Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,627
- 46,272
Mojawapo ya vigezo, tunu na utamaduni muhimu wa demokrasia ni ushindani wa haki wa wagombea kupitia sanduku la kura. Kunapokosekana huo ushindani demokrasia inakuwa imekanyagwa na kusiginwa. Kwa msingi huo Tume ya taifa kuwa na mamlaka ya kuengeua wagombea ni kosa kubwa sana katika mchakato wa kidemokrasia.
Ni wakati sasa tume ya taifa kuondolewa hayo mamlaka ya kuengeua wagombea na yapewe kwa mahakama. Kama kuna dosari yoyote kwa mgombea basi wagombea wenzake, wanachi au serikali ikafungue kesi mahakamani na mgombea husika apewe nafasi ya kujitetea kupitia wakili. Wakati haya yanafanyika mahakamani uchaguzi wa nchi, jimbo, kata au mtaa husika usimame mpaka maamuzi ya kesi yafikiwe na mahakama.
Taasisi na mifumo yetu ina matobo mengi sana yanayoikwamisha nchi kuwa demokrasia halisi, inahatijika kazi ya ziada kuondokana na demokrasia ya kiini macho "sham democracy", suluhu ya kudumu ya haya yote ni Katiba Mpya.