwezekano wa Raila kushindwa unapokuwa mkubwa kutokana na population kubwa ya wapiga kura iliyo nyuma ya umoja wa G7 inayobebwa zaidi na Central-Uhuru, Rift Valley-Ruto, Kalonzo-Eastern, na toss-up Luhya, time will tell...

  Challenge, je G7 itasurvive mpaka kwenye uchaguzi? je Wakikuyu watakuwa tayari sasa kumpigia kura mgombea asiye Mkikuyu incase Uhuru Kenyatta atakuwa na kesi ya kujibu Hague au kama hatashika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa awali? bado hawana historia hiyo...na je kama maGiant wote wa G7 watagombea uraisi, vipi ushawishi wa ma-Vice Presidential candidates kwenye maeneo wanayotoka (ukiondoa Central-No way kwa Raila) hasa kwenye runn-off?

  Vyovyote itakavyokuwa, uchaguzi ujao ni kura ya maoni ya kupendwa na kuchukiwa kwa Raila Odinga, kisiasa amefanya kosa kubwa sana kuipoteza Rift Valley, binafsi nampa nafasi kubwa Raila kushinda kwenye round ya kwanza, na kisha kushindwa kwenye round ya pili, na hivyo serikali ijayo ya Kenya kuundwa na G7...
   
 19. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu Arafati...

  Japo kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu lakini unless utokee muujiza hakuna uwezekano wa Ruto kumuunga mkono Raila na wala hakuna uwezekano wa Kalonzo kuungana na Raila katika uchaguzi ujao, Martha Karua pamoja na kuwa amegoma kujitoa kugombea kumwachia Uhuru ili kuunganisha nguvu za mkoa wa Kati-Wakikuyu, zaidi sana hawezi kujitoa kwa ajili ya Raila japo ata akifanya hivyo hana effect kubwa kwa sababu anatokea kwenye jamii ambayo ni himaya ya Uhuru Kenyatta na hasimu wa Waluo na Raila...

  Wote Moi, Kibaki, Ruto, Uhuru na Kalonzo wanaunganisha na kitu kimoja, kumzuia Raila Odinga kuwa the most powerful person in Kenya..., anachopaswa kufanya Raila ni kujaribu kumvuta Eugen Wamalwa kwenye wing yake na wakati huohuo am-maintain Musalia Mudavadi, hii itamhakikishia support ya block muhimu ya Waluhya.
   
 20. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ben. Maneno yafuatayo umeyatumia kwa kuyabebesha maana gani
  1. Mkakati wa kuvuna kura za Vijana
  2. Wameonekana kuwa Mtaji Mkubwa
  3. Political tacticians
   
Loading...