Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
- Thread starter
- #21
Kimsingi Raila Odonga is more popular kuliko wagombea wengine wote na anatarajiwa kushinda kwenye round ya kwanza ya uchaguzi, lakini kikwazo kikubwa kwake ni hali halisi kuwa hawezi kufikisha 50% ya kura zote katika round hiyo na hivyo marudio ya uchaguzi kwa washindi wawili wa juu ni kitu kinachotarajiwa....
Raila Odinga katika uchaguzi wa 2007, aliungwa mkono sana kwenye maeneo yenye population ya kutosha kumpa uraisi ya Nyanza-Kwao, Nairobi, Rift Valley kwa Rutto na Western-Luhya kwa Mudavadi na kushindwa?? na Kibaki,..lakini kueleka 2012 Raila Odinga hana ushawishi tena kwenye eneo muhimu la Rift Valley na ana changamoto kubwa kwa Waluhya hasa kutokana na kupungua kwa ushawishi wa Mudavadi kwa kuonekana mtu dhaifu asiye na ambitions za kuwa raisi na wakati huohuo kuibuka kwa kijana Eugen Wamalwa anayeonekana kuelekea kumfunika Mudavadi kwenye siasa za Luhya, time will telll...
Kutokana na siasa hizi za kikabila, mkakati wa G7 ni kuunganisha nguvu kwa yeyote miongoni mwao atakayeshika nafasi ya pili na kushirikiana as a team kwenye uchaguzi wa marudio dhidi ya Raila, na hapa ndipo uwezekano wa Raila kushindwa unapokuwa mkubwa kutokana na population kubwa ya wapiga kura iliyo nyuma ya umoja wa G7 inayobebwa zaidi na Central-Uhuru, Rift Valley-Ruto, Kalonzo-Eastern, na toss-up Luhya, time will tell...
Challenge, je G7 itasurvive mpaka kwenye uchaguzi? je Wakikuyu watakuwa tayari sasa kumpigia kura mgombea asiye Mkikuyu incase Uhuru Kenyatta atakuwa na kesi ya kujibu Hague au kama hatashika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa awali? bado hawana historia hiyo...na je kama maGiant wote wa G7 watagombea uraisi, vipi ushawishi wa ma-Vice Presidential candidates kwenye maeneo wanayotoka (ukiondoa Central-No way kwa Raila) hasa kwenye runn-off?
Vyovyote itakavyokuwa, uchaguzi ujao ni kura ya maoni ya kupendwa na kuchukiwa kwa Raila Odinga, kisiasa amefanya kosa kubwa sana kuipoteza Rift Valley, binafsi nampa nafasi kubwa Raila kushinda kwenye round ya kwanza, na kisha kushindwa kwenye round ya pili, na hivyo serikali ijayo ya Kenya kuundwa na G7...
Kwa waluhya bado inaonekana Eugene wamalwa kupitia nafasi yake ya kamati ya mambo ya nje na ulinzi alihusika kumkaanga waziri wa mambo ya nje Moses Wetang'ula.Waluhya bado wana hasira naye .Ni lazima ODM iwakumbushe waluhya at the same time iwaonyeshe kwamba wanataka Kenya moja isiyo na ukabila
Kundi la G7 lityasambaratika kutokana na Ruto na uhuru kutokuwa na vision kwanza wanapata backup kutoka kwa Saitoti ambaye hajawaeleza wakenya kuhusu uhusika wake kwenye Goldensberg scandal